Thursday, December 10, 2015

BARAZA LA HALAMSHAURI YA WILAYA YA MOSHI LAMCHAGUA MICHAEL KILAWILA KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI

Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,wakiwa ukumbini hapo kabla ya kuapishwa.
Wagombea waliopitishwa na Chadema kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu Mwenyekiti wakiwa katika ukumbi wa
halmashauri hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kabla ya kuapishwa.
Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,wakiapishwa kuwa madiwani rasmi.
Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri hiyo,Moris Makoyi akiwa katika kikao cha kwanza cha baraza hilo.
Katibu tawala wilaya ya Moshi,Remida Ibrahim akiongoza zoezi la upigaji kura kwa ajili yakumpata Mwenyekiti na Makamu wake wa Halmashauri hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akiteta jambo na Diwani wa kata ya Kahe ,Rodrick Mmanyi wakati wa kikao cha baraza hilo.
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Joseph Chata akiomba kura mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Moshi.
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti kupitia chama cha Demokasia na Maendeleo (Chadema)  Michael Kilawila akijinadi mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Moshi akiomba kuchaguliwa kuogoza baraza hilo.
Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Sephen Charles akiomba kura mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Moshi.
Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kupitia chama cha Demokasia na Maendeleo (Chadema)  Exaud Mamuya akijinadi mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Moshi akiomba kuchaguliwa kuogoza baraza hilo.
Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kupitia chama cha NCCR -Mageuzi Gibrata Riwa akijinadi mbele ya wajumbe wa baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Moshi akiomba kuchaguliwa kuogoza baraza hilo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akipiga kura wakazi wa zoezi hilo.
Wajumbe wakishiriki zoezi la upigaji kura.
Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava akimpongeza Diwani wa kata ya Kindi,Michael Kilawila baada ya kutangazwa mshindi kwa kupigiwa kura 36 .
Madiwani wakifurahia mara baada ya kuvaa joho rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa baraza hilo.
Mwenyekiti mpya wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akiongozana na Makamu wake ,Exaud Mamuya wakati wakiingia katika ukumbi wa baraza hilo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akitoa muongozo wakati wa uzinduzi rasmi wa baraza hilo.
Mwenyekiti wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akitoa hotuba yake ya kwanza wakati wa uzinduzi rasmi wa baraza hilo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi.
Mwenyekiti wa Halamshauri ,Michael Kilawila na Makamu wake ,Exaud Mamuya wakifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya (hayupo pichani).
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Severine Kahitwa akitoa maelekezo mbalimbali ya uendeshaji wa baraza hilo kwa Madiwani na uongozi mpya wa baraza hilo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akifuatilia .
Menyekiti wa Chadema wilaya ya Moshi vijijini Ekarist Kiwia pia alikuwa ni miongoni mwa mashuhuda wa mchakato wa kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Michael Kilawila.
Makamu Mwenyekiti wa baraza la Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Exaud Mamuya.
Ndugu wa madiwani wakifurahia nje ya ukumbi wa Hlamshauri ya wilaya ya Moshi mara baada ya Madiwani kuapishwa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kakskazini (0755659929).

No comments: