Tuesday, September 18, 2012

WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI MKOANI IRINGA LEO

Waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake wakati wa wa uzinduzi wa wiki ya Nenda kwa usalama barabarani iliyozinduliwa leo mkoani Iringa katika Uwanja wa Samora mjini Iringa huku viongozi mbalimbali wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na mabaraza mbalimbali kutoka mikoani wakihudhuria katika muzinduzi huo.
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dk Emmanuel Nchimbi akipokea Mordem ya Airtel kutoka kwa meneja uhusiano wa kampuni ya Airtel Bw. Jackson Mbando wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mjini Iringa leo, Katika picha katika ni wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri wa mambo ya ndani Sirima Pereira na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma.
 
Naibu Waziri wa mambo ya ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama barabarani Taifa Mh. Sirima Pereira akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Usalama barabarani mkoani Iringa leo
 
Wanafunzi mbalimbali wakiwa wamekaa wakiangalia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri katika uzinduzi huo.
 
 
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Dk Emmanuel Nchimbi akimkabidhi Cheti Bw. Beda Meneja wa Airtel Kanda ya Nyanda za juu kusini kwa mchango wa kampuni hiyo katika maadhimisho hayo.
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dk Emmanuel Nchimbi akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Dk Cheristine Ishengoma, wakati akiwasilisha salama za mkoa wa Iringa katika maadhimishi ya wiki ya Nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
 
Viongozi mbalimbali wa mabaraza ya Usalama Barabarani na mgeni rasmi wakiwa kwenye meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi huo
 
 
Banda la polisi linavyooneekana
 
 
Brasi Bendi yailiyoongoza maandamano hayo.
 
Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani mkoani Iringa Salim Ahmed akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama barabarani Taifa na Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mh. Sirima Pereira wakati alipowasili katika uwanja wa Samora.
Maafisa mbalimbali wa kikosi cha usalama barabarani kutoka makao makuu nao wamekuwepo katika maadhimisho hayo ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani mkoani Iringa mara baada ya kuwasili katika uzinduzi huo kwenye uwanja wa Samora.
 
Kutoka kulia ni Theresia Kimaro Mkaguzi wa polisi kutoka makao makuu ya Trafiki, Insp. Zauda Mohamed, Insp Kurthum Bambo na Insp. Agatha Isaack wakiwa katika maadhimisha hayo mkoani Iringa leo
 
Mkaguzi Msaidizi kutoka kikosi cha Zimamoto Puyo Nzalayaimisi akimpa maelezo Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Sirima Pereira wakati alipotembelea bada la kikosi hicho, kulia ni Kamanda kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga
 
Mh Sirima Pereira akipita katika banda la Polisi, aliyeongozana naye ni kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani Mohamed Mpinga
 
Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Emmanuel Nchimbi akipata maelezo kutoka kwa katika banda la polisi kutoka kwa Ispekta Abel Bartazar Swai. kulia ni Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
 
Askari wa kikosi cha kuzima moto akimuokoa mmoja wa majeruhi wa mfano katika ajali baada ya kufanikiwa kukata milango ya gari na vifaa maalum ambamo majeruhi huyo alikuwa amenaswa na vyuma.
 
Mmoja wa wasanii wa Kikundi Mizengwe akiigiza kama trafiki katika maadhimisho hayo
 
Ahmed Omary Kasu meneja Masoko wa kiwanda cha maziwa cha ASAS DAIRIERS LTD cha Iringa akimpa maelezo Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Sirima Pereira wakati alipotembelea katika banda hilo na kuona shughuli zao.
 
Waziri wa Mambo ya ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa uhusiano wa SUMATRA Bw David Mziray wakati alipotembelea katika banda hilo leo katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama Barabarani mjini Iringa leo, katikati ni Ahmad Kilima kaimu mkurugenzi wa SUMATRA.

No comments: