Wednesday, July 25, 2007

HONGO YA NGONO!


Na Richard Manyota
Kigogo mmoja wa Benki jijini Dar es Salaam, (jina limehifadhiwa) ameonesha kufuru ya pesa kwa kumhonga Miss Tanzania kiasi cha shilingi milioni 3 (3,000,000/=), sambamba na kumuahidi mrembo huyo kumjenge nyumba na kumnunulia gari la kifahari.

Meseji na baadhi ya vielelezo vilivyotua mezani kwa Amani hivi karibuni vimefichua matumizi hayo makubwa ya fedha yanayodaiwa kufanywa na kigogo huyo kwa ajili ya kupalilia penzi la mlimbwende mwenye heshima ya Miss TZ.

Kwa mujibu wa sms hiyo, kiasi hicho cha pesa alichodaiwa kupewa Miss huyo (jina lake limehifadhiwa) ni mwanzo wa huduma atakazopewa endapo atakubali kukandamiza raha na mheshimiwa huyo.

“Nenda (inatajwa sehemu) kachukue shilingi milioni 3 kwa ajili ya matumizi yako, na huo ni mwanzo tu wa huduma yangu kwako, nafanya hivi ili kukuonesha kuwa nakupenda, lakini mambo mazuri zaidi yanakuja.

“Naomba ukubali ombi langu ili tupange kuhusu mambo ya maendeleo zaidi maana naona umuhimu wa kukununulia gari na kukujengea nyumba,” ilisema sehemu ya meseji kutoka kwa kigogo huyo.

Aidha meseji zilizoletwa dawatini kwa Amani na rafiki wa karibu wa Miss huyo mwembamba mrefu hazikufafanua kama mrembo huyo alikwenda kutia mfukoni kitita hicho cha pesa ama laa.

“Sijui kama alichukua pesa zote au hakuchukua, alichoniambia mimi ni kuwa alivyokwenda huko alikuta pesa nusu, jambo lingine jamaa (kigogo) anamsumbua sana kiasi kwamba anahatarisha uchumba wa rafiki yangu,” alisema rafiki wa mrembo huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.
Aliongeza kuwa, rafiki yake amekuwa akisita kulikubali ombi la kigogo huyo kwa hofu ya uvumi uliopo mtaani kwamba kibosile huyo ana virusi vya ugonjwa wa UKIMWI.

Alisema, yeye kama rafiki wa miss huyo aliamua kuzihamisha meseji hizo kutoka katika simu ya swaiba wake na ‘kuzimuvuzisha’ Amani akilenga kuharibu mpango wa kigogo huyo muathirika.
Amani lilimtafuta mlimbwende huyo anayewindwa na mkubwa huyo wa benki na kukiri kuwepo kwa ishu hiyo

“Ni kweli amekuwa akinitongoza na kunishawishi lakini nimeshamkatalia kwani nina mpenzi wangu,” alimalizia na kuongeza kuwa hana taarifa ya hongo ya milioni 3.

Naye kigogo wa benki alipotafutwa na mwandishi wetu ili azungumzie kuhusu tuhuma hizo alisema, “Unaweza kuthibitisha kuwa mimi nimemhonga? Mambo yangu achana nayo ikiwa namfahamu huyo miss au simfahamu hayo hayakuhusu,” alijibu na kukata simu.


SANGOMA APATA KICHAPO

Na Dotto Mwaibale
Mganga mmoja wa kienyeji ‘Sangoma’ aliyefahamika kwa jina la Kamende Shabani mkazi wa Tabata Kimanga Jijini Dar es Salaam mtaa wa darajani hivi karibuni amejikuta akipata kipigo kikali kutoka kwa wananchi kufuatia tabia yake ya kuwadhalilisha watu wanaofika kwake kwa ajili ya matibabu.

Chanzo chetu cha habari kinachoishi maeneo hayo kimedai kuwa, sangoma huyo amekuwa na tabia ya kuwatibu watu wanaofika kwake hasa wanawake kwa njia ambazo si nzuri kiasi cha kuwakera wananchi.

“Tangu mganga huyu ahamie maeneo haya tumekuwa tukisikia watu wakipiga makele ndani kwake, awali tukajua ni sehemu ya matibabu lakini tukaja kubaini kuwa anawafanyia wateja wake vitendo ambavyo sinyo,” kilidai chanzo hicho.

Akizungumzia tukio hilo mmiliki wa nyumba anayoishi Bw. Kamende, aliyefahamika kwa jina moja la Bw. Manjwili alikiri kukithiri wa tabia chafu za sangoma huyo na kudai kuwa alifikia hatua ya kumtimua lakini alikuwa akikaidi amri.

“Kwa kweli nimekuwa nikiishangaa tiba anayoitoa mganga huyu, amekuwa akiwatibu watu katika chumba chenye giza na wakati mwingine akiwa amelewa, kitendo kilichonifanya nimtimue nyumbani kwangu,”alisema Bw. Manjwili.

Alizidi kueleza kuwa, hivi karibu alimshuhudia mganga huyo akimfanyia udhalilishaji wa kutisha mwanamke mmoja aliyefika nyumbani hapo kwa ajili ya matibabu. “Juzi nililetewa taarifa kuwa kuna mwanamke analia ndani ya chumba cha mganga huyo, nilipoingia ndani nikamuona mwanamke huyo ambaye ni mgeni machoni mwangu akiwa katika wakati mgumu huku Sangoma huyo akiwa amemkaba koromeo kwa mkono wa kushoto na wa kulia alikuwa akimpiga kisogoni,” alitanabahisha Bw. Manjwili.

Aliongeza kuwa, kitendo hicho na vingine vya namna hiyo ndivyo vilivyowafanya wananchi kushikwa na hasira na siku hiyo kuamua kumtolea uvivu kwa kumpa kipigo kikali hadi kuzimia
Mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo Bw.Ali Singa alipoulizwa na mwandishi wetu juu ya tukio hilo alidai kutokuwa na taarifa za kuwepo kwa Sangoma huyo katika eneo lake na kuahidi kulifanyia kazi.

“Sina taarifa za kuwepo kwa mganga huyo wa kienjeji katika eneo langu ila kwasababu umeniambia basi nitafanya uchunguzi,” alisema mjumbe huyo.

2 comments:

Anonymous said...

Bwana Abdallah, pole na kazi. Kwa kweli nasikitika kwamba umetupunja story moja, naomba nikurudishe nyuma, ulituonyesha picha ya gazeti moja lililo andika kuhusu "mzimu wa amina wamtokea maimatha", ukaishia hapo, story hujatupa, matokea yake sisi tulio nje ya nchi tumeanza kuamini kwamba kumbe amina ana mzimu unaowatokea watu. Naomba tuweke sawa au tueleze anachodai maimatha tafadhali kuhusu hii story.

Anonymous said...

MIMI NAMSHAURI HUYO MISS TANZANIA KAMA AKIAMUA KULALA NA HUYO BABA AMBAE KWA JINA MNAMSTAI, KWAMBA KABLA YA KULALA NA HUYO BABA ACHIMBE KABISA KABURI LAKE.!!!