Friday, August 24, 2007

POLISI AFUMANIWA!

Na Waandishi Maalum
Askari Polisi mwenye namba F.8906 PC Tumaini wa Kituo cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii alifumwa 'akikandamiza raha' chumbani kwake na Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu mwenye umri wa miaka 18 (jina lake na shule anayosoma vimehifadhiwa kwa sababu za kimaadili).

Fumanizi hilo lililohusisha askari kadhaa wa Kituo cha Polisi cha Oysterbay, lilitokea Agosti 21, mwaka huu katika chumba cha askari huyo kilichopo Manyanya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Kukamatwa kwa PC Tumaini, kunafuatia malalamiko dhidi yake kutoka kwa majirani zake kuwa licha ya binti huyo kuwa na uhusiano nae wa kimapenzi, alikuwa akimpiga mara kwa mara na kumzuia kwenda shule kwa kumfungia ndani mchana kutwa.

Chanzo chetu cha habari ambacho ni jirani na askari huyo kilidai kuwa yeye na wenzake waliokuwa wakimuonea huruma binti huyo kwa kipigo alichokuwa akipata na kufungiwa ndani bila kwenda shule, Jumanne wiki hii walitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow juu ya uchafu na ukatili aliokuwa akiufanya askari huyo.

Aidha mtoa habari huyo alisema kuwa alitoa taarifa kwa waandishi wetu ili nao waweze kufuatia tukio hilo, hatua ambayo ilichukuliwa baada ya mwanafunzi huyo kuonekana akiingia katika chumba cha PC Tumaini.

Hata hivyo, baada ya kupata taarifa hiyo, Kamanda Rwambow alituma polisi kadhaa kwenda kwa askari huyo ambapo walikutana na waandishi wetu waliokuwa tayari wamefika katika eneo hilo na kufanikisha zoezi la kuwafuma wawili hao wakiponda raha kama wanavyoonekana pichani ukurasa wa mbele wa gazeti hili.

Timu hiyo ya askari kanzu walioutumwa na Kamanda Rwambow, walipigwa na butwaa baada ya kugundua waliyekwenda kumkamata alikuwa ni askari mwenzao wa Kituo cha Polisi walichokuwa wakitoka wao (Oysterbay)!

Aidha, waliweza kumtambua mwanafunzi aliyekuwa naye kuwa ni mtoto wa askari mwenzao wa kituo hicho.

Baaada ya PC Tumaini na mwanafunzi huyo kutiwa mbaroni, walipelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano zaidi.

Waandishi wetu waliwahoji baadhi ya majirani wa askari huyo ambapo walidai kuwa PC Tumaini alikuwa akitembea na mwanafunzi huyo kwa muda mrefu na mara kwa mara ‘denti’ huyo alikuwa akifika nyumbani kwake asubuhi akiwa amevaa sare za shule kisha huzivua kabla ya kuzivaa tena jioni wakati wa kurudi kwa wazazi wake.

Aidha, jirani huyo aliongeza kuwa, kufuatia tabia chafu ya askari huyo, yeye na majirani zake walikereka na kuamua kutoa taarifa kwa bosi wake (Kamanda Rwambow) ili kunusuru maisha ya baadae ya binti huyo na kuwafumbua macho wazazi wake ambao waliamini binti yao alikuwa akienda shule.

"Mimi na wenzangu tuliumia sana kila tulipokuwa tukimuona binti huyo akipika na kufua nguo za polisi huyo badala ya kwenda shuleni na mbaya zaidi tulikuwa tukijisikia vibaya jinsi alivyokuwa akipigwa bila huruma,'' alisema mmoja wa majirani hao.

Akizungumza na Waandishi Wetu juu ya tukio hilo, Kamanda Rwambow alisema PC Tumaini atashitakiwa kijeshi na kuchukuliwa hatua zaidi ambazo hakuzifanunua.


(MWANDISHI 'ATUNDIKWA MIMBA,' IJUMAA SEXIEST GIRL ALIYETOLEWA BONYEZA HAPA http://www.globalpublisherstz.com/ijumaa/ (WARNING: STILL UNDER CONSTRUCTION)!

No comments: