Tuesday, August 7, 2007

MISS MATATANI BAADA YA FUMANIZI!


Na Imelda Mtema
Siku chache baada ya kumfumania Miss mwenzake, Mrembo wa Utalii mkoa wa Tanga 2005, Ania Saidi amekumbwa na balaa kubwa baada ya kubondwa na kuumizwa vibaya na kundi la watu wasiojulikana.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa Julai 31, mwaka huu Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Akiongea na mwandishi wetu, Ania ambaye ni Miss Ngorongoro Crater na aliyewahi kushika mataji ya Miss Ubungo namba 2 mwaka jana, alipatwa na kimbembe hicho alipokuwa ameenda eneo hilo kumpitia rafiki yake.

“Nilikuwa nimeenda kumpitia rafiki yangu ili tuweze kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa rafiki yetu anayeishi Mikocheni,” alisema Ania.

Alisema alikodi gari dogo (taxi) kutoka nyumbani kwake Sinza Palestina hadi Mwananyamala na alipofika maeneo anayoishi rafiki yake huyo dereva huyo aliegesha gari naye kuteremka.

“Dereva alinishusha eneo hilo kwa sababu gari lake halikuweza kufika katika eneo analoishi rafiki yangu huyo”, alisema mrembo huyo.

Mrembo huyo aliongeza kuwa baada ya kushuka na kupiga hatua tano alistukia amekabwa koo na kupigwa na kitu kizito kichwani kabla ya kuanguka chini.

Akiwa chini, miss huyo alisema kuwa, alifanikiwa kuwaona vijana watatu ambao walimpora pochi yake iliyokuwa na cheni pamoja na simu vyote vikiwa na thamani ya shilingi 750, 000.

Hata hivyo, alisema aligoma kutoa vitu hivyo lakini alizidiwa nguvu baada ya mmoja wao kuchomoa kisu na kumkata mkononi huku wakimchania nguo na kumfanya abaki nusu uchi.

Alisema kuwa, baada ya tukio hilo vijana hao walikimbia na kumwacha akiwa na maumivu makali mwilini.

“Nilinyanyuka na kujikongoja hadi kwa rafiki yangu na kupiga simu kuwapa taarifa ndugu zangu akiwemo mchumba wangu,” alisema mrembo huyo.

Alisema kuwa, mchumba wake alifika kwa rafiki yake ambapo alimchukuwa na kumpeleka katika Hospitali ya Mico, Sinza jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Ania alisema kuwa, anahisi vijana hao walitumwa na wabaya wake kumfanyia kitu mbaya, kwani wakati wakimpiga aliwasikia wakitoa maneno ambayo aliamini kuwa walikuwa wametumwa na mtu fulani.

Hivi karibuni Ania aliripotiwa kumfumania miss mwezake aliyefahamika kwa jina la Nadia Mohamed, Msasani Club jijini Dar es Salaam.



WEMA, KANUMBA KUKOMBA TSH. 180,000,000

Na Mwandishi Wetu
Miss Tanzania 2006/07 Wema Sepetu na Msanii wa Maigizo nchini, Steven Kanumba huenda wakakomba kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni 180 endapo watashinda kesi watakayoifungulia kampuni inayochapa gazeti hili Global Publishers & General Enterprises.

Uwezekano huo wa kuukwaa utajiri wa chapchap umekuja, kufuatia wawili hao wiki iliyopita kuiandikia barua kampuni hiyo na kudai pesa hizo wakidai kuwa wamechafuliwa majina lao.

Katika barua mbili tofauti kwa kampuni hiyo ambayo imetolewa na Rattansi & Company, Advocates na kusainiwa na wakili wake Nasir H.Rattansi, Wema na Kanumba wanadai kuwa habari mbili zilizochapishwa na gazeti hili kwa matoleo yake namba 400 la Julai 18 na namba 403 la Julai 28 mwaka huu zimewadhalilisha.

Barua ya kwanza iliyokuwa ikilalamikia gazeti hili, ilihusu habari iliyosema kuwa ‘Wema, Kanumba wabambwa laivu’. Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao walionekana usiku katika Ukumbi wa Mercy Club, walikokwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa msanii wa Kaole Rachel Kongojole.

Ilidaiwa kuwa Wema na Kanumba walishindwa kuingia ukumbini humo na kutulia kwavile walistuka baada ya kudokezwa kuwa kulikuwa na waandishi wa habari.

Hata hivyo, barua ya wakili wao ilidaiwa kuwa Si Wema wala Kanumba aliyekuwepo ukumbini humo siku hiyo, hivyo kudai fidia ya shilingi milioni 90.

Katika habari ya pili ambayo pia fidia ya shilingi milioni 90 inadaiwa, iliyomhusu Wema pekee na kupewa kichwa cha habari, ‘Hata aoshwe vipi, Wema hatakati’, ilidaiwa kuwa mrembo huyo ni miss wa kwanza nchini kukumbwa na kashfa nyingi za ngono.

Barua ya wakili wa Wema ilidai kuwa mteja wake si mhuni ‘kihivyo’ hivyo kulitaka gazeti hili kukanusha na kulipa fidia ya kiwango hicho cha pesa.



Two moons on 27th August 2007

*27th August; the day the Whole World is waiting for ......

Planet Mars will be the brightest in the night sky starting August.

It will look as large as the full moon to the naked eye. This will cultivate on Aug. 27 when Mars comes within 34.65 Million miles of earth.
Be sure to watch the sky on Aug. 27 12:30 am. It will look like the earth has 2 moons.
The next time Mars may come this close is in 2287.

Share this with your friends as NO ONE ALIVE TODAY will ever see it again.

BIG BROTHER AFRICA KUMEKUCHA!!!

BBA Guy...Mrithi wa Mwisho Mwampamba .. Richard Bezuidenhout...ndiye mwakilishi wa Tanzania katika shindano la BBA2 liloanza rasmi Jumapili iliyopita Afrika Kusini ...ubini wake ndo kasheshe..!
Deal or No deal.... Lola Opanga (kulia), Matanzania aliyewahi kushiriki lile game la Deal or no Deal na kujinyakuliwa USD 16, 500 (shilingi za kibonngo 20,000,000) akifurahi na Miss Africa wakati wa utambulisho wa BBA juzi Sea Clif Hotel.... mambo tambarale kwake..! (Sorry niliandika kwa makosa dola 60,000, thx for your comments)
Project Fame girl.... Nakaaya (kati) mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka jana akipozi na wadau wa Showbiz, Henry Mdimu wa gazeti la Mwananchi (kushoto), nami mdau wa blog hii, juzi katika uzinduzi wa BBA Sea Cliff Hotel. Binti ni ndugu dam na Miss Africa 2005, Nancy Sumary..imetulia!

MWONGOZO SAHIHI WA ULAJI


YUO ARE WHAT YOU EAT

Asalaam aleikum jaman! Bwana Yesu asifiwe sana! Tunakutana tena katika kona hii kuelimishana kuhusu staili ya maisha tunayopaswa kuitumia ili tuishi maisha yaliyo huru na maradhi, magonjwa na mateso mengine ya kiafya.

Wiki hii nataka kuwafundisha mwongozo bora wa ulaji sahihi kwa kufuata vipengele 10 katika ulaji wako wa kila siku, vitu unavyopaswa kuvila ambavyo vitaimarisha afya ya mwili wako na kukupa kinga madhubuti dhidi ya maradhi mengine.

Kuwa na afya njema inaweza kuwa kitu rahisi sana iwapo utazingatia vipengele 10 vya msingi vifuatavyo, ambavyo vitakupa angalau mwanga wa kitu gani kinafaa kufuatwa katika staili yako ya kula kila siku .

Jaribu kadri uwezavyo kufuata vipengele hivi na kuvifanya kuwa sehemu ya maisha yako. Hata hivyo usijilazimishe sana kama hutawezi kuvifuata vyote. Ukishindwa kuvifuata vyote, basi angalau jaribu kufuata ile sheria ya asilimia 80 kwa 20.

Sheria hiyo inasema kwamba iwapo utakuwa ukila na kunywa vizuri kama inavyotakiwa kwa kiwango cha silimia 80, basi hata kama ikitokea ukala na kunywa vibaya kwa kiwango cha asilimia 20, bila shaka mwili wako utaweza kukabiliana na vitu hivyo vya asilimia 20 na vitadhibitiwa kirahisi.

1: KULA MLO WA ASUBUHI (breakfast)

Anza siku kwa kula mlo mzuri ili upate kiwango kizuri cha nishati mwilini na kuwa na uwezo wa kujidhibiti na utakacho kula baadae siku hiyo, ikiwa ni pamoja na kula kiwango kidogo cha sukari na kahawa. Upe mwili wako nishati ya kutosha kwa kunywa uji wa ulezi, mtama au mahindi ya lishe.

2. KUNYWA MAJI YA KUTOSHA (drink enough water)

Kunywa lita mbili za maja kila siku, maji ni muhimu sana kwa ufanisi wa mwili wako. Unaweza kukaa wiki kadhaa bila kula, lakini huwezi kukaa muda huo bila kunywa maji. Kama hujazoea kunywa maji kiasi hicho, basi anza kujizoesha taratibu kwa kunywa kiasi kidogo hadi mwili utakapoweza kufikisha lita 2.

Unaweza kunywa maji kiasi utakachoweza kisha kiasi kingine ukakifidia kwa kunywa sana juisi za matunda, matunda yenyewe, kama vile papai, machungwa, lakini epuka kunywa kahawa. Kama tulivyoona wiki iliyopita, ukiona mkojo wako ni wa njano au kahawia na una harufu kali, elewa mwili wako umepungukiwa maji.

Kipimo kizuri cha kutambua kama umekunywa maji ya kutosha kwa siku, ni kujiwekea mazoea ya kununua au kutumbea na chupa ya maji ya ujazo wa lita moja, ambayo utainywa mara mbili kwa vipindi tofauti vya siku ili kufikia kiwango cha lita 2.

3. TUMIA KAHAWA KIASI KIDOGO

Punguza unywaji wa kahawa, kwa sababu kahawa huwa ni chanzo cha upungufu wa maji mwilini na la msingi zaidi kahawa hukausha maji mwilini! Vile vile kahawa huharibu virutubisho na madini mengi yanayoingia mwilini na vile vile inaweza kukuchangamsha kupita kiasi na kusababisha matatizo ya kiakili.

Jiwekee ukomo wa kunywa kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa siku, usizidishe. Pombe vile vile nayo ina kilevi cha kuchangamsha mwili, hivyo nayo inapaswa kunywewa kwa kiasi kidogo na kwa uangalifu.

4. NUNUA VITU ASILIA (buy fresh)

Penda kununua vitu asilia na hai, kwani kadri vyakula hivyo vitakavyokuwa katika hali yake ya asili ndivyo ambavyo vitakavyoweza kukupatia virutubisho vingi mwilini. Usipenda kununua vyakula vya kwenye makopo na kuacha kununua vitu asilia sokono. Jaribu kununua kila kitu kikiwa halisi, mfano; kama ni nyaya iwe halisi na siyo ya kwenye kopo. Kama maharage, pika mwenyewe, usile ya kwenye kopo.

5. ANDAA MLO WAKO MWENYEWE (prepare your meal)

Andaa chakula chako mwenyewe, vyakula vilivyokwisha pikwa na vile viliivyokwisha tayarisha kabisa, huwa siyo bora kiafya, kwani mara nyingi huwekewa dawa za kuhifadhi na kuongeza maisha ya kukaa dukani, dawa hizo zaweza kuwa na madhara kiafya zinapotumiwa kwa wingi. Aidha vyakula hivyo huwa na kiasi kikubwa cha sukari, chumvi na mafuta mabaya. Unapoandaa mwenyewe chakula, utajua kipi kizuri ukiweke na kipi kibaya ukiache.

Itaendelea wiki ijayo.....

Monday, August 6, 2007

DUNIA TAMBARA BOVU, IMANI IMEKWISHA, INASIKITISHA!


MAUAJI YA KUTISHA

Na Makongoro Oging’
Mauaji ya kutisha yametokea katika mkoa wa Pwani ambapo mkazi mmoja wa kitongoji cha Mihande, Mlandizi wilaya ya Kibaha, Bi. Rehema Maskati ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na mume wake aliyetambulika kwa jina la Stivin Mayala ambaye naye alijiyonga hadi kufa baada ya tukio hilo.

Taarifa zilizopatikana mwishoni mwa wiki iliyopita kutoka kwa watu walio kuwa katika eneo la tukio, zilidai kuwa Bi. Rehema ambaye alikuwa mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Taluka, Mlandizi mwili wake uliokotwa ukiwa katika dimbwi la damu wiki iliyopita majira ya asubuhi.

Mashuhuda hao ambao waliomba majina yao kuhifadhiwa, walisema kuwa inaonekana mwanamke huyo aliuawa katika eneo hilo kwani hakukuwa na mburuzo na damu zilionekana sehemu hiyo ya tukio tu.

Aidha walidai kuwa inasemekana mume wa marehemu alijua muda ambao mkewe alipita katika eneo hilo kwenda kazini kwake ndipo alimvizia kisha kumuua.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Bi. Rehema alikuwa ametengana na mumewe kutokana na migogoro ndani ya nyumba na alikuwa akiishi kwa dada yake huko Mihande ambapo Bw. Mayala alikuwa akiishi Mlandizi B.

Habari zaidi zinasema siku hiyo ya tukio bwana huyo alikutana na mkewe karibu na Mto Mkalama sehemu ambayo alifanyia mauaji, naye kujiyonga hadi kufa katika mti wa mkorosho hatua kama 30 kutoka alipolala mwanamke huyo.

Ndugu wa karibu wa marehemu Rehema ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema mwanaume huyo inadaiwa kuwa alishauriwa na mkewe wakati bado wanaishi pamoja kuwa atahiriwe kitu ambacho kilikuwa kinaleta mgogoro ambapo hata hivyo alikubali kutahiriwa ili waishi kwa amani.

Taarifa zaidi zinadai kuwa pamoja na makubaliano hayo, lakini kulizuka tabia nyingine ya mwanaume huyo kunywa pombe kupita kiasi kisha kurejea nyumbani usiku na mara nyingi alikuwa akikojoa kitandani jambo lililokuwa likimuudhi sana Bi. Rehema.

Aidha madai hayo yameelezwa kuwa ndiyo yaliyosababisha mwanamke akimbie na kuishi na dada yake. Hata hivyo, inasemakana mwanaume huyo alikuwa akimbembeleza mkewe waendelee kuishi pamoja waache tofauti zao, jambo ambalo Bi, Rehema alikuwa hajaafiki ndipo mumewe akafikia hatua hiyo ya kumuua naye kujimaliza.

Imeelezwa kuwa baada ya miili hiyo kuonekana na wapiti njia, ilitolewa taarifa polisi ambapo walifika katika eneo la tukio na kuichukua kwenda kuihifadhi katika chumba cha maiti Hospitali Teule ya Tumbi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani, ACP Andrew Salewi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


MAUAJI YA SINDANO

Dotto Mwaibale na Issa Mnally
Kumeibuka mauaji mapya ya kutumia sindano ya sumu ambapo mfanyabiashara mmoja, Bw. Miasi Nyamatimo (30), Mkazi wa Vingunguti Kiembembuzi jijini Dar es Salaam amenusurika kufa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake usiku na kudungwa sindano mgongoni.

Tukio hilo la aina yake na la kuogopesha, limetokea Agosti mosi mwaka huu ndani ya chumba alichopanga mfanyabiashara huyo muda mfupi aliporejea kutoka kwenye shughuli zake za biashara ya kuuza ng'ombe na mbuzi kwenye mnada wa Pugu.

Akiongea na waandishi wetu wiki iliyopita, Bw. Nyamatimo alisema kwamba siku hiyo alirudi nyumbani kwake saa 2.00 usiku ambapo aliwakuta wapangaji wenzake wakiwa wameingia katika vyumba vyao kujipumzisha.

Alisema baadaye alitoka kwenda kuoga huku mlango wa chumba chake akiwa ameufunga, lakini alisahau kutoa ufunguo.

Bw. Nyamatimo aliendelea kueleza kuwa baada ya kumaliza kuoga aliingia chumbani kwake, ghafla alivamiwa na mtu na kukabwa koo huku akimkandamiza kwenye madumu ya maji yaliokuwepo nyuma ya mlango wa chumba hicho.

Alisema alilazimika kupambana naye huku akishindwa kupiga mayowe ya kuomba msaada kutokana na mtu huyo kuendelea kumkaba kwa nguvu huku akiwa ameufunga mlango wa chumba hicho kwa ndani akitumia mguu wake.

Nyamatimo alisema kwamba alimuuliza kama alikuwa anataka pesa ampe, lakini hakumjibu chochote na katika hali ambayo hakuitegemea mvamizi huyo ambaye alikuwa amevaa soksi ya kuficha sura kama ‘Ninja’ huku mikononi akiwa amevaa soksi za mikononi (gloves), aliingiza mkono wake mmoja katika kaptula yake aliyovaa na kuchomoa sindano ambayo alimchoma nayo mgongoni.

Alisema akiwa amekata tamaa na kuishiwa nguvu, ghafla alisikia kishindo kikubwa cha mlango huo ukifunguka na mvamizi wake kudondoka chini kisha alimuona mama mmoja mpangaji mwenzake aitwaye Mama Jordan akiingia ndani na kuanza kupambana na aliyemchoma sindano huku akisaidiwa na watu wengine.

Bw. Nyamatimo aliendelea kusema kwamba watu hao walimtoa nje mvamizi huyo ambapo waliendelea kumpiga hadi akapoteza fahamu kisha walipiga simu polisi ambao walifika na kuwachukua wote wawili na kuwapeleka Kituo cha Polisi Buguruni.

Alisema baada ya kufika kituoni hapo alidondoka chini na kupoteza fahamu ambapo alikimbizwa Hospitali ya Amana na kupatiwa matibabu na siku iliyofuata aliruhusiwa kurudi nyumbani.

Alifafanua kuwa alipokwenda kumtambua mtuhumiwa huyo kituo cha polisi alishangaa kuona ni binamu yake ambaye siku za nyuma alikuwa akiishi maeneo hayo ya Vingunguti kwa shangazi yake mdogo.

Bw.Nyamatimo aliendelea kusema kwamba ndugu yake huyo alipohojiwa kituoni hapo alidai kuna mtu mmoja alimtuma aende akamuue kwa makubaliano ya kulipwa shilingi 500,000.

Afisa mmoja wa polisi wa Kituo cha Buguruni ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa sio msemaji, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea na upelelezi.


Ubalozi kulipuliwa?

Luqman Maloto na Mashirika ya habari
Hofu imeibuka kwamba huenda Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ukalipuliwa, kufuatia kitisho kilichotolewa hivi karibuni na mmoja wa wanachama watiifu wa Mtandao wa Al - qaeda, Adam Yahiye Gadahn.

Hofu hiyo imeibuka, wakati leo ndiyo inatimia miaka tisa, tangu Balozi za Marekani za Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya zilipolipuliwa Agosti 7, 1998 na kuua mamia ya watu.

Kwa mujibu wa video ya Gadahn, iliyonaswa na Shirika la Habari la CNN, mtandao huo unaandaa shambulio katika balozi zote za Marekani ili kulishikisha adabu taifa hilo kubwa duniani.

Gadahn, raia wa Marekani, alisema, lengo la kulipua balozi hizo ni sehemu ya mkakati wa Al - qaeda kuiwinda Marekani ndani na nje, kama ambavyo nchi hiyo inavyousakama mtandao wao.

"Tunaendelea kuiwinda Marekani ndani na nje, kama ambavyo wao wanavyotuwinda ndani na nje," ilisikika Gadahn ambaye pia anajulikana kama Azzam katika video hiyo.

Akiongelea kitisho hicho, Msemaji wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Richard Kolko alisema, wataalamu wanaifanyia uchunguzi video ya Gadahn kujua mahali alipo.

"Kuongezeka kwa ujumbe wa vitisho kutoka Al- qaeda, kunaweza kuonesha vitu tofauti na watafiti wetu wanafanya kazi na wapelelezi kutathmini kila ujumbe kwa alama na mwongozo," alisema Kolko.

BBA LAUNCH AT SEA CLIF

Ni hivi..... BBA itakuwa ikipatikana Channel 37 saa 24 kila siku, na show ya nusu saa kila siku M-net... Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Lucy Kwhele.. akiteta nami uzinduzini jana sea cliff Hotel
Mmhh...., Nikiwa na mrembo, Miss TZ 2, Jokate Mwegelo tukiwakilisha uzinduzini BBA 2 jana Sea Clif hotel

UCHAFU, USAGAJI!

Na Waandishi Maalum
Pamoja na Serikali kuongeza mkazo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi, inaonekana baadhi ya Watanzania bado hawajali, kwani hivi karibuni kamera yetu iliwabamba warembo wawili wakifanya vitendo vya usagaji chooni.

Warembo hao waliofahamika kwa majina moja moja, Khanifa na Mwaija (pichani kushoto), walibambwa Agosti 2, mwaka huu ndani ya choo kilichopo kwenye Ukumbi wa Baa ya Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakifanya uchafu.

Kamera yetu iliyokuwepo ukumbini humo kushuhudia burudani kutoka kwa Kundi la Jahazi Modern Taarab, ilitonywa na chanzo chetu kimoja kuhusu uwepo wa ‘kamchazo kachafu ka' warembo hao chooni.

Chanzo hicho, jinsia ya kike ambacho kilionesha kukerwa na uchafu wa warembo hao, kilitupasha kuwa, Khanifa na Mwaija walikuwa kero kwa watu wengine kwa sababu waligeuza choo kuwa chumba cha kufanyia mapenzi.

Kiliendelea kutanabahisha kwamba, warembo hao walikuwa wameingia chooni muda mrefu, lakini cha ajabu badala ya kutimiza kilichowapeleka, waliamua kufanya vitendo vya kusagana.
“Wanatia kinyaa, tunaomba mtusaidie, yaani wamevuana nguo, mmoja matiti yako nje, sisi wengine tukienda chooni ni kero tupu,” kilisema chanzo hicho.

Baadaye, katika kupata ukweli wa mambo, ‘paparazi’ wetu wa kike aliingia kwenye choo hicho ambapo aliwakuta warembo hao na kufanikiwa kuwapiga picha wakiwa katika pozi la kimahaba huku wakitomasana.

Hata hivyo, kutokana na kile kilichotafsiriwa kama ni kutokujali, warembo hao waliendelea na mchezo wao bila wasiwasi licha ya kushuhudia wakipigwa picha huku baadhi wateja wakiwataka waondoke chooni.

Aidha, baada ya paparazi wetu kufanikiwa kuwapiga picha wasagaji hao, chanzo chetu kingine kilichodai kinawafahamu warembo hao, kiliwataja majina yao kuwa ni Mwaija na Khanifa ingawa hakikuwatofautisha.

Kilisema, warembo hao wameshakubuhu kwa vitendo vya usagaji na mara wanapozidiwa na kilevi, hushindwa kujizuia na kufanya mapenzi sehemu yoyote.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba kwa sasa wasagaji hao wanaishi kama mke na mume nyumbani kwao, ingawa hakikusema ni sehemu gani ya Jiji la Dar es Salaam.

Gazeti linalaani vikali vitendo vya aina hiyo, kwani siyo tu kwamba vinakwenda kinyume na maadili ya Mtanzania bali pia vinachochea kasi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Tunaiomba serikali idhamirie kukomesha hali hiyo. MHARIRI

The Big Brother Guy - Mwisho Mwampamba.

Mwisho Mwampamba kafika MWISHO!
Na mwandishi wetu Morogoro

Mshiriki wa Tanzania katika Shindano la Big Brother Africa (BBA) mwaka 2003, Mwisho Mwampamba a.k.a Mr. Morogoro, amedaiwa kuwa muuza chips baada ya kufilisika kimaisha.

Mwisho anadaiwa ‘kuchoka’, wakati shindano hilo lililompatia umaarufu na mafanikio kiasi baada ya kushika nafasi ya pili, likizinduliwa tena jana nchini Afrika Kusini, baada ya kusitishwa kwa muda ambapo mshindi wa mwaka huu anatarajia kujipatia Dola za Kimarekani laki moja (shilingi mil. 130).

Ndugu wa karibu na Mwisho, alilipasha gazeti hili kuwa 'staa' huyo ambaye alishika nafasi ya pili BBA, anafanyia biashara hiyo ya kuuza chips katika eneo la Forest, mjini Morogoro.

Mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini aliongeza kuwa Mr. Morogoro anafanya biashara hiyo katika banda ambalo anachangia na kaka yake aitwaye Isambe Mwampamba.

“Mambo yamebadilika, kila kitu kimemuendea mrama, hivi sasa maisha yake ni ya kubahatisha kwa sababu hata hilo banda la chips halimuingizii pesa kama alizokuwa akizipata na kutumia hovyo kipindi alichotoka BBA," alisema ndugu huyo.

Mtoa habari huyo aliongeza: "Wakati mwingine anategemea michango ya ndugu, hivi karibuni ndugu yetu mmoja baada ya kuona kero zimezidi za kila mara Mwisho kumuomba hela, aliamua kumpa daladala ili awe anaendesha usiku.

"Kwahiyo kuna wakati usiku huwa anaendesha daladala ili kuganga njaa, lakini hapendi kuonekana, si unajua ni 'supastaa', kwa kweli tunamhurumia, Mwisho hakuwa mtu wa kupigika kiasi hicho, kwa sababu alikuwa ameshatoka kimaisha".

Jitihada za gazeti hili kumpata Mwisho azungumzie madai hayo ziligonga ukuta, kwakuwa lilielezwa kwamba yupo safarini Dar es Salaam, pia lilipojaribu kumsaka kwa njia ya simu ya mkononi halikufanikiwa kwani namba yake ilikuwa haipatikani.

Alipopatikana kaka yake Mwisho, Isambe Mwampamba alisema kuwa banda la chips ni mali yake, lakini watu wanavumisha ni la Mwisho kwa sababu huwa wanashirikiana, pia huwa anakwenda bandani hapo mara kwa mara.

"Banda ni langu na kwa kuwa Mwisho ni ndugu yangu kuna wakati tulikuwa tunashinda naye pale bandani, sasa watu wanadhani ni lake, ukitaka kuamini hivi sasa nimelifunga kwa sababu nimepata kazi Kiwanda cha Tumbaku," alisema Isambe.

Baada ya tetesi kuzagaa kwamba Mwisho 'ameishiwa', watu mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni tofauti, kuhusiana na mabadiliko ya kimaisha ya Mr. Morogoro huyo.

Wakiongea na gazeti hili mjini hapa, wananchi kadhaa walisema, Mwisho amekumbwa na balaa hilo kwa sababu alikuwa mfujaji wa pesa.

"Aliposhinda BBA alipata mikataba mingi, ikiwemo kurekodi filamu Nigeria, lakini jamaa alikuwa mtu wa matanuzi," alisema Kulwa Ibrahimu wakati Happy Kushamu alieleza: "Mwisho alitaka kuishi kizungu ndiyo maana amewahi kuishiwa.”

Hata hivyo, Chris Kabala alisema, anaamini matatizo ya Mwisho yametokana na laana aliyoachiwa na aliyekuwa mchumba wake, Elpy Zembatakis ambaye anadai alimtosa baada ya kupata mafanikio BBA.

"Laana siyo mpaka itoke kwa wazazi, kitendo cha Mwisho 'kumwaga' Elpy hakikuwa kizuri kabisa, fikiria alikuwa ndiye mchumba wake kabla hajaenda BBA, lakini aliporudi 'alimtosa', hiyo ilikuwa ni laana kwa sababu yule dada aliumia sana.

"Mwisho hakujali alitaka 'masupastaa' wenzake, kama Ray C (Rehema Chalamila) ambaye walitesa na tukasikia walifunga ndoa, lakini haikudumu, mara Rah P (Fredinah Payton), wakatangaza wanaona lakini ndoa yenyewe ikawa hewa tu," alisema Chris.

Sunday, August 5, 2007

BIG BROTHER AFRICA II LIVE LAUNCH!

