Kippi Warioba akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano huo. |
Kippi Warioba akibadilishana mawazo na Mmoja wa makada wa CCM waliohudhuria mkutano huo. Kulia ni Mkewe Nkaleni Warioba. |
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Zarina Madabida akiongozana na Kippi baada ya mkutano kumalizika. |
Mtoto
akiwa bango lenye picha ya Kippi Warioba.
PICHA ZOTE/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Na
Mwandishi Wetu
MGOMBEA
ubunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba,
amesema anafahamu changamoto zinazowakabili wamachinga, mamalishe, baba lishe
na wajaririamali wadogo; na kuomba wamchague ili azishughulikie.
Aidha,
baba mzazi wa mgombea huyo, Jaji Joseph Warioba, amewataka wakazi wa Kawe
wamchague kijana wake kwa kuwa ni msikivu, anayejituma na siyo mtu wa
kusukumwa.
Akizungumza
kwenye mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Songas ulipo Kata ya Makongo Juu
juzi, Kippi alisema amewahi kufanyakazi na sekta binafsi ambayo ilimkutanisha
na wajasiriamali, vikundi vya ujenzi, Saccos na Vicoba, hivyo alifanikiwa kujua
changamoto zinazowakabili.
“Changamoto
za makundi haya nazifahamu, nafahamu mnahitaji mafunzo na rasilimali mbalimbali
kuendesha biashara zenu nithibitisheni Oktoba 25 nikazifanyie kazi,” alisema.
Kuhusu
Makongo Juu, Kippi alisema Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020, imeainisha kwamba
barabara ya Makongo kuanzia Chuo cha Ardhi hadi Goba itajengwa kwa kiwango cha
lami na tatizo la maji litakwisha kwa kuwa serikali itakamilisha mradi wa kutoa
maji Kimbiji hadi Dar es Salaam.
“Matatizo
ya michango mingi shuleni ambayo wazazi wanailalamikia, uhaba wa madawati,
matundu ya vyoo, vitabu na madawati ni mambo ambayo tutashirikiana kwa pamoja
kuyatatua wala hayahitaji mipango mikubwa ya serikali,” alisema.
Alisema
wakazi wa Kawe wanapaswa kumchagua Dk. John Magufuli, yeye (Kippi) pamoja na
madiwani wa CCM ili wakamsaidie kazi ya kutekeleza ilani.
Naye
Jaji Warioba alisema wakazi wa Kawe hawapaswi kufanya makosa ya kuchagua
wagombea wa upinzani kwa kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi wa Magufuli,
itafanyakazi nzuri.
Alisema
Dk. Magufuli ni mtendaji mzuri asiyependa rushwa hivyo ni wajibu wa wananchi
kumchagulia wasaidizi kutoka CCM ili wakafanyekazi ya kuwatumikia.
Alisema
hulka za Dk. Magufuli zinafanana na za mtoto wake (Kippi), kwa kuwa naye ni
mchapakazi, msikivu na mtu mwenye ushirikiano mkubwa.
Naye
mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo Juu, William Iteba, alisema kero za wakazi
wa kata hiyo zinajulikana ikiwamo ukosefu wa kituo cha polisi, soko na ajira;
hivyo akichaguliwa atatatua kero hizo.
No comments:
Post a Comment