Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akisani kitabu cha wageni wakati wa Halfa fupi ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni. Kushoto ni Diwani wa kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela.
Diwani wa kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela akizungumza na wakazi wa Kata yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akitoa taarifa wakati akizindua Mradi wa Maji Pugu Kajiungeni ambapo amesema mradi huo unatokana na kisima cha maji chenye urefu wa mita 122 toka usawa wa ardhi.
Mstahiki meya amesema kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita 60,000 kwa saa. Ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na mtandao wa mabomba wa kilometa 9, vituo 25 vya kuchota maji, nyumba ya pampu, fensi pamoja na uzio.
Aidha amewataka wananchi wa maeneo husika ya Pugu Kajiungeni ni kuitunza miradi hii na kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili kuweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Pugu Emelda Samjela na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kassim Mjesa na Kulia ni Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd inayoshughulikia mradi huo Method Mlay.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya wakazi wa Kata Pugu Kajiungeni watakaofaidika na mradi huo wakimsikiliza mstahiki Meya Jerry Silaa (hayupo pichani).
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akimkabidhi Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) barua rasmi ya mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni unaotekelezwa kwa ushirikiano na wahisani /wafadhili wa Serikali ya Ubelgiji, Umoja wa Ulaya (EU), Serikali ya Tanzania, Halmashauri ya manispaa ya Ilala na wafadhili wengine mbalimbali. Anyeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Kassim Mjesa.
Mkandarasi wa Kampuni ya Meero Contractors ltd Method Mlay (kulia) akitoa neno la shukrani baada Mstahiki Meya kumkabidhi barua rasmi ya ujenzi wa mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni na kuahidi kutoa ajira kwa Vijana wa maeneo ya Pugu kuanza sasa mpaka mradi utakapokamilika.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na wakazi wa Pugu baada ya kuzindua rasmi mradi wa maji wa Pugu Kajiungeni ulioanza kubuniwa rasmi mwaka 2011.
Sehemu ya wakazi wa Pugu Kajiungeni waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo utakaochukua miezi Sita kukamilika na kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa sita kushoto) akikagua sehemu ya mradi huo kilipojengwa kisima chenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita elf 60,000 kwa saa.
Muonekano wa Kisima hicho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa nne kushoto) na Diwani wa Kata ya Pugu Kajiungeni Emelda Samjela katika picha ya pamoja na viongozi wa kata hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akingumza na vyombo vya habari ambapo amesema mradi huo wa maji wa Pugu Kajiungeni uhahudumiwa na tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 140,000 lilipo katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto na matenki mnegine ya maji yenye ujazo wa lita 45,000 na 100,000 ambayo yanapatikana Pugu Kajiungeni karibu na Zahanati ya Pugu.
Amefafanua kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imechangia kiasi cha Shilingi 378,000,000 na kiasi kingine kinachobaki kinatolewa na Serikali Kuu pamoja na wahisani.
Mradi wote utagharimu kiasi cha shilingi 1,024,000,000/=.
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa kata ya Pugu Kajiungeni Nuru Daniel akitoa shukrani zake za pekee kwa Serikali ya awamu na uongozi kwa kutekeleza ilani za Chama ikiwemo kuwapatia maji wakazi wa Pugu Kajiungeni.
No comments:
Post a Comment