TUNAWAKILISHAA....! Miss Africa 2005/6 - Nancy Sumary (kulia), sister 'ake Naakaya Sumary na Miss Tanzania namba2, 2006/7 Jokate Mwegelo wakiwakilisha kwenye uzinduzi wa BBA2 uliofanyika Sea Clif Hotel usiku wa kuamkia leo. Mtanzania Richard nd'o mwakilishi wa Bongo ndani ya jumba hilo watakalo kaa kwa siku 98! Richard ana demu wa kizungu, aliagana nae kwa kupeana denda la nguvu kabla ya kujitoma ndani... ambako nako kuna watoto wakali 6..kaazi kweli kweli!Karibuni jamanni eh..! Meneja Mkuu, MultiChoice Tanzania, Peter Fauel, aki-lounchi' rasmi BA2 usiku wa kumakia leo, Sea Clif Hotel
Mtu na Boss wake...hahaa! Lucy Kiwhele (kulia) na Peter Fauel, ambaye ni Meneja Mkuu mpya wa MultChoice Tanzania, wamiliki wa mtandao wa DSTV itakayokuwa ikionesha BBA kupitia Channel 37, @$ 24 hrs a day... whooo!
Meneja uhusiano wa Multichoice Tanzania, Lucy Kiwhele (kulia), akimkaribisha kansela wa ubalozi wa Afrika Kusini nchini, Bw. Mditshwa, kusema machache kuhusu BBA.., asante sana!
Boss wa Africa Media Group (wamiliki wa Channel Ten, Magic FM, DTV) Franco Tamontana (Kati) akiwa na Meneja Mkuu wa MultiChopice Tanzania, Peter Fauel, kwenye 'lounchi' ya BBA2Tupo pamoja: mdau na 'engine' ya Kamati ya Miss Tanzania, Makoye (kushoto), ndani ya Sea Clif kwenye uzinduzi wa BBA2 usiku wa kumakia leo
Kansela wa Ubalozi wa Afrika Kusini, Bw. Victor Mditshwa (kushoto) akiteta na Menaja Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Peter Fauel, wakati wa uzinduzi wa BBA2 usiku wa kuamkia leo
Haa ngoja nikae uzuri....! Resty Ngonyani (kulia) Sales & Marketing Manager wa Africa Media Group, akiwa na mfanyakazi mwenzake Prosper, wote hawa ni 'vigogo' wa Channel Ten, Magic Fm, C2C na DTV!
'Big guy.'..... Mbunifu maarufu wa mitindo ya mavazi ya warembo nchini, Hassanal 'the big guy' nae alikuwepo

MATUMAINI KWA BINTI SOFIA KUTOKA LONDON!

Sofia, binti mdogo (17), mrembo, lakini anaishi katika maisha yenye mateso sana!



leo asubuhi nimetembelewa katika chumba chetu cha habari na Bw. James (pichani kulia) ambaye ni baba mzazi wa binti Sofia anayesumbuliwa na uvimbe wa ajabu miguuni. Amenieleza kwamba, mara baada ya kutolewa kwa habari kuhusu binti yake katika blog hii wiki 2 zilizopita, amepigiwa simu na watu mbalimbali, na hivi karibuni amepata matumaini ya kupona kwa binti yake kutoka kwa Umoja wa Watanzania waishio London, Uingereza, ambao wameahidi kumsaidia binti yake, seriuosly!

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa umoja huo aliyejitambulisha kwa jina moja la Lucas (samahani kama hakuku 'koti' vizuri), Jumamosi ya jana suala hili lingejadiliwa katika mkutano maalum na kuona jinsi ya kuokoa maisha ya binti yake.
Pia kuna msamaria mwema mwingine kutoka Dubai nae ameahidi kumsadia, baada ya kupata maelezo ya kina ya tatizo la binti yake.. shime watanzania tumsaidie binti huyo, naamini inawezekana..... let's change Sofia's life!!


Ifuatayo ndiyo historia ya ugonjwa wa mtoto Sofia na maelezo yaliyotolewa na baba yake mzazi, Bw. James Mwiga, leo asubuhi mbele yangu katika chumba chetu cha habari…....

MIMI Sofia James, nilizaliwa 1990, nina umri wa miaka 17 nilizaliwa mkoani Tabora, wilaya ya Tabora mjini.

Ninaomba msaada wa matibabu ya uvimbe wa miguu yangu, naomba msaada kutoka nchi yoyote itakayo kuwa tayari kunitibu, mimi nakubali endapo nchi yoyote itakuwa tayari kunisaidia. Nasumbuliwa na uvimbe wenye maumivu yapata miaka kumi (10).

MAELEZO MAFUPI ALIPO ANZA KUUGUA SOFIA
Mara baada ya kuzaliwa 1990, mwaka 1998 alianza kupata dalili za uvimbe mdogo miguuni, alipelekwa katika Hospitali mbalimbali Mkoa wa Tabora kwa uchunguzi, lakini hawakubaini tatizo.

Mwaka 2005 hali ilibadilika ghafla baada ya kuvimba sehemu mbalimbali za miguu, mfano wa manundu huku akisikia maumivu makali. Alilazwa kwa muda wa miezi mitano (5) Kitete Hospitali Tabora, kisha akapewa rufaa ya kwenda Muhimbili Government Hospital, Dar es Salaam, Kwa uchunguzi na matibabu zaidi alichukuliwa vipimo Muhimbili na Agakhan Hospital na kuonekana ana tatizo linalojulikana kitaalamu kama Lymphoedema.

Baada ya uchunguzi huo alipangiwa afanyiwe upasuaji awamu sita mara sita kwa siku tofauti, alipangiwa tarehe 04 May 07 apelekwe kwa ajili ya maamdalizi ya upasuaji yaliyopangwa kufanyika tarehe 24-May 07. Alipofikishwa hospitali, madaktari walikaa kikao na kusitisha upasuaji, baada ya kuona mafanikio yatakuwa madogo, wangeweza hatarisha maisha yake badala ya kumuokoa.

Hivi sasa yupo katika hospitali ya Jeshi la Wananchi Tanzania ya Lugalo, jijini Dar es Salaam ambako amepata hifadhi ya kitanda na kusubiri hatma yake, kwa msaada wa Waziri wa Ulinzi, Mh. Juma Kapuya, ambaye ndiye aliyemtoa Tabora.

Kama kuna nchi ambayo itakuwa tayari kumsaidia binti huyu yeye mwenyewe yupo tayari na baba yake yupo tayari( Amekubali).

Kwa mawasaliano zaidi, baba mzazi anawaomba wasamaria wema wote watumie email yangu ya amsalawi@yahoo.com au wawasiliane nae moja kwa moja kwa simu namba: +255 0753 916 690








Saturday, August 4, 2007

Profesa Jay aporwa demu na kizito



Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule ‘Prof. Jay’ anadaiwa kukimbiwa na mchumba wake aitwaye Nice Chande.

Tukio hilo limetokea wiki iliyopita nyumbani kwa mwanamuziki huyo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa marafiki wa karibu wa Nice ni kuwa, mwanamke huyo amehamishwa nyumba kinyemela na kizito mmoja ambaye yuko karibu sana na kiongozi mmoja wa juu wa chama cha siasa nchini (jina tunalihifadhi).

Habari zaidi zimeeleza kuwa kitendo cha mwanamke huyo kutoweka nyumbani kimemsononesha mwanamuziki huyo na kuathiri utendaji wake wa kazi.

“Kama ulikuwepo Leaders kwenye Tamasha la One Mic utakubaliana nasi kuwa Prof. Jay amechanganywa na mapenzi kwani alishindwa kufanya ‘makamuzi ya kufa mtu’ kama ilivyo kawaida yake,” alisema mmoja wa marafiki hao.

Aidha, inadaiwa kuwa Nice alifika nyumbani kwa msanii huyo baada ya kuambiwa hayupo na kuchukua baadhi ya nguo zake kisha kutoweka.

Mwandishi wetu alimtafuta Prof. Jay ‘ the heavy weight’ na kumuhoji kuhusu madai hayo badala ya kujibu, yeye aliuliza “hayo ni mambo ya siri, wewe umeyapataje?”

Hata hivyo, Prof. Jay alisema kuwa, kwa sasa yuko mikoani akifanya kazi zake za muziki hivyo hajui chochote kinachoendelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine Nice alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu madai ya kutoroshwa na kizito, aliomba apewe muda wa dakika tano ndipo ajibu swali.

Alipopigiwa baada ya dakika tano, aliuliza “hizo habari umezipata wapi na nani amekupa, nakuja huko huko ofisini kwenu uniambie aliyekueleza hayo yote,”alisema.

Prof. Jay amekuwa akiishi na msichana huyo kwa muda mrefu kama wachumba na mara kwa mara wamekuwa wakionekana pamoja katika majumba ya starehe.

Prodyuza maarufu afmaniwa

Produza maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Akil Mohamed a.k.a The Brain, hivi karibuni alijikuta akikumbwa na aibu kubwa baada ya kufumaniwa na jimama lake lililojulikana kwa jina moja la Rosemary akiwa na kimwana mwingine.

Tukio hilo la aina yake lilitokea katika Mgahawa wa Steers uliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam ambapo produza huyo alifumwa na mfadhili wake ambaye pia ni mpenzi wake wakiwa katika mahaba mazito.

Waandishi wetu waliokuwepo katika mgahawa huo walimshuhudia Akil akiwa ‘beneti’ na msichana mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja.

Akiwa katika mgahawa huo, Akil na binti huyo waliagiza vinywaji baridi na kuanza kunywa lakini ghafla aliingia dada mmoja aliyeonekana kuwa na umbo kubwa ‘jimama’ na kuanzisha varangati kubwa.

“Wewe msh**** umenigandisha nyumbani muda wote kumbe upo huku na kimada wako, utanikoma,” alisikika jimama huyo akilalama.

Rosemary alionekana kufura kwa hasira alimuuliza Akil “huyu uliyenaye ni nani?” Lakini hakupata majibu.

Kufuatia kutojibiwa jimama hilo limfuata Akil na kumnyanyua msobe msobe na kuanza kumshushia kipigo cha nguvu.

Wakati varangati hilo linaendelea, mwanamke aliyekuwanaye Akil alitimua mbio kuelekea kwenye gari walilokujanalo lililokuwa pembeni ya mgahawa huo na kumuacha produza huyo akichezea kichapo.

Hata hivyo, produza huyo alifanikiwa kuchomoka kwenye mikono ya jimama hilo na kukimbilia katika gari na bila kupoteza muda aliliondoa kwa kasi.

Aidha, mwandishi wetu alimshuhudia Rosemary akiwasha gari lake na kulifuata kwa nyuma gari la produza huyo.

Mwandishi wetu hakuweza kufahamu mara moja nini kilitokea huko walikoelekea.

Thursday, August 2, 2007

WATATU WANA NGOMA!

Wakati zoezi la kupima Ukimwi kwa hiari linaendelea kote nchini, takwimu zilizopo zinaonesha kuwa, hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini inatisha na wasanii wametajwa kuwa miongoni mwa watu walio hatarini zaidi.

Hali hiyo inakuja kufuatia takwimu za hivi karibuni za Tume ya Taifa Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) kuonesha kuwa, kati ya watu kumi waliopimwa, watatu wameathirika na watu hao ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15-49 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.

Aidha takwimu hizo zinabainisha kuwa, kati ya watu milioni 5 waliopima asilimia 7 wameathirika lakini kundi kubwa la wasanii limekuwa likikwepa kwenda kupima afya zao kitendo kinachoashiria kuwa, hawajiamini na afya zao kutokana na mfumo wa maisha wanaoishi.

Hata hivyo, inawezekana hakuna msanii yeyote kati ya wasanii kumi waliotajwa ukurasa wa mbele aliyeathirika lakini, wameshauriwa kwenda kupima afya zao ili waweze kuishi maisha ya uhakika na kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii.

Takwimu za hivi karibuni za Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na masuala ya Ukimwi,UNAIDS zinaonesha kuwa, takribani watanzania wapatao milioni 1.5 wanaishi na virusi vya Ukimwi wakiwemo watu hao maarufu.

Kwa mujibu wa Takwimu hizo, watu milioni 1.3 ya idadi ya wanaoishi na virusi ni wale wenye umri wa kati ya miaka 15-. 45 ambapo wanawake wanaoishi na virusi ni 710,000.

Aidha mtandao wa shirika hilo umetaja kuwa, watoto wanaoishi na virusi vya Ukimwi walio kati ya umri wa miaka 1-14 ni 110, 000 .

Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya wataalam wa afya ambao wanajihusisha na zoezi la upimaji Ukimwi kwa hiari linaloendelea nchini, walisema kuwa wameshangazwa na idadi kubwa ya mastaa kutojitokeza kupima afya zao.

Mmoja wa wataalam hao kutoka kituo cha Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema, tangu zoezi hilo limeanza amewapima wasanii wawili tu.

“Wamejitokeza watu wengi kuja kupima afya zao katika kituo hiki lakini kati ya hao nimewapima wasanii wawili tu ninaowafahamu hali inayoonesha kuwa, wengi wao wanalikwepa zoezi hili,” alisema mtaalamu huyo.

Uchunguzi uliofanywa na Ijumaa umebaini kuwa, baadhi ya mastaa wanaambukizwa virusi vya Ukimwi kufuatia tabia yao ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na kubadilisha baada ya muda mfupi.


Lile shindano la kumtafuta msichana mwenye mvuto wa gazeti la Ijumaa limeanza tena rasmi wiki hii; they are sexy, aren't they? But who is the sexies?

HII NI LAANA TUPU !

Na Mwandishi Wetu

Hii sasa ni laana tupu! Akina mama ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja hivi karibuni walitoa kali ya mwaka baada ya kupandwa na mdadi wa muziki na kufikia hatua ya kuvua nguo hadharani.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita mchana kweupe katika maeneo ya Manzese Tip Top, jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na sherehe ya kumtoa nje mtoto aliyekuwa akitimiza siku arobani.

Chanzo chetu cha habari kilichokuwa katika eneo la tukio kilishuhudia akina mama hao wakipanda jukwaani kushindana kukata viuno huku wengine wakishindwa kuzuia mizuka yao na kujikuta ‘wakichojoa’ nguo na kubaki uchi wa binadamu.

Kufuatia tukio hilo, baadhi ya wananchi hasa wenye heshima zao waliohudhuria sherehe hizo, walilazimika kuziba nyuso zao na wengine kuondoka eneo hilo kukwepa aibu.

“Hii ni hatari, yaani mwanamke na akili zake anafikia hatua ya kuvua nguo mbele ya kadamnasi bila hata chembe ya aibu, nadhani kuna kila sababu ya sherehe kama hizi kupigwa stop,” alisema Bi. Aisha Shabani mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa, sherehe hizo ambazo wanawake hupanda juu ya meza na kukata mauno huku wakionesha sehemu zao nyeti (Kusasambua) ni miongoni mwa mambo yanayochangia kumomonyoka kwa maadili ya nchi yetu.

“Wewe fikiria mwanamke anavua nguo huku watoto wadogo wakishuhudia, unatarajia kizazi cha baadaye kitakuwaje? Mbaya zaidi sasa watoto hao wanashangilia na kuona ni sawa, kwa kweli inaudhi,”alisema mama huyo kwa masikitiko.

Vitendo vya wanawake kuvua nguo wakipandwa na midadi katika sherehe za kutoa mwali, kicheni pati na nyingine za namna hiyo, hasa kwa baadhi ya makabila, vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara hali inayoonesha kuwa, vichwa vya wengi wao vimetawaliwa na ulimbukeni.

Hata hivyo Amani linaiomba serikali kuhakikisha kuwa, sherehe kama hizo ambazo kwa namna moja ama nyingine zinakwenda kinyume na maadili ya kitanzania zinadhibitiwa.



Joti wa Ze Commedy apigwa stop

Kumezuka tafrani kubwa baina ya wazazi na watoto wanaoiga utukutu na vituko vya mwigizaji Lucas Mhuvile ‘Joti’ kiasi cha kufikia hatua ya kumpiga stop mchekeshaji huyo asiharibu tabia za watoto.

Stop hiyo ya wazazi ni mwendelezo wa ile ya wazanzibari ambao nao walimjia juu hivi karibuni msanii huyo kufuatia maneno yake ya mdebwedo na kubonyeza kizenji ambayo yalitafsiriwa kuwakejeli watu wa visiwani.

Wanzazibari hao walieleza kuwa, jinsi msanii huyo anavyoyatumia maneno hayo yanawafanya baadhi ya watu kuamini kuwa wao ni legelege.

“Sisi tunamuomba Joti aache kutunga na kutumia maneno ambayo kwa namna moja ama nyingine yanawadhalilisha baadhi ya watu na akiendelea na tabia yake hiyo, kwa kweli tutamtolea uvivu,” alisikika kijana mmoja mwenye asili ya Zanzibar akisema.

Aidha Amani limeshuhudia wazazi kadhaa, jijini Dar es Salaam, wakiwacharaza bakora watoto wao baada ya kuwaona wakiigiza miondoko ya mchekeshaji huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini.

“Nimemtandika (fimbo) kwa sababu hana adabu, nilimtuma maji, eti anatembea kijoti joti, unajua huyo Joti anatuharibia watoto,” alisema mama Jackson Mkazi wa Sinza, Dar es Salaam.

Kundi la sanaa la Ze Commedy linalorusha kazi zake kupitia kituo cha East African Television, linaundwa na wasanii kibao akiwemo Joti, Mpoki, Masanja, Macregan na Wakuvwanga.