Monday, August 20, 2007

MTOTO MATHEW NJIANI KUPONA!

Bw. Abbas Bungara akikabidhi msaada wake pamoja na wa ndugu yake wa Marekani kwa mwandishi Mariam Mdeme kwenye ofisi za Global Publishers jijini Dar. (soma habari kamili)

Mtoto aliyekuwa na hali mbaya, Mathew Pascal (pichani), yu njiani kupona baada ya kufanikiwa kupokea baadhi ya michango na kulipia hospitali ambapo mapema tarehe 30 mwezi huu atalazwa tayari kwa kufanyiwa operesheni.

Mathew atafanyiwa operesheni za aina mbili ikiwemo ya kufungua njia ya haja kubwa na kufanyiwa operation kubwa ya kumrudisha utumbo mkubwa ndani na kufanya tatizo lake hilo kufikia ukingoni.

Akiongea Kwa furaha mama yake Neema amesema kuwa tayari alishakata tamaa juu ya mtoto wake na anawashukuru wale wote ambao wamemchangia na walioahidi kufanya hivyo kwani mwanae kama Mungu akimsaidia atakuwa kama watoto wengine.
Tayari mpaka sasa kiasi cha shilingi laki saba zimepatikana ambapo kiasi cha shilingi laki tano zimekabidhiwa kwa Daktari Sai wa Hospitali ya Taifa (Muhimbili) na zingine zimekabidhiwa kwa mama yake mtoto ili zimsaidie kujikimu kimaisha kwani yupo katika wakati mgumu.

Waliotoa michango yao baada ya kuona habari na picha hiyo kwenye Blog hii wiki mbili zilizopita, ni Mtanzania aishie Japan aliyetoa kupitia ngugu yake aliyeko Dar (200, 000) na Mtanzaia mwingine aishie Marekani ambaye nae alitoa shilingi 200,000 kupitia ndugu yake aishie Dar aitwae Abbas Bungara ambaye nae aliongeza kiasi cha shilingi 100,000 alizokuja nazo kwenye ofisi za Global.

Watanzania wengine wawili waishio jijini Dar es salaam, ambao hawakupenda kutaja majina yao, wametoa laki moja kila mmoja na kumkabidhi moja kwa moja mama mtoto mkononi.

Tunawashukuru wote kwa moyo mlioonyesha, tumuombee kwa Mungu mtoto Methew oparesheni zake zifanikiwe na kupona. Blog hii itakuwa ikiwaletea maendeleo ya mtoto huyo hadi hatua ya mwisho.


Methew akilia kwa uchungu akiwa na mama yake wiki mbili zilizopita

No comments: