Ishu nyingine iliyoifikia safu hii, kabla haijaelelea mtamboni ni kwamba, TMK Halisi wanaoongozwa na Juma Kassim 'Sir Nature' (pichani) lipo katika maandalizi makali kwa ajili ya kukamilisha albamu tatu kwa mpigo.
Mkurungezi wa kundi hilo, Hassani Isaac 'Chichi' alisema kuwa wasanii watatu wa kundi hilo ndiyo wanakuwa wahusika wakuu katika santuli hizo, kwani hivi sasa wameamua kutoana kwa awamu kama ilivyo kwa wenzao wa TMK Family.
'Wasanii hao ni BK ambaye albam yake ina nyimbo kumi, itakwenda kwa jina la 'Kwa Maisha', albamu ya pili ni ya 'Dollo' itakayoitwa 'Kuishi na Watu', ya tatu ni ya kwake Inspector Haroun ambayo bado haijapewa jina. Albamu hizo zitatambulisha kwa pamoja katika shoo ambayo tutaitaja hivi karibuni, kabla ya hapo tutaachia video ya wimbo wenye jina la 'Leo Tena', alisema Chichi.
Mwisho Chichi amewaomba Wabongo wampigie kula Nature ili video yake ya wimbo unaoitwa Mugambo ishinde kupitia tuzo zinazoandaliwa na televisheni ya 'Channel O' ya Afrika Kusini. 'Ili Nature ashinde tuzo hizo Watanzania wanatakiwa wampigie kura kwa kuandika Juma Kassi kisha watume kwenda 15331. Mwisho wa zoezi hilo ni Oktoba 4, mwaka huu, shughuli ya utoaji tuzo hizo itafanyika Novemba, mwaka huu ndani ya City Hall J, iliyopo Johannesburg' alisema.

No comments:
Post a Comment