Saturday, December 1, 2007

Aisha Madinda kukamua Desemba 7 Diamond


Mnenguaji mahiri wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ Aisha Madinda ameibuka na kuzima uvumi uliokuwa ukisambaa kwa kasi ya ajabu kuwa ameitema Twanga Pepeta.

Akizungumza na mwandishi wetu mapema wiki hii Kinondoni jijini Dar es Salaam, Aisha alisema kuwa ameshangazwa na uvumi huo kuwa aliamua kuachana na Twanaga Pepeta ikiwa imebaki siku chache tu bendi hiyo izindue albamu yake katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

“Watu wanazusha kuwa mimi nimeimwaga Twanga, lakini ninachotaka kusema ni kuwa mimi bado nipo Twanga ila nasumbuliwa na afya kidogo nawaomba wapenzi wangu wasiwe na hofu kwani naendelea vizuri, naamini Desemba 7 nitakuwepo Diamond Jubilee kwenye uzinduzi wa albamu yetu ya Mtaa wa Kwanza,” alisema Aisha.

Aisha Madinda ni miongoni mwa wanenguaji wachache wenye uwezo wa kuteka hisia za wapenzi wa muziki wa dansi nchini mara tu apandapo jukwaani na kuanza kupinda mugongo!

UDAKU ZAIDI: WWW.GLOBALPUBLISHERSTZ.COM

No comments: