Monday, September 24, 2007

Dudu asikitishwa na Kalapina

Kufutia bifu kali lililoibuka hivi karibuni, kati ya Kundi la Kikosi cha Mizinga na vijana wa Nako 2 Nako, ambao wanadaiwa kupigwa na wana Hip Hop hao, msanii Godfrey Tumaini 'Ze Dudu' ameiambia Abby Cool & MC George Over The Weekend kwamba anampa ushauri wa bure rafiki yake wa karibu, Karama Masoud 'Kalapina' kuwa ugomvi unamuharibia jina, Catherine Kassally ameshuka nayo.

Akiongea kwa njia ya simu, Dudu alisema kwamba anasikitika sana baada ya kusikia rafiki yake huyo, ambaye ndiye kiongozi wa Kikosi cha Mizinga kila kukicha hana jambo la kusifiwa zaidi ya lawama kutoka kwa watu aliowapiga kitu ambacho si kizuri kwa msanii mkubwa kama yeye.

'Mimi namuomba Kalapina awe mpole kwani katika sanaa kuna maudhi mengi, ambapo asipojiangalia atakuwa akiwapa kibano hata watu wake ambao wamemfanya afike hapo alipo. Suala ni kukubaliana na kila hali ili kulinda heshima yake'.

'Kalapina ni ndugu yangu kisanii, akumbuke mimi nilikuwa zaidi yake, nikajiona ninaubavu, niliwadunda maadui zangu na wasio maadui, sheria ikafuata mkondo wake niliishia jela kitu ambacho sikukitegemea. Atulie, amuombe Mungu amuondolee hasira vinginevyo atakosa mikataba minono kwa ajili ya ubondia' alisema Ze Dudu.

No comments: