Monday, January 28, 2013

Malaika Orphanage Foundation yakaribisha wadau kusaidia kituo

 Wikiendi hii Mkurugenzi na muasisi wa kituo cha kulelea watoto yatima,kinachoitwa Malaika Orphanage Foundation,  Rahma Manji(Pichani kushoto) alipokea msaada kutoka kwa mwambata wa jeshi kutoka nchini Ujerumani, Bw Abel Gunta(Pichani kulia) ambaye aliguswa na moyo wa mwenyekiti huyo aliyemua kuanzisha kituo cha kusaidia watoto baada ya yeye mwenyewe kujikuta akilea watoto wengi wa ndugu zake kwa sababu mbali mbali takriban miaka 1o iliyopita
 Abel ambaye aliambatana na mkewe walitoa vifaa vya zahanati vikiwemo vitanda na madawa ambavyo kwa ujumla wake, vimegharimu fedha za kitanzania shilingu milioni 10. Hapa Gunta akimkabidhi Bi Manji msaada wa madawa huku mkewe Nana, ambaye aliambatana naye akishuhudia
 Vaeni watoto...
 Gunta pia alikabidhi fulana ambazo zitatumika kama sare baada ya masomo kwa watoto hao, hapa akishiriki katika kuwakabidhi watoto wenyewe. Kituo hicho kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani kina watoto 61 wanaoishi hapo huku 48 wakiwa wanasoma za msingi zilizopo wilayani Mkuranga, saba shule ya Sekondari na waliobaki wakiwa hawajafikia umri wa kwenda shule
Hii ni picha ya pamoja ya wanakituo
Chuo kinakabiliana na changamoto mbali mbali katika kipindi hiki ambacho bado hawajakuwa na miradi ya kujiendesha, vitu kama mavazi, chakula, ada za watoto ambao wanasoma nje ya Kituo, na waalimu wa kujitolea kuwafundisha watoto masomo ya ziada baada ya saa za masomo.
Kufuatia hilo unakaribishwa kutembelea Kituo na kujionea mwenyewe hali halisi na kutoa chochote utakachojisikia iwapo utahamasika.
namba ambayo unaweza kupiga pia ili kupata maelekezo zaidi ni  +255 655 786 011 
Unaweza kusaidia wanakituo hawa kupitia akaunti ya KBC namba 3300828357

No comments: