Mraghbishi Zaituni Rashida toka wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga
Katika
vijiji vya mikoa ya Geita, Simiyu, Shinyanga na Arusha, wananchi wamekuwa
mstari wa mbele kuhakikisha wanajisimamia wao wenyewe na viongozi wao ili kufanikisha
shughuli za maendeleo. Hata hivyo, si wote wanaofanya hivyo. Wale walio mstari wa mbele tunawaita waraghbishi na kile wanachofanya ni uraghbishi.Hawa ni wale wanaochukua hatua kustawisha au kulinda haki za binadamu na maslahi ya jamii kwa ujumla wake; kiuchumi, kisiasa au kijamii. Watu hawa wapo kwenye makundi tofauti tofauti wakiwamo wenyeviti wa vijiji, madiwani, wakulima, wafugaji, viongozi wa kidini, sungusungu, na walimu. Watu hawa wamechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuwashawishi na kuwawezesha wanavijiji wenzao kuwa waraghbishi. Uraghbishi wao kwa wenzao unafanyika kwa njia mbalimbali; iwe kwa kukutana kwenye vijiwe vya kahawa, mashambani, kwenye visima vya kuchotea maji, shuleni ama popote pale wanapopata nafasi zikiwamo sehemu za ibada.
shughuli za maendeleo. Hata hivyo, si wote wanaofanya hivyo. Wale walio mstari wa mbele tunawaita waraghbishi na kile wanachofanya ni uraghbishi.Hawa ni wale wanaochukua hatua kustawisha au kulinda haki za binadamu na maslahi ya jamii kwa ujumla wake; kiuchumi, kisiasa au kijamii. Watu hawa wapo kwenye makundi tofauti tofauti wakiwamo wenyeviti wa vijiji, madiwani, wakulima, wafugaji, viongozi wa kidini, sungusungu, na walimu. Watu hawa wamechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuwashawishi na kuwawezesha wanavijiji wenzao kuwa waraghbishi. Uraghbishi wao kwa wenzao unafanyika kwa njia mbalimbali; iwe kwa kukutana kwenye vijiwe vya kahawa, mashambani, kwenye visima vya kuchotea maji, shuleni ama popote pale wanapopata nafasi zikiwamo sehemu za ibada.
Harakati
hizi zimewawezesha kujisimamia kwa kutambua wajibu na haki zao wanazostahili
kuzidai kutoka, aidha kwa viongozi wao waliowachagua ama wale waliopewa dhamana
ya kusimamia rasilimali kwa niaba yao. Mifano ipo mingi kuanzia kudai taarifa
na mapato na matumizi, kudai huduma bora za kijamii kama upatikanaji wa dawa
kwenye zahanati, huduma za maji na elimu n.k.Pamoja na
mafanikio hayo, bado ni jukumu la uraghbishi si rahisi. Ni gumu na
linalokatisha tamaa. Waraghbishi hawalipwi malipo yoyote zaidi ya kutumia zaidi
walichonacho, kubwa zaidi likiwa ni muda wao. Ni shughuli ambayo wakati
mwingine yaweza kukutia matatizoni.
Hakuna mtu anayependa kufuatiliwa
mambo yake, hasa yanapokuwa na matatizo; yawe ya kujisababishia au ya bahati
mbaya. Uraghbishi ni pamoja na kumulika mambo ambayo yanawahusu watu wengi. Akieleza changamoto ya kufanya
uraghbishi, Melina Ndumuzi, toka wilayani Mbogwe mkoani Geita anasema: “Yataka moyo wa ujasiri sana kufanya
uraghbishi vinginevyo unaweza ukaogopa kuthubutu. kwa sababu ya mtazamo wa
jamii kuhusu watu waraghibishaji.” Kwa upande wake Epifania Mwenda toka
kijiji cha Tanga, kata ya Katente wilayani Bukombe anasema: “Maisha ya uraghbishi ni ya kujitolea zaidi,
si rahisi ni kazi sana, njia pekee ni kupenda kufanya unachofanya. Matokeo ya
kile unachofanya ndio utaona mwisho wa siku wengine wanavutika kuraghbisha. Ila
ni kazi nzito na kama una moyo mdogo huwezi kuifanya.”
