Na Makongoro Oging’
Warembo wanaodaiwa kufanya biashara ya uchangudoa katika maneno kadhaa ya jiji la Dar es Salaam, huku baadhi yao wakiwa wanafanya mambo machafu na wanaume ‘kubonyezwa kizenji,’ hivi karibuni wamedakwa na askari.
Tukio hilo lilitokea kati ya saa 4 saa na 6.30 usiku wiki iliyopita, katika msako maalum uliofanywa na askari wa Manispaa ya Ilala karibu na Baa za Kimboka, Sewa na maeneo mengine ya Buguruni, jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo la aibu tupu lililovuta umati mkubwa wa watu na kuhudhuriwa na mwandishi wetu, wengi wa machangudoa hao walikuwa katika ‘pea’ wawiliwawili katika maeneo yaliyokuwa na giza nene.
Mwanahabari wetu alifanikiwa kuwaona askari wa Manispaa ya Ilala wakiwasomba wasichana hao pamoja na wanaume zao na kuwaingiza katika gari la wazi lililotengwa kwa ajili ya zoezi hilo, kisha kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Buguruni.

Hata hivyo, katika zoezi hilo kulitokea heka heka kubwa huku baadhi yao wakitimua mbio katika jitihada za kukwepa kukamatwa.
Mwandishi wetu alishuhudia kondomu zilizotumika zikiwa zimetapaa karibu na makazi ya watu ambapo baadhi ya wazazi wa eneo hilo walitoka nje wakati wa operesheni hiyo na kudai kuwa kuna kila dalili ya watoto wao kuharibika kitabia, kutokana na mambo machafu yanayofanywa na wasichana wanaojiuza.
Kitu cha ajabu kilichotokea ni kuwa wakati waandishi wanawapiga picha, baadhi yao walifurahi na kusema kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wametangaziwa soko. Hata hivyo, habari za uhakika zinasema kuwa zoezi hilo litaendelea na waliokamatwa wote walifikishwa katika Mahakama ya Jiji na wengine wako gerezani baada ya kukosa wadhamini.

No comments:
Post a Comment