Na Mwandishi Wetu
Hali ngumu ya maisha inayosababishwa na tatizo la uhaba wa ajira, inaonekana kuwapeleka puta vijana wengi ambao wameshindwa kumudu makali yaliyopo hivyo kulazimika kuyakatisha maisha yao kwa kujiua.
Uchunguzi wa Amani umebaini kuwa vijana wanaokatisha maisha yao wengi wao walikuwa wafanyabiashara wadogo (wamachinga), wapiga debe, wanafunzi waliokosa muelekeo na wafanyakazi wa ndani waliofukuzwa na waajiri wao.
Uchunguzi huo uliochukua zaidi ya mwezi mmoja, umethibitishwa na matukio ya hivi karibuni kwa kijana mmoja kujirusha kutoka ghorofani na mwingine kujichoma kisu kama picha za ukurasa wa mbele zinavyoonesha.
Kijana wa kwanza (jina lake halikufahamika) aliyeamua kujirusha kwenye jengo moja lililopo barabara ya Msimbazi Kariakoo alisema kuwa, amefikia uamuzi huo baada ya maisha kuwa magumu kufuatia kuporwa biashara yake na watu aliowataja kuwa ni askari wa jiji la Dar es Salaam.
Alisema "ni bora kufariki kuliko kuishi, maana kila unachokifanya hakifanikiwi, nimenyang'anywa kila kitu na migambo, nifanye nini sasa nami nina watoto, si bora nife" alisikika akisema kijana huyo ambaye hata hivyo aliokolewa na wasamaria wema.
Naye kijana Said Ally, mkazi wa Kimara aliyeripotiwa kujichoma kisu tumboni alisema ameshindwa kuvumilia ugumu wa maisha, kutokana na kile alichosema kuwa ni kukosa ajira licha ya kuwa na elimu ya chuo.
Baadhi ya watu ambao ni mashuhuda wa matukio hayo mawili waliiomba serikali kuwa makini na wimbi la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, na kuonya kuwa kama hali hiyo haitadhibitiwa taifa liweza kujikuta katika hali mbaya.
“Ni vema serikali ikatazama ugumu wa maisha unaowakabili vijana wetu, wasipuuze. Wakiona ni jambo la mchezo mauaji ya kutisha yatatokea hapa nchi," alisema Said Abeid wa Kariakoo wakati akiongea na Amani.
Matukio ya watu kujiua kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni ugumu wa maisha yamekuwa yakiongezeka siku za hivi karibuni, huku ongezeko la wahalifu likipewa sababu hiyo hiyo ya ukata.

No comments:
Post a Comment