Friday, May 30, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!

Tuzo za vinara: Leo ni leo Diamond
Leo ndiyo ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa sanaa ya filamu nchini ambao wanashauku ya kutaka kufahamu msanii gani wa muvi ataondoka na tuzo au filamu gani iliyojishindia tuzo ya ubora kwa mwaka 2007/2008, kupitia Tuzo za Vinara ambazo zitatolewa ndani ya UKumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Kabla sijaendelea mbele siyo mbaya kama nikiwatambulisha wakali wa muziki watakaopanda stejini kwa ajili ya kuzipamba zaidi sherehe hizo. Kwa upande wa mashabiki wa muziki wa dansi, timu nzima ya wanenguaji wa Akudo Impact itafanya maajabu kupitia staili yao ya Pekecha pekecha.

Profesa Jay atawakilisha kwa upande wa Hip Hop, huku Matonya akiwabembeleza kwa staili zake za ‘Malove dave’, Nakaaya (PICHANI JUU) pia ataendeleza harakati zake za ukombozi kwa Watanzania wengi, hususan wanawake. Kwa upande wa muziki wa mwambao, Jahazi Morden Taarab watafanya shughuli hiyo, huku vijana wa THT wakionesha uwezo mkubwa wa kucheza na jukwaa kwa shoo zao kali.

Habari kutoka ndani ya One Game Promotions wanaoandaa tuzo hizo, zinasema kwamba kila kitu kiko fresh, kinachosubiriwa ni muda wa shughuli hiyo ya kihistoria kuanza. Tuzo zaidi ya kumi na mbili zinatarajiwa kutolewa leo na tayari mastaa wengi wa muvi waliotajwa kuwania, ‘presha’ ziko juu.

Tuzo hizo zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka zinakujia kwa udhamini mrefu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Global Publishers, Digital Art, Clouds FM, Regency Park Hotel, KIU Investment na Vayle Springs. Siyo ishu ya kukosa mtu wangu.

****************************************************************
H. baba: Ngoma mpya, staili mpya, mkwanja bado kilio
Kutoka maeneo ya Kijitonyama, Dar es Salaam ShowBiz ilipata kupiga stori na Hamisi Ramadhani Baba ‘H. Baba’ ambaye anafanya kazi kupitia ajira ya muziki wa kizazi kipya na kubaini mambo mawili matatu mapya kutoka kwake.

Safu hii ilibaini kwamba, baada ya ukimya wa muda mchizi amerudi tena na ngoma mpya yenye jina la Nibebe iliyomshirikisha msanii mwenye jina la ‘Pasha’. Mbali na hilo H. Baba amebadili staili ya nywele zake, badala ya kunyoa na kuzungusha ‘timbaland’ sasa anasuka na kuachia ndevu pana.

Msanii huyo alisema na safu hii kwamba, pamoja na umaarufu alionao ishu ya maslahi bado inamuumiza kichwa, kwani kazi alizofanya na mkwanja alionao ni vitu viwili tofauti. “Lakini bado sijakata tamaa, nakuja na albamu nyingine ambayo naamini itaniweka mahali pazuri”.
************************************************************

Nyoshi (kushoto) na Choki
Kapt.Komba,Nyoshi Wamchana Choki laivu
Kiongozi wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’, Nyosh El Saadat na Mkurugenzi wa Bendi ya TOT-Respect, Kapt. John Komba (juu) mwanzoni mwa wiki hii ‘walimchana’ laivu staa wa muziki wa dansi nchini, Ally Choki wakimtaka atutulize akili katika muziki.

Ishu hiyo ilitokea ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa bendi ya T-Respect baada ya kusukwa upya. Nyoshi ndiye aliyeanza kumtupia madongo Choki baada ya kupanda jukwaani kwa kumtaka aache tabia yake ya kuhamahama bendi bali sasa atulie ndani ya T-Respect.

“Nasema uache tabia ya kuhamahama bendi, Komba amekupa kila kitu, T-Respect ni bendi nzuri, ina wasanii wazuri pamoja na vyombo vizuri, tulia,” alisema Nyoshi.

Aidha, kiongozi huyo wa FM Academia alimgeukia Kapt. Komba na kumtaka awanunulie pamba za maana wasanii wake ili kulinda heshima yao.

Kwa upande wa Komba, naye alimtaka Choki atulie kwani kila kitu alichokihitaji ameshampa na kwamba anatarajia kumwaga neema zaidi ndani ya T-Respect ikiwa ni pamoja na kuwanunulia basi wanamuziki wake pamoja na lori la kubebea vyombo.

No comments: