Thursday, July 16, 2015

TIMU YA WATU 39 KUTOKA AFRIKA KUSINI WAPNDA MLIMA KILIMANJARO

Timu ya watu 39 wakiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia kununua taulo maalumu kwa wasichana waliopo shuleni zisaidie wakati wanapokuwa kwenye siku zao za Hedhi.
Katika timu hiyo wamo wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za nchini Afrika Kusini ,watu maarufu ,watangazaji katika vituo vya Luninga,wachezaji filamu n.k. katikati hapo ni Ofisa Uhusiano wa nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini Afrika kusini,Maya Makanjee.
Muigizaji maarufu wa filamu,Jack Devnarain akijulikana kama Rajesh Kumar katika tamthiliya ya Isidindo the Need akiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi mkuu Hfadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akizungumza wakati akitoa historia fupi ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki katika changamoto hiyo.
Mwanzilishi wa taasisi ya Imbumba Foundation ,Richard Mabaso akizungumza lengo la safari hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanao kama Trek4 Mandela ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuchangisha fedha zausaidia wasichana walioko mashuleni.
Baadhi ya washiriki katika changamoto hiyo.
Katibu tawala wilaya ya Moshi ,Remida Ibrahim akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wageni hao kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki wa Changamoto hiyo.
Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi ya taifa Mlima Kilimanjaro,Ibrahim Musa akitangaza ofa kwa mcheza filamu maarufu wa nchini Afrika Kusini Jack Devnarain (Rajesh ) kuja nchini kucheza sehemu ya filamu zake katika moja ya hifadhi za Tanzania.
Mcheza filamu maarufu nchini Afrika Kusini,Jack Devnrain(kulia) akituma picha mbalimbali za tukio hili kwenye mitandao ya kijamii.
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Washiriki wa changamoto hiyo.
Jack Devnarain maarufu kama Rajesh Kumar wa kwenye tamthiliya ya Isidingo the Need akifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Ofisa Uhusiano wa nje wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini Afrika Kusini ,Maya Makanjee akifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Ofisa Uhusinao wa nje wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom ,Maya Makanjee akizungumza jambo katika hafla hiyo kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki.
Washiriki wa Changamoto hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania,Allan Kijazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania ,Allan Kijazi akiwa na Mkurugenzi wa Utalii wa shirika hilo,Ibrahimu Musa wakiongozwa na Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya kuelkea eneo maalumu kwa ajili ya kuanzisha safari ya kupanda mlima Kilimanjaro. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi bendera za taifa la Tanzania na Afrika Kusini kwa kiongozi wa timu hiyo Richard Mabaso ikiwa ni ishara ya kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wageni hao wakipia "Serfie"kabla ya kuanza kupanda Mlima.
Safari ya kupanda Mlima ndio imeanza.
Rajesh wa Isidingo the Need akiwa miongoni mwao.
Ofisa Uhusiano wa nje waKampuni ya Mawasiliano ya Vodacom,Maya Makanjee ni miongoni pia mwa wapandaji hao hapa akiianza safari"Pole pole"

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: