Saturday, October 3, 2015

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE MKOANI SINGIDA

 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma (hawapo pichani),alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru kiongozi huyo wa dini kwa kujitolea kumuombea Dua ya heri na afya njema katika nafasi yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida jioni ya leo ,wakati akiwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani. 



Dkt. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali  hasa za mashirika ya  dini ambazo zinaendesha hospitali  katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili   kuimarisha huduma  za kiafya  kwa jamii.


Sehemu ya umati wa Wakazi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi kwenye mkutano wake wa mwisho kwa jioni ya leo,ambapo kesho anatarajia kuendelea na kampeni mkoani Singida na baadae kuhitimisha kampeni zake kwenye mkutano mkubwa ambao unatarajiwa kurushwa live na kituo cha Star TV.

 Kiongozi wa Msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli,Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt.Magufuli kuwahutubia wananchi wa Ikungi jioni ya leo na kuwaomba kumpigia kura ya ndio ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchahuzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.
Wananchi  wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na pia kuwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia debe Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye  mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi,mkoani Singida.
 Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili mjini Itigi mkoani Singida mapema leo mchana,tayari kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni mjini humo.
 

 Baadhi ya Wazee wakifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya wananchi wa mji wa Itigi mkoani Singida mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Manyoni wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara wa Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba kura ili awe Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ambapo ameaomba ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kumpigia Kura za Urais,Ubunge na Udiwani..
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Ndugu Damiel Mtuka mara baada ya kukabidhiwa Kitabu cha Ilani ya chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana mjini Manyoni mkoani Singida
 Baadhi ya Wakazi wa mji wa Manyoni wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Itigi Ndugu Yahaya Omar Masele mbele ya Wakazi wa mji huo (hawapo pichani),waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Itigi Ndugu Yahaya Omar Masele mbele ya Wakazi wa mji huo (hawapo pichani),waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana.
 Baadhi ya wananchi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi
PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.

No comments: