Sunday, April 27, 2014

HAFLA YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA VIWANJA VYA IKULU

1Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakikata keki katika sherehe ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Aprili 26 mwaka 1964 hafla hiyo iilifanyika jana kwenye viwanja vya Ikulu na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Seif Ali Idd, Waziri Mkuu Tanzania Mh. Mizengo Pinda na viongozi mbalimbali wa serikali taasisi za dini na vyma vya siasa, Kushoto ni Mke wa Rais mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkewa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 3Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein wakiwalisha keki wake zao katika hafla hiyo. 4Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kifaa maalum cha kufyatua mafataki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. 6Mafataki yakilipuka katika viwanja vya ikulu ikiwa ni moja ya burudani katika sherehe hizo. 7Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Msanii MwanaFA aka Binamu. 8Wazee wa Politiko Lifo Chipaka na Fahmi Dovutwa kulia wakifurahia Muungano. 9Wasanii mbalimbali walikuwepo katika hafla hiyo. 9aWadau kutoka Lugumi Enterprises walihudhuria katika hafla hiyo. 10Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jembe Jesca Msambatavangu kushoto na Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu wakiwa katika hafla hiyo. 11Mama Arafa Ridhiwani akiwa na ndugu zake katika hafla hiyo. 12Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mama Arafa Ridhiwani Kikwete kulia pamoja na ndugu zake. 14Wadau wa Fullshangwe wakakaa mble ya Kamera. 15gRais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein kulia, Dr. Gharib Bilal Makamu wa Rais wa pili kutoka kulia ni Balozi Seif Ali Idd Makamu wa pili wa Rais Zanzibar wakiongoza watanzannia katika hafla hiyo. 16Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti Kijana Calvin Nyoni Mshindi wa Musiki wa kizazi kipya kwa ajili ya sherehe za Muungano wa Tanzania 18Kikundi cha muziki kikiburudisha katika hafla hiyo kwenye viwanja vya Ikulu. 19Babu Tale Meneja wa Diamond kushoto nia Mkubwa Fella kiongozi wa kundi la TMK Family walikuwepo pia. 20Kulia ni Mzee Nyantori kutoka Idara ya Habari Maelezo Mdau Cliford Tandali katikati na Nyakia kutoka CCM Makao makuu. 22Waziri wa Habari, Maendeleo ya Vijana Utamaduni na Michezo Dr. Fennela Mukangara akizungumza na Mhariri Mtendaji wa TSN Bw, Gabriel Nderumaki na mdau Mabhare Matinyi katikati. 23Wadau wa Fullshangwe kutoka Zanzibar. 24Wake wa viongozi katika picha ya pamoja. 25Wadau wa Fullshangwe Mamaa Farida kushoto na Matrina wakipozi mbele ya Keki. 26Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati kundi la muziki wa Taarabu kutoka Zanzibar lilipokuwa likitumbuiza jukwaani. 27Wadau Esther Zelamula na mume wake kulia ni Frola Wingia wa Nipashe walikuwepo pia. 28Mdau David Robert na mke wake Alice pia walikuwepo katika hafla hiyo. 29Kikundi cha ngoma kikitumuiza jukwaani 30Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Bw. Joseph Msukuma wa kwanza kulia na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Simiyu Bw. Njalu Silanga wa pili kutoka kulia pamoja na wadau wengine wamehudhuria pia katika hafla hiyo.

No comments: