MAUAJI YA KUTISHA
Na Makongoro Oging’
Mauaji ya kutisha yametokea katika mkoa wa Pwani ambapo mkazi mmoja wa kitongoji cha Mihande, Mlandizi wilaya ya Kibaha, Bi. Rehema Maskati ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na mume wake aliyetambulika kwa jina la Stivin Mayala ambaye naye alijiyonga hadi kufa baada ya tukio hilo.
Taarifa zilizopatikana mwishoni mwa wiki iliyopita kutoka kwa watu walio kuwa katika eneo la tukio, zilidai kuwa Bi. Rehema ambaye alikuwa mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Taluka, Mlandizi mwili wake uliokotwa ukiwa katika dimbwi la damu wiki iliyopita majira ya asubuhi.
Mashuhuda hao ambao waliomba majina yao kuhifadhiwa, walisema kuwa inaonekana mwanamke huyo aliuawa katika eneo hilo kwani hakukuwa na mburuzo na damu zilionekana sehemu hiyo ya tukio tu.
Aidha walidai kuwa inasemekana mume wa marehemu alijua muda ambao mkewe alipita katika eneo hilo kwenda kazini kwake ndipo alimvizia kisha kumuua.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Bi. Rehema alikuwa ametengana na mumewe kutokana na migogoro ndani ya nyumba na alikuwa akiishi kwa dada yake huko Mihande ambapo Bw. Mayala alikuwa akiishi Mlandizi B.
Habari zaidi zinasema siku hiyo ya tukio bwana huyo alikutana na mkewe karibu na Mto Mkalama sehemu ambayo alifanyia mauaji, naye kujiyonga hadi kufa katika mti wa mkorosho hatua kama 30 kutoka alipolala mwanamke huyo.
Ndugu wa karibu wa marehemu Rehema ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema mwanaume huyo inadaiwa kuwa alishauriwa na mkewe wakati bado wanaishi pamoja kuwa atahiriwe kitu ambacho kilikuwa kinaleta mgogoro ambapo hata hivyo alikubali kutahiriwa ili waishi kwa amani.
Taarifa zaidi zinadai kuwa pamoja na makubaliano hayo, lakini kulizuka tabia nyingine ya mwanaume huyo kunywa pombe kupita kiasi kisha kurejea nyumbani usiku na mara nyingi alikuwa akikojoa kitandani jambo lililokuwa likimuudhi sana Bi. Rehema.
Aidha madai hayo yameelezwa kuwa ndiyo yaliyosababisha mwanamke akimbie na kuishi na dada yake. Hata hivyo, inasemakana mwanaume huyo alikuwa akimbembeleza mkewe waendelee kuishi pamoja waache tofauti zao, jambo ambalo Bi, Rehema alikuwa hajaafiki ndipo mumewe akafikia hatua hiyo ya kumuua naye kujimaliza.
Imeelezwa kuwa baada ya miili hiyo kuonekana na wapiti njia, ilitolewa taarifa polisi ambapo walifika katika eneo la tukio na kuichukua kwenda kuihifadhi katika chumba cha maiti Hospitali Teule ya Tumbi.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani, ACP Andrew Salewi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
MAUAJI YA SINDANO
Dotto Mwaibale na Issa Mnally
Kumeibuka mauaji mapya ya kutumia sindano ya sumu ambapo mfanyabiashara mmoja, Bw. Miasi Nyamatimo (30), Mkazi wa Vingunguti Kiembembuzi jijini Dar es Salaam amenusurika kufa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake usiku na kudungwa sindano mgongoni.
Tukio hilo la aina yake na la kuogopesha, limetokea Agosti mosi mwaka huu ndani ya chumba alichopanga mfanyabiashara huyo muda mfupi aliporejea kutoka kwenye shughuli zake za biashara ya kuuza ng'ombe na mbuzi kwenye mnada wa Pugu.
Akiongea na waandishi wetu wiki iliyopita, Bw. Nyamatimo alisema kwamba siku hiyo alirudi nyumbani kwake saa 2.00 usiku ambapo aliwakuta wapangaji wenzake wakiwa wameingia katika vyumba vyao kujipumzisha.
Alisema baadaye alitoka kwenda kuoga huku mlango wa chumba chake akiwa ameufunga, lakini alisahau kutoa ufunguo.
