Tuesday, August 22, 2017

Tigo yachimba kisima chenye thamani ya 18m/- kijiji cha Usongelani Tabora


Mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora, Mhe.  Aggrey  Mwanry akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa kisima cha maji kilichokabidhiwa na kampuni ya Tigo chenye thamani  ya Tsh 18m/-kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya  Urambo mkoani  Tabora jana 

Mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora, Mhe.  Aggrey  Mwanry akipampu maji kuzindua kisima cha maji alichokabidhiwa na kampuni ya Tigo chenye thamani  ya 18m/-kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya  Urambo mkoani  Tabora jana . Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya ziwa (mwenye miwani), Alli Maswanya, Diwani wa viti maalum kata ya Usoke, Aneth Msangama na Diwani wa Usoke, Said Kazimilo.


Mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora, Mhe.  Aggrey  Mwanry akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya Usoke wilayani Urambo, Nusura Swalehe mara baada ya uzinduzi wa kisima cha maji chenye thamani ya tsh 18m/-alichokabidhiwa na kampuni ya Tigo  kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya  Urambo mkoani  Tabora jan


Mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora, Mhe.  Aggrey  Mwanry akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata ya Usoke wilayani Urambo,  Rehema Maganga mara baada ya uzinduzi wa kisima cha maji chenye thamani ya tsh 18m/-alichokabidhiwa na kampuni ya Tigo  kwa kijiji cha Usongelani wilaya ya  Urambo mkoani  Tabora ja

-Mkuu  wa  mkoa  wa  Tabora Aggrey  Mwanry  akicheza mziki  na baadhi  ya  wakazi  wa kijiji cha Usongelani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kisima cha maji kilichotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi nchini Tigo



Ni sehemu ya msaada wa Tigo katika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama
Tabora, Agosti 22, 2017- Tigo Tanzania imejenga kisima cha maji  chenye thamani  ya Sh 18m/-katika kijiji cha Usongelani katika wilaya ya Urambo, mkoani  Tabora kama sehemu ya ahadi iliyotolewa na  kampuni hiyo ya kuunga mkono ya kuunga mkono ustawi wa kijamii katika maeneo inamohudimia pamoja na juhudi za kuunga mkono katika kuhakikisha kuwa wananchi wote nchini wanapata maji safi na salama.
Akizungumza kwenye sherehe ya makabidhiano  iliyofanyika katika Kijiji cha Usongelani mkoani Tabora, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya alielezea matumaini yake kuwa kisima hicho kitachangia kwa kiwango kikubwa  kupunguza  tatizo la uhaba wa maji katika eneo hilo  kwa kuipatia jumuia ya eneo hilo  kupata maji ya uhakika, safi na salama.
"Tumejitahidi kuboresha maisha ya jamii , sio tu kwa kuhakikisha kuwa wanafurahia huduma nzuri za mawasiliano kutoka katika mtandao wetu, bali pia kupiga hatua zaidi kuhakikisha kuwa afya zao na ustawi wao unaboreka," alisema.
Maswanya alibainisha kwamba msaada huo  unafanya vijiji vilivyonufaika  kufikia  21,  na hivyo kuwafanya watu zaidi ya 187,000 kunufaika na kujituma huko kwa Tigo katika  kuwapatia watu  maji safi na salama kote nchini.
Mwaka huu, Tigo inakusudia kuchimba visima katika maeneo yaliyo na uhitaji mkubwa  ambapo inatarajiwa kuwa zaidi ya watu  350,000 watafaidika na mchango wetu wa kuisaidia juhudi za za kupunguza uhaba wa maji safi na salama  uliopo nchini.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa  Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Aggrey Mwanri ambaye wakati akiwashukuru Tigo kwa msaada unaohitajika sana alisema kuwa kisima hicho  kitasaidia kwa kiwango kikubwa kuimarisha afya na ustawi wa jamii kwa kusaidia  kukua kiuchumi na kijamii. Aliwataka watu wengine wenye mapenzi mema  kujitokeza kuunga mkono jitihada za kuondokana na tatizo la uhaba wa maji katika mkoa huo.
Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa kutusaidia katika jitihada zetu za kuwapatia  maji ya uhakika katika eneo hili kwa kutatua uhaba wa maji uliokuwepo. Tunaamini kuwa upatikanaji wa maji safi na salama karibu na makazi kutaongeza pia uzalishaji wa kiuchumi hasa kwa wasichana na wanawake ambao hawatakuwa  wakitumia tena muda mwingi  kutafuta maji safi mahali pengine. Hii itawapa wasichana fursa ya kuhudhuria kwa uhuru shuleni na kuwapunguzia mzigo wa kijamii hasa wanawake, hivyo kupata nafasi ya kushughulikia kwa ufanisi majukumu yao ya kila siku  kwa maendeleo ya taifa, " alisema Mkuu wa Mkoa.

No comments: