Monday, June 2, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Offside Trick wadondoka Uswazi
Baadhi ya wasanii waliokuwa wanafanya umoja wenye jina la Offside Trick kutoka Visiwani Zanzibar wamedondoka Bongo na kujichanganya kunako familia ya Uswazi kwa ajili ya kutafuta maisha zaidi, huku wakijiita ‘Akenato’.

Wakipiga stori na safu hii, vijana hao, Ramadhani ‘IT’, Mudathur Masoud ‘Da Criss’ na Juma Issa ‘J.I’ wamesema kwamba kilichowafanya wavuke maji na kuja Bara ni kutafuta maslahi zaidi kwani pamoja na kufanya kazi nzuri, wakiwa kwao Zanzibar, ikiwemo ile yenye jina la ‘Tunakuja’ ambayo ilibamba ile mbaya lakini bado mkwanja haujakaa sawa.

“Tumekuja kama Simba aliyejeruhiwa, tunataka kupoteza vibaya kwasababu uwezo wetu katika game unafahamika. Zanzibar tayari hatuna mpinzani, kupitia Uswazi Family tunataka kuwaonesha Watanzania Bara kwamba tunaweza kufanya kila aina ya muziki,” alisema Da Criss. Aidha mchizi alisema kwamba, kwa kuanza kila mmoja atatoka na albamu yake.

Afande Sele achomoa
Kutoka pande za Morogoro, msanii Selemani Msindi a.k.a Afande Sele ‘amechomoa’ uvumi ulionea kwamba ameingia mitini baada ya kuona game gumu ndiyo maana akawa kimya kwa muda, Frank Kadende alicheki naye.

Akipiga stori na safu hii kwa njia ya simu Afande ambaye bado anakomaa na taji la Ufalme wa Rhymes alisema kwamba majukumu ya kifamilia na shoo nyingi sehemu mbalimbali ndiyo vitu vilivyomfanya akawa kimya kihivyo na sasa amerudi na ngoma mpya. ‘’Mimi ni simba dume ntaogopaje wasanii wachanga, kwanza nyimbo zangu zinakaa kwenye Top 10 za redio na masikioni mwa mashabiki muda mrefu.

************************************************************************
Nature: Sitaki kