Friday, October 12, 2007

MTANGAZAJI RADIO ONE HATUNAYE!

Marehemu Moses Justine..1965 - 2007 (RIP)
Wazazi wakiaga mwili wa Justine aliyezikwa Alhamis 11, katika makaburi ya Kinondoni. Daima atakumbukwa kwenye kipindi chake maarufu cha MTAA WA MANGOMA na AFRICAN PANORAMA!
Misanya Bingi msibani..aliwahi kufanya kazi na Marehemu ..siku hizi mzee Misanya mambo yake...!
Abubakary Sadik(kati), mtangazaji Radio One, akiwa msibani.
Benny Kinyaiya (shoto) Mtangazaji Channel Ten akiwa msibani
Idd Azzan mbunge wa Kinondoni (shoto) na Steven Chuwa Mtangazaji wa ITV wakiwa msibani
akina mama wakifarijiana msibani...


DEMU AZUA KASHESHE MSIBANI!

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Beatrice Mwendapole, mkazi wa jijini Dar es Salaam,
katikati ya wiki hii alivamia msiba wa Mtangazaji wa Kituo cha Radio One na Televisheni cha ITV, Moses Justine na kudai alikuwa mchumba wa marehemu huyo.

Kitendo hicho, kiliwashangaza wengi miongoni mwao ni mama mzazi wa Moses na dada zake ambao walisema hawamtambui.
Akizungumza na Ijumaa, Beatrice alidai alishangazwa na kitendo cha mama mkwe na wifi zake kumkana wakati yeye na marehemu waliishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili.

Beatrice alisema kinachomuuma ni kitendo cha ndugu wa Moses kumtimua na kumuambia akitaka kukaa pale msibani akae kama waombolezaji wengine lakini madai yake ya uchumba hawayatambui.
Huku akilia, mwanamke huyo alidai yeye ndiye aliyekuwa akimuuguza marehemu mpaka alipofariki Oktoba 10, mwaka huu katika Hospitali ya Dk. Kairuki, Mikocheni jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa wiki mbili.

Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alifanikiwa kuzungumza na mama mzazi wa Moses, Mary Justine ambaye alimkana mwanamke huyo.

Mama huyo alimtaja mwanamke mwingine aitwaye Isabela Massawe kuwa ndiye alikuwa mchumba wa marehemu mwanaye. "Kwa ujumla simtambui huyo dada Isabela anayejiita mchumba wa mwanangu," alisema mama Mary.

Mama huyo alisema mwanaye ameacha mtoto mmoja aitwaye Goodluck.

Naye dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Dora Justine, alisema; "sisi tunamshangaa huyu mwanamke anayejitangazia eti, yeye ndiye mchumba wa marehemu wakati wifi yetu aliyetuonyesha kaka ni Isabela, yeye wala hatumjui".

Marehemu alizaliwa mwaka 1965 kijiji cha Mkalama wilayani Iramba mkoani Singida na kusoma Shule ya Msingi Naura mwaka 1975 mpaka 1981 na hatimaye alipata elimu ya Sekondari katika Shule ya Enaboisho iliyopo Arusha na baadaye kupata kozi mbalimbali.

2 comments:

Anonymous said...

kaka mrisho website yenu ya globalpulisher mbona haifunguki nini tatizo nimevumilia wiki lote nasema kesho kesho itarudi ila bado.turudishieni hadithi zinatupita jamnii

Anonymous said...

poleni kwa msiba jamni mungu amlaze mahali pema peponi