Zaituni Rashid anayefanya uraghbishi
katika kijiji cha Mhunze, kata ya Kishapu, mkoa wa Shinyanga anataja changamoto
ya kukimbiwa na wale anao waraghbisha, “Huku kwa ujumla tunajitolea, inafika
mahali wenzako wanakukimbia kila mmoja ana sababu zake, yaani shidaa!” Ugumu unakuja hasa pale unapokuwa ni
mwajiriwa wa serikali na wakati huo huo unafanya uraghbishi. Kwa mfano mraghbishi
ambaye ni mwalimu na kwa upande mmoja anawaunga mkono wale wanaopingana na
mwenendo wa mkurugezi wa wilaya, ambaye ndiye mwajiri wake. “Ebu fikiria unamuona mwenzako
anatafutwa na mwajiri wako, na wewe upo upande wa mraghbishi. Ni changamoto
sana,” anaeleza mraghbishi William Msangi toka kijiji cha Buluhu kilichopo kata
ya Ipoja wilayani Mbogwe.
Akiunga
mkono changamoto hiyo ya kimaslahi Zaituni Rashida anasema, “Sisi huku ni shida, mapato yanaliwa
na wakuu wako. Unaanzaje kuwasonga? Na ukiwahoji viongozi wa chini wanakueleza
kwenda kwa mkurugenzi wako,” Said Simoni toka kijiji cha Mheza, yeye
kwa upande wake anaanza kwa kuuliza waraghbishi wenzake toka vijiji vya wilaya
yao Bukombe kuhusu uragbishi wao katika vijiji vyao. Swali hili anawauliza
baada ya kukutana na wenzake“Vipi vikao vya wazazi mashuleni
vimefanyika nyie huko kwenu.?”Swali hili anauliza akilinganisha na
changamoto zinazokabili uraghbishi katika eneo hilo na kamati za shule za
vijijni. Kamati hizi zinaundwa na watu 9; Diwani (1), walimu (3) na wazazi (5).
Mwenyekiti wa kijiji anakuwa kama mgeni mwalikwa.
Mraghbishi William Msangi
toka kijiji cha Iponya, wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita
Akiongelea changamoto anazokumbana
nazo hasa linapokuja suala la kusimamia kamati za shule, Simon anasema:“Yaani hadi mtu anafikia mahala
anasema unataka uchukue cheo chake, kisa nimeuliza maswali yanahusu mapato na
matumizi ya shule. Ni ngumu sana kwa sababu wabadhirifu hawapendi sana
kufuatwafuatwa. Hivyo, muda mwingine unajikuta upo kwenye mtafaruku usioutarajia.”Hofu hii ya wananchi kuuliza maswali
kwa viongozi waliowachagua ni chagamoto. Simon anaongeza kwa kusema: “Elimu inahitajika mno ili watu waweze
kujiamini kwani kuna watu wanawasujudia madiwani kama miungu watu wakati wao
ndio waliomweka madarakani. Hali hii ya kuwaogopa viongozi ni tatizo kubwa.”
Na hapo ndipo wanapokiri kuna umuhimu
wa kuwa na mbinu mbadala ya kufanya uraghbishi, vinginevyo waraghbishi na wale
raia waamilifu ambao ni waajiriwa na muda huo huo ni wananchi hujikuta katika
mazingira hatarishi. Na hawa viongozi wa chini wanahitaji kupatiwa mbinu za
uraghbishi. Kwa nini? Kwa sababu kuna baadhi yao wana hofu na woga kwa wakubwa
zao.
Hatua mbalimbali wanazochukua
zinatokana na uamilifu wao; yaani uwezo wa kujitambua na kusimamia kile ambacho
wanaamini sahihi. Kwa kufanya hivyo wanakuwa si tu waraghbishi bali pia raia
waamilifu. Pamoja na changamoto hizo, na nyingine
nyingi kama za kutishiwa kufungwa au kudhuriwa, bado raia hawa waaminifu
wameendelea na uamilifu wao. Akifafanua nini hasa kinachowasukuma kufanya uraghbishi,
Gabriel Jonathan toka kijiji cha Lugunga anasema: “Watu hawa ni wa muhimu na mafanikio
ya uraghbishi ni kuungwa mkono na watu wengi. Hapa changamoto lazima iwe
inahusisha watu wengi, hiyo ndio tunaiita changamoto.” Ili mtu aweze kuchukua hatua ni lazima
awe na sababu inayomgusa. Mraghbishi
unapoibua jambo ni lazima uwe umelifanyia tathmini ya kutosha na kujiridhisha
kwamba unachowaambia watu ni sahihi.
Watu ni changamoto ambayo inaendana na
muda. Waraghbishi wengi ni watu ambao wana shughuli zao. Na shughuli hizi ndizo
zile zinazowaingizia kipato wanachotumia na familia zao. Akifafanua changamoto
hii baba wa watoto wanne na mke, Gabriel Jonathan anasema:
“Ili waweze kuchukua hatua ama kufanya
kitu fulani, wanahitaji uwepo wako. Wasipokuona kwenye vikao hivyo huwa
inawakatisha tamaa, hivyo inakulazimu kufunga biashara na kuja kujumuika na
watu. Hii ni changamoto kubwa.”Unahitajika ubunifu mpya wa
kuwawezesha waraghbishi kukabiliana na changamoto hizi. Njia mojawapo ni kutengeneza urafiki
na wale ambao tunahitaji kuwabadilisha. Njia hii ni muhimu katika kushawishi
wale ambao kwa njia moja ama nyingine wanaoneka kwenda kinyume na maadili ya
uongozi. Kwa kufanya hivi inasaidia kupunguza uhasama na kuonana kama maadui. Akisisitiza umuhimu wa dhana ya nguvu,
Richard Mabala anasema waraghbishi wakumbuke daima kwamba nguvu yao hutokana na
nguvu ya watu na si mapambano binafsi. Na hii ndio siri ya mafanikio ya
waraghbishi ama raia waamilifu. Kwa kawaida wajumbe wengi wa
halmashauri ya serikali ya kijiji hutegemea posho za vikao kama njia mojawapo
wa kujikimu. Hawa hawana mshahara na ni watu kutoka kwenye jamii ile ile ya
wale waliowachagua. Ni mara chache sana wanaunga mkono hoja ya kutolipwa kwenye
vikao.
Kutokana na uraghbishi, wajumbe wa
kijiji cha Buluhe kilichopo kata ya Iponya walikubaliana kutopokea fedha za
posho na badala yake zitumike katika shughuli nyingine. Akielezea jinsi
alivyowabadilisha wajumbe wa halmashauri ya kijiji kuwa raia waamilifu, katika
maana ya kujitambua, William Msangi toka anasema: “Baada ya kuwaraghbisha wajumbe wa
halmashauri ya serikali ya kijiji kuhusu dhamana yao kwa wananchi kwa kuacha
kujitazama wao wenyewe zaidi, walikubali kutopokea posho. Kwa siku hiyo
tuliweza kuokoa kiasi cha shilingi laki tatu na elfu sabini na tano,” Baada ya fedha hizo kukusanywa
zilikabidhiwa kwa mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha ikiwa kama ni sehemu
ya uraghbishi kwani hapo mwanzo fedha alikuwa anakaa nazo mtendaji wa kijiji, jambo
ambalo halikuwa sahihi. Kwa hiyo ili uamilifu na uraghbishi
uwe wa kweli inabidi liwe ni suala la watu na si la mtu mmoja mmoja ili nguvu
za pamoja zifanye kazi. Na hapo ndipo ujenzi wa taifa unapoonekana moja kwa
moja kwa sababu ni chetu si sote. Pamoja na changamoto zote bado raia hawa
waamilifu wamendelea na harakati za ujenzi wa taifa pasipo kukata tamaa na badala
yake wanaendelea kuhamasishana wao kwa wao.
No comments:
Post a Comment