Na Mwandishi Wetu
Hali ya kiafya ya Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Mpakanjia maarufu Meddy ambaye alipelekwa Hospitali ya Kuu ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii kutibiwa bado tata na sasa anatibiwa na daktari maalum wa hospitali hiyo, Risasi limedokezwa.
Koffi Olomide afanya laana!, Hali ya Mpakanjia bado tata!
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Mpakanjia ambaye alipelekwa hospitalini hapo usiku wa kuamkia Jumatano mwaka huu na Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba amelazwa katika chumba cha watu maalum (VIP) chini ya uangalizi wa Daktari Mkuu wa Hospitali hiyo, Brigedia SS Salim.
"Mpakanjia amelazwa katika chumba cha watu maalum, chini ya uangalizi wa daktari mkuu wa Hospitali Brigedia SS Salim na hakuna mtu yeyote mwingine anayemhudumia zaidi yake," alisema mtoa habari wetu.
Chanzo chetu hakikuweza kusema mfanyabiashara huyo anasumbulia na nini zaidi ya kupooza sehemu ya mwili wake lakini alisema kuwa anapatiwa vipimo vya uhakika na matibabu ya nguvu.
"Hali ya ugonjwa wa Mpakanjia bado tata, ingawa juhudi zinafanyika ili kuweka mambo sawa na baadhi ya vipimo tayari vimechukuliwa ili kujua tatizo hasa linalimsumbua," kilisema mchanzo hicho.
Habari zaidi zinasema kuwa kuna ulinzi wa kutosha katika sehemu alikolazwa mfanbiashara huyo, hivyo si rahisi kwa mtu kuingia kumjulia hali bila ruhusa maalum kutoka kwa walinzi na baadhi ya ndugu wanaomuuguza.
Mwandishi wetu alimpigia simu Brigedia Salim na kumuuliza hali ya mgonjwa anayemtibu lakini hakuwa tayari kusema lolote kuhusu afya ya mfanyabiashara huyo.
"Siwezi kusema chochote, wapigie ndugu zake wanaomuomuuguza, watakupa hali ya mgonjwa wao," alisema daktari huyo.
Mpakanjia alianza kuumwa muda mfupi baada ya mkewe Amina Chifupa kufariki dunia, ambapo baadhi ya watu wanadai kuwa kuumwa kwake kunatokana na mshituko uliosababishwa na msiba mkubwa alioupata.
(Tayari watu wameshaanza kumchulia, mchana mzima wa leo jiji la Dar limeenea uvumi kuwa Mpakanjia ameshafariki dunia! Ukweli ni kwamba hadi natuma taarifa hii sasa saa 10:01 saa za Afrika Mashariki yu ngali mzima, japo hali yake ni tete pale hospitalini Lugalo)
No comments:
Post a Comment