Thursday, July 12, 2007

Jamani Gavana wa Benki Kuu mbaguzi?!




Pichani juu ni baadhi ya waandishi waliobaguliwa kuingia ndani ya benki kuu (picha ya juu), akiwemo mwandishi wa Redio Ujerumani anayewahoji waandishi wenzie...jamani ubaguzi huu...!


Tanzania- July 13, 2007
Na Jimmy Mfuru

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Balali jana alibagua baadhi ya wandishi wa habari na kuongea na wachache aliowahitaji yeye, jambo lililozua maswali mengi yasiyokuwa na majibu.

Gavana huyo alifanya kitendo hicho katika mkutano wa wandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Balali ilikuwa aongee na wandishi wa habari juzi lakini aliahirisha ghafla bila maelezo yoyote na kisha kufanya kikao hicho jana huku akiwa na majina ya waandishi wa habari aliopanga kuongea nao.

Wandishi wa habari walikusanyika katika idara ya mapokezi ya ukumbi huo saa 5 asubuhi, ambapo kwa mshangao mkubwa ofisa mmoja wa benki hiyo alifika na kuanza kuita majina ya wandishi ambao walipangwa kuingia katika mkutano huo.

Hatua hiyo iliwafanya baadhi ya wandishi wa habari waliokataliwa kuingia mkutanoni akiwemo mwandishi wetu, kulalamika wakidai kuwa hawakutendewa haki yao ya msingi ya kukusanya habari.

"Lazima kuna kitu kinafichwa, kwa nini Gavana achague vyombo vya habari vya kuongea navyo? tena kwa majina! Hata Ikulu Rais akiitisha mkutano huwa habagui chombo, " alisema Christopher Buke, Mtangazaji wa Sauti ya Redio ya Ujerumani (Deutch Welle) ambaye naye hakuruhusiwa kuingia.

Hatua ya Gavana Balali kuongea na wandishi wa habari imekuja kufuatia madai ya kuwepo kwa ubadhirifu wa mabilioni ya fedha ndani ya benki hiyo, jambo lililofanya baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kulalamikia hali hiyo.

4 comments:

Anonymous said...

Mkome ! na nyie waandishi wa udaku mngeenda kuuliza nini huko kwa gavana kama sio udaku tu, tehe tehe tehe tehe theeth !
mkomeeeeeeeeeeeeeeeeeee,
afadhali huyo wa radio ya ujerumani

Anonymous said...

Oh Noooo!!!! Hiyo si sawa kabisa. Hapo Bwana Mkubwa huyu amechemsha! Katika nchi yetu hasa kipindi hiki cha uwazi na ukweli ndani ya kasi Mpya, Nguvu Mpya watu wa kaliba hii hawafai hata kidogo! Nafikiri Mheshimiwa mwenye dhamana na Nchi hii ameliona hilo, Poleni sana vijana, msife moyo!!! Iko siku tutafika tu! Hata mimi inaniuma sana.

Anonymous said...

kwa nchi kama Uingereza na Marekani magazeti haya mnayoyaita ya udaku yanaheshimika sana na hufanya kazi kubwa tu, wanaowajibu wa kuripoti kitu kwa upande mwingine, usiseme wangeripoti nini, kama wasingekuwepo ungeyajua haya wewe said!

Anonymous said...

wwewe fala hapo juu acha ushamba mwandishi ni mwandishi tu awe wa udaku,wa futari au huko ujerumani unapoona ni bora wote wana hai sawa tu,babako balali kachemsha sana,wenye nchi tunakuja huko tumeshachukua mafunzo ya kutosha ya kivita