Thursday, October 6, 2016

MUWSA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI ZA KUTOA ELIMU BURE

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa tofali 2300 kwa ajili ya ujenzi
wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakati wa kukabidhi madawati kwa ajili ya shule ya msingi Msamadi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiongozana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA),Joyce Msiru wakitizama ujenzi wa madarasa matatu unaoendelea katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msamadi ,Seseama Bayo mara baada ya kupokea matofali 2300 yaliyotolewa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Mafundi wakishusha tofali zilizotolewa na MUWSA kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa .wengine ni watumishi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa madarasa hayo.
Jengo jipya lenye madarasa mawili katika shule ya msingi Msamadi ambalo kwa kiasi kukamilika kwake kutasaidia kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa shuleni hapo.
Moja ya madarasa yaliyopo shuleni hapo kama linavyoonekana ambapo wanafunzi wamekuwa wakikaa chumba kimoja kwa idadi kubwa kuliko uwezo wa darasa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini. 

No comments: