Msanii Hamad Ally a.k.a Madee ambaye ndiye staa wa Bongo aliyepiga bonge la ‘intavyuu’ na safu hii. Kutoka kwake msomaji utapata kusikia mawili matatu ambayo ulikuwa hauyafahamu, cheki na Rebeka Bernard aliyeangusha naye stori.
Hot Corner: Mambo vipi Madee?
Madee: Fresh tu, karibu sana.
Hot Corner: Ahsante, unajisikiaje kuwa maarufu?
Madee: Najisikia vizuri kwasababu unanisaidia katika kazi zangu.
Hot Corner: Kitu gani usichokipenda?
Madee: Majungu, bora unipe ‘live’ kuliko kunikalia vikao.
Hot Corner: Nasikia umewahi kuchezea kipigo kwasababu ya wimbo wako, ‘Hip Hop Haiuzi’, ni kweli?
Madee: Kiasi fulani kuna ukweli, kipigo siyo mpaka uchapwe hata maneno ni kipigo tosha.
Hot Corner: Huwezi kuishi bila nini?
Madee: Bila furaha
Hot Corner: Mwanamitindo gani wa Bongo anayekuvutia?
Madee: Khadija Mwanamboka
Hot Corner: Ukipata nafasi ya kukutana na Rais utamshauri nini?
Madee: Aongeze viwanda ili kuboresha ajira kwa vijana.
Hot Corner: Kitu gani kinakufurahisha?
Madee: Nikiamka na afya njema.
Hot Corner: Msanii yupi wa Bongo Fleva anayekuvutia?
Madee: Fid Q
Hot Corner: Malengo yako baada ya miaka 10 yakoje?
Madee: Nataka kuwa mfanyabiashara mashuhuri ndani na nje ya Bongo.
Hot Corner: Unavutiwa na mchumba mwenye tabia zipi?
Madee: Nzuri, zinazokubalika katika jamii.
Hot Corner: Poa Madee nakutakia siku njema.
Madee: Nawe pia
DStv kuwapaisha wasanii wa Bongo ulimwengu mzima
Akipiga stori na safu hii, ndani ya Hoteli ya New Afrika, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultChoice Tanzania, Lucy Kihwele(picani juu), alitamka kwamba kupitia muungano huo vipindi vyote vya TBC1 vitakuwa vikionekana katika chaneli za DStv kwa saa 24.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha TBC1 , Edda Sanga alisema kuwa, hiyo itasaidia kazi za wasanii wa Tanzania kutambulika ulimwengu mzima kupitia DStv.
“Sisi upande wetu tunaufurahia muungano huu kwani sasa vipindi vyetu vitaweza kufika mbali zaidi tofauti na hapo awali,” alisema mtangazaji huyo mkongwe nchini Tanzania. (Taarifa kamili hii hapa kwa kimombo):
Multichoice WELCOMes TBC1 TO THE DStv BOUQUET in TanZANIA
TBC1 will launch on DStv on the 23rd May 2008 at 00:00 CAT. The launch will enable viewers in areas of
“The launch is the result of many months of discussions between MultiChoice and TBC, and follows the inclusion of other free-to-air broadcasting services to local DStv bouquets. There has been very positive feedback from our subscribers in various African countries following the launch of free-to-air channels on the pay-tv bouquets, which enables subscribers to enjoy superior viewing quality”, said
Tido Mhando, Director General TBC, highlighted that “The launch of TBC on the DStv platform represents our commitment to take national broadcasting services into the digital era. Though this agreement with MultiChoice Africa, we will improve quality for all viewers across the country, ensuring they are able to obtain world class viewing quality on both pay- and free-to-view television services.”
MultiChoice
No comments:
Post a Comment