Makubwa!!
Hatimaye Mzee Chifupa ameweka wazi mazingira yaliyosababisha kifo cha mwanae. kikubwa alichokisema jana katika mkutano na waandishi wa habari ni kwamba mwane alikuwa amepigwa juju kwa sababu ugonjwa aliokuwa akiuumwa Amina ni wa Kiswahili na ndo maana hawakumpeleka hospitali mapema... (Tunazo taarifa aliwahi kuombewa hata na wachungaji wa dini nchini) kama ambavyo sikuzote ilivyokuwa inasemwa chini ya kapeti .......! ilifikia mahali alikuwa anaweweseka masikini binti wa watu.... na kutaja majina ya vigogo ambao tunadhani ni wa madawa ya kulevya na ndo waliomuondoa...
..... "Hii ni siri kubwa, hata mkiniuliza sitaweza kuwaambieni kwanini marehemu Amina alikuwa akiwataja kwa majina viongozi wa ngazi za juu, itabaki kuwa siri yangu," alisema Mzee Chifupa katika taarifa yake kwa media jana asubuhi pale MAELEZO. Ijumaa wiki hii lina Full story!!!
6 comments:
nadhani muache kumfuatilia dada wa watu, halafu sio mzee chifupa wa mpakanjia ni mzee chifupa unampaje ubini mwingine? wabongo bwana... kwanza gazeti lenu ndio lilimsakama sana, bora sikuona manake siko huko, mwacheni apumzike jamani dada wa watu, kuna maneno mlipewa na mwanablogu mmoja sijui yaliwafikia??? acheni dhambi nyie ijumaa kama vipi toa au usitoe utakuwa umepata ujumbe
weka comment yangu wewe cool guy no problem, kama huna problem weka hiyo comment, umekosea jina la mzee chifupa rekebisha kwanza halafu nyie magazeti ya udaku pia mnatakiwa mtoe tamko especially haya ya kwenu mnaotoa hadith uchwara tena uchwara.......weka comment yangu jitu la bisu la huku na kule....ile comment yangu kuuzu magazeti yenu uchwara iko wapi?
vipi mmekosea jina hapo mkuu!
pia gazeti lenu ni udaku mwingi, wawezekana nao ulikuwa sababu, toeni boriti kwanza wazee
hakuna juju hapo amina alikuwa mgonjwa kwanini atuwi wakweli tunapo fiwa maladhi nikawaida kwa mwanadamu tunajua wote amina alikuwa mwenzie liyumba sasa huwo uchawi umetoka wapi?
mh mzee chifupa wa mpakanyia??? bila shaka umepitiwa mkubwa!!
ukisikia udaku ndo huu, karibuni sana nyie wageni wa maneno ya kiudaku, hakuna kilichokosewa hapo, Chifupa wa Mpakanjia ni sawa tu, jamaa kaweka msisitizo.. Said, welcome to the world of Udakus!
Post a Comment