Bw. Nyamatimo aliendelea kueleza kuwa baada ya kumaliza kuoga aliingia chumbani kwake, ghafla alivamiwa na mtu na kukabwa koo huku akimkandamiza kwenye madumu ya maji yaliokuwepo nyuma ya mlango wa chumba hicho.
Alisema alilazimika kupambana naye huku akishindwa kupiga mayowe ya kuomba msaada kutokana na mtu huyo kuendelea kumkaba kwa nguvu huku akiwa ameufunga mlango wa chumba hicho kwa ndani akitumia mguu wake.
Nyamatimo alisema kwamba alimuuliza kama alikuwa anataka pesa ampe, lakini hakumjibu chochote na katika hali ambayo hakuitegemea mvamizi huyo ambaye alikuwa amevaa soksi ya kuficha sura kama ‘Ninja’ huku mikononi akiwa amevaa soksi za mikononi (gloves), aliingiza mkono wake mmoja katika kaptula yake aliyovaa na kuchomoa sindano ambayo alimchoma nayo mgongoni.
Alisema akiwa amekata tamaa na kuishiwa nguvu, ghafla alisikia kishindo kikubwa cha mlango huo ukifunguka na mvamizi wake kudondoka chini kisha alimuona mama mmoja mpangaji mwenzake aitwaye Mama Jordan akiingia ndani na kuanza kupambana na aliyemchoma sindano huku akisaidiwa na watu wengine.
Bw. Nyamatimo aliendelea kusema kwamba watu hao walimtoa nje mvamizi huyo ambapo waliendelea kumpiga hadi akapoteza fahamu kisha walipiga simu polisi ambao walifika na kuwachukua wote wawili na kuwapeleka Kituo cha Polisi Buguruni.
Alisema baada ya kufika kituoni hapo alidondoka chini na kupoteza fahamu ambapo alikimbizwa Hospitali ya Amana na kupatiwa matibabu na siku iliyofuata aliruhusiwa kurudi nyumbani.
Alifafanua kuwa alipokwenda kumtambua mtuhumiwa huyo kituo cha polisi alishangaa kuona ni binamu yake ambaye siku za nyuma alikuwa akiishi maeneo hayo ya Vingunguti kwa shangazi yake mdogo.
Bw.Nyamatimo aliendelea kusema kwamba ndugu yake huyo alipohojiwa kituoni hapo alidai kuna mtu mmoja alimtuma aende akamuue kwa makubaliano ya kulipwa shilingi 500,000.
Afisa mmoja wa polisi wa Kituo cha Buguruni ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa sio msemaji, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea na upelelezi.
Ubalozi kulipuliwa?

Luqman Maloto na Mashirika ya habari
Hofu imeibuka kwamba huenda Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ukalipuliwa, kufuatia kitisho kilichotolewa hivi karibuni na mmoja wa wanachama watiifu wa Mtandao wa Al - qaeda, Adam Yahiye Gadahn.
Hofu hiyo imeibuka, wakati leo ndiyo inatimia miaka tisa, tangu Balozi za Marekani za Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya zilipolipuliwa Agosti 7, 1998 na kuua mamia ya watu.
Kwa mujibu wa video ya Gadahn, iliyonaswa na Shirika la Habari la CNN, mtandao huo unaandaa shambulio katika balozi zote za Marekani ili kulishikisha adabu taifa hilo kubwa duniani.
Gadahn, raia wa Marekani, alisema, lengo la kulipua balozi hizo ni sehemu ya mkakati wa Al - qaeda kuiwinda Marekani ndani na nje, kama ambavyo nchi hiyo inavyousakama mtandao wao.
"Tunaendelea kuiwinda Marekani ndani na nje, kama ambavyo wao wanavyotuwinda ndani na nje," ilisikika Gadahn ambaye pia anajulikana kama Azzam katika video hiyo.
Akiongelea kitisho hicho, Msemaji wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Richard Kolko alisema, wataalamu wanaifanyia uchunguzi video ya Gadahn kujua mahali alipo.
"Kuongezeka kwa ujumbe wa vitisho kutoka Al- qaeda, kunaweza kuonesha vitu tofauti na watafiti wetu wanafanya kazi na wapelelezi kutathmini kila ujumbe kwa alama na mwongozo," alisema Kolko.

No comments:
Post a Comment