Sunday, June 14, 2015

Dkt Mwele: Kutoka binti mwenye ndoto kuwa mtafiti hadi mwanasayansi wa kimataifa


Mapema wiki hii, mwanasanyansi wa kimataifa Mtanzania, mwanamama Dokta Mwelecele (Mwele) Malecela, alitangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania kwa kuomba ridhaa ya kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi CCM. Dokta Mwele ambaye hadi wakati anatangaza uamuzi huo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), ana historia ya kipekee ambayo nilibahatika kuifahamu kupitia chapisho moja lililopo katika blogu hii. Hata hivyo, chapisho hilo ambalo lilisomwa na maelfu ya watu, lilikuwa katika lugha ya Kiingereza. Makala hii ni marudio ya chapisho hilo kwa lugha ya Kiswahili. Maelezo hayo yanatoka mdomoni mwa Dkt Mwele mwenyewe ila mie nimetafsiri tu kwa Kiswahili.
Ajira yangu katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ni hadithi ya bahati yenye matokeo mazuri ambayo awali haikuwa katika nia yangu. Nilijiunga na taasisi hiyo mwaka 1987 baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika stadi ya wanyama na tabia zao (BSc in Zoology) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1986. Baada ya usahili mzito, nilipangiwa kufanya kazi Kituo cha Amani (Amani Centre), hususan kushughulikia ugonjwa unaofahamika kama Bancroftian Filariasis. Nilishawahi kusikia kuhusu ugonjwa huo nilipokuwa mwanafunzi UDSM chini ya uangalizi mzuri wa Mhadhiri Dokta Parkin lakini sikujua nini nitafanya kuhusiana na ugonjwa huo. Kichwani mwangu, nilitamani kufanya kazi kuhusu ugonjwa wa malaria ambao kwa wakati huo nilidhani ulikuwa eneo la kuvutia kiutafiti. Kwahiyo, lazima Nikiri kwamba nilifadhaika kujikuta nashughulikia ugonjwa wa Bancroftian Filariasis badala ya malaria, ambayo ilikuwa na nyenzo nyingi kwa maana ya vifaa na ufadhili. Hata hivyo, niliambiwa bayana kuwa lazima nishughulikie kufufua shughuli ya ugonjwa huo wa Bancroftian Filariasis hapo Amani.


Nikiwa mtu ninayependa kukabiliana na changamoto, nikaanza safari ndefu ya kupita Milima ya Usambara, kuelekea sehemu hiyo  inayoitwa Amani.Safari ilikuwa katika mlolongo wa kupanda na kushika vilima kama mawimbi vile hadi wakati flani sikuona watu wala makazi. Hofu yangu ilipunguzwa na mandhari mazuri, misitu ya kupendeza, na hewa ilivyokuwa mwanana kadri tulivyopanda milima. Nilipofika Amani, hofu yangu ilinirudia tena, nikijiuliza iwapo ningemudu kweli kumudu maisha katika sehemu hiyo ambayo ilikuwa kama mafichoni kwa wakati huo. Nilijifariji mwenyewe kwa kujikumbusha kwamba sehemu hiyo tayari ilikuwa na wanasayansi kadhaa, na wamemudu kuishi hapo, Kwahiyo nami ningeweza pia. Baba yangu alikuwa na msemo maarufu, ‘Ni juu yako kumudu mazingira yanayokukabili,’ na hivyo ndivyo nilivyoamua kufanya.


Baada ya wiki kadhaa za mafunzo ya kuelewa mazingira, hatimaye nilipangiwa kufanyakazi katika maabara ya minyoo (helminthology laboratory) ambapo nilijifunza kuhusu parasaiti aitwaye Wuchereria Bancrofti, ambaye ndiye anayeeneza ugonjwa wa Bancroftian Filariasis. Nikajifunza kutambua hatua za awali za mzunguko wa maisha ya parasaiti huyo na mwingine aitwaye Onchocerca Volvulus. Nikajifunza kupasua mbu kwa ajili ya ucuhunguzi wa lava wa maambukizi na utambuzi wa mabara wa parasaiti mbalimbali, kama vile wa kichocho (schistosomes), minyoo ya tumboni (hookworks), trikurisi (Trichuris), nk. Wakati huo, dunia yangu ilikuwa dunia ya minyoo, na watu walioniinghiza katika dunia hiyo walikuwa miongoni mwa wajuzi wa mabara na wasaidizi wa mabara, ambao walinipatia mafunzo bora kabisa. Nathamini mafunzo hayo kwa sababu yamesaidia sana kunifanya kuwa mtu niliye sasa. Mmoja wa wasaidizi wa mabara alipendelea kunikumbusha kwamba alianza kazi mwaka niliozaliwa. Haikujalisha walivyonichukulia kama mtoto, nilichukua kila walichoniambia, na nilifurahia kila dakika. Kuna Nyakati familia yangu ilikuwa na wasiwasi kuhusu maendeleo yangu.Niliwapigia simu zile za zamani za mkonga kuwajulisha kuwa nilikuwa naendelea vema na kwa hakika ninapenda mahala hapo.



Kazi zangu za awali zilijumuisha kuchunguza uhusiano kati ya parasaiti wa eosinophilia na helminth. Pia nilichunguza matokeo ya majaribio ya maangamizi ya malaria katika maambukizi ya Bancroftian Filariasis. Pia nilifanya kazi na marehemu Profesa Chris Curtis kudhibiti mbu aina ya Culex katika mji wa Muheza kwa kutumia dawa za kuua wadudu za polystyrene beads.

Baadaye nilikwenda London, Uingereza kufanya Shahada ya Uzamili na ya Uzamifu katika Taasisi ya Magonjwa ya Kitropiki ya Chuo Kikuu cha London, ambapo nilifanyia kazi maambukizi ya filarial kwa paka. Paka hao walikuwa kwa ajili ya majaribio ya uchunguzi ambao ulikuwa muhimu kwa uelewa wa maambukizi ya filarial. Kazi niliyofanya ilikuwa kupata uelewa jinsi parasaiti wanavymudu kukwepa mfumo wa kinga ya mwili wa kiumbe aliyeambukizwa, na matokeo ya uchunguzi wangu yaligundua  kuwa kuna molekyuli za kiprotini (immunoglobulins) ambazo zilikuwa zikiwakinga parasaiti husika. Hii ilisaidia kuongoza uelewa kuhusu watu wenye maambukizi ya filarial lakini hawaonyeshi dalili za wazi.

Baada ya kurudi nyumbani, nilijihusisha na kuandaa utafiti wa kuelewa kitu ambacho kwa lugha ya kitaalam kinachoitwa immunoepidemiology ya maambukizi ya ugonjwa wa mabusha.Utafiti huo uliofanyika Kingwende, Kenya na Masaika, Tanzania. Machapisho kadhaa ya kitaaluma yalitokana na utafiti huo uliotuwezesha kufahamu zaidi kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa mabusha, ambao ungetuwezesha kutafuta mbinu bora za udhibiti.


Wakati huohuo, nilihusika na kuandaa mpango wa kimkakati kwa ajili ya mradi wa kutokomeza mabusha  nchini Tanzania. Hii ilifuatiwa na azimio la Shirika la Afya Duniani Mei 1997 ambalo lilisisitiza kuangamizwa kwa ugonjwa huo.Uaandaji wa mpango huo madhubuti ulifuatiwa na kuteuliwa kwangu kubwa mkurugenzi wa mradi unaohusu maradhi hayo mwaka 2000. Mwaka huohuo, mradi wa kupambana na ugonjwa wa mabusha ulianzishwa katika kisiwa cha Mafia, na mchango wangu kutoka maabara hadi kwenye eneo ambapo utafiti unatafsiriwa kwa vitendo ulitimia kamili. Kuna msemo wa Kiswahili kwamba safari moja huanzisha nyingine. Kwa upande wangu, hakujawa na mwisho wa safari hii bali ni vituo tofauti tu ninaposimama kidogo lakini naendelea mwelekeo huohuo.

Mradi huo wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha ulizidi kuimarika na sasa unafanya kazi katika wilaya 53 na umewafikia watu MILIONI 13. Huku msukumo sasa ukiwa kwenye magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika, njia zilizotumika katika mpango wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha zimepanuliwa na kujumuisha ugonjwa wa kichocho, minyoo wanaosambaa kupitia udongo na trakoma. Kwa kiasi kikubwa, usaili wangu katika makao makuu ya NIMR uliniandaa kwa ajira ya utafiti na udhibiti wa ugonjwa wa mabusha lakini kama ilivyo katika maeneo mengine ya maisha, sikujua hilo kwa wakati huo. Nilipata fahari kubwa pale Rais Jakaya Kikwete alipotangaza kuwa ataanzisha mfuko maalum kwa ajili ya ugonjwa huo kuwasaidia watu wanaosumbuliwa nao. Rais alitoa tangazo hilo katika Mkutano wa kimataifa wa masuala ya afya jijini Arusha, na hii imesaidia kupanua uelewa wa madhila yanayowakabili wahanga wa ugonjwa huo nchini Tanzania na kwingineko barani Afrika. Matokeo kutoka kituo cha uangalizi Tandahimba yanaonyesha  mradi wa kukabiliana na ugonjwa wa mabusha umefanikiwa kupunguza maambukizi katika wilaya hiyo, na hiyo itakuwa sehemu ya kwanza ya mafanikio ya kuingilia kati maambukizi kwa upande wa Tanzania Bara.
[IMG_7940.jpg]
 Je hii habari inayoelezea mafanikio? Ni habari kuhusu binti mdogo aliyekuwa na ndoto za kuwa mtafiti; kuhusu msichana aliyepanda vilima vya Amani kusaka ndoto yake, na ya mwanamke ambaye sasa anaishi katika ndoto hiyo kwa kufanya tafiti na kuchangia katika kukabiliana na ugonjwa ambao amekuwa akijishughulisha nao kwa takriban maisha yake yote. Labda hayo ndio mafanikio. Au waonaje?

Nina deni kubwa kwa watu wengi walioniwezesha kufanikisha safari hii, hususan baba yangu Dokta John Malecela na marehemu Mrs Ezerina Malecela ambao walinihakikikisha kuwa "ndiyo, waweza kutimiza ndoto yako."

Hapa chini ni machapisho mbalimbali ya kitaaluma 


Malecela M.N. Baldwin C.I and Denham D.A (1994) Hosts antigen on the surface of microfilariae of Wuchereria bancrofti and Brugia pahangi.
Transactions
Awarded prize for best presentation

Baldwin C.I., Medieros F, Malecela M.N. and Denham D.A (1994) Humoral responses in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Parasite 1,1S

Malecela (1995): Microfilariae and the immune response in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Ph.D. thesis, University of London.

P.E.Simonsen, D.W Meyrowitsch, W.G.Jaoko,M.N.Malecela, D.Mukoko, E.M.Pedersen, J.H. Ouma, R.T.Rwegoshora, N.Masese, P.Magnussen, B.B.A Estambale and E.Michael (2001) Bancroftian Filariasis infection,Diseaese and Specific Antibody Response Patterns in a high and a low endemicity community in East Africa. Parasite Immunology 23: 373-388

Michael E., Simonsen P.E., Malecela M., Mukoko D., Pedersen E.M., Rwegoshora R.T., Meyrowitsch D.W, Jaoko W.G., (2001)Transmission intensity and immunoepidemiology of bancroftian filariasis in East Africa. Parasite Immunology No 23. Pp 373-388

Paul Simonsen,Peter Bernhard, Walter Jaoko, Dan Meyerowitsch, Mwele N.Malecela-Lazaro, Pascal Magnussen and Edwin Michael (2002) Filaria Dance sign and subclinical hydrocele in two East African communities with Bancroftian filariasis. Transactions of the Royal Society of Tropical Medicine and Hygiene

Simonsen,P.E, Meyerowitsch, D.W, Jaoko W.G., Malecela, M.N., Mukoko, D., Pedersen, E.M., Ouma,J.H., Rwegoshora, R.T., Masese.N Magnussen, P., Estambale, B.B.A & Michael E. (2002) Bancroftian filariasis infection disease and specific antibody responses patterns in a high and low endemicity community in East Africa. American Journal of Tropical Medicine and Hygiene Vol 66(5) pp550-559

Simonsen P.E Meyrowitsch D.W., Mukoko D, Pedersen E.M., Malecela-Lazaro M.N., Rwegoshora R.T., Ouma J.H., Masese, N. , Jaoko W.G., Michael E., (2004) The effect of repeated half-yearly mass treatment on Wuchereria bancrofti infection and transmission in two East African communities with different levels of endemicity. American Journal of Tropical Medicine and Hygiene No 70 pp. 63-71




No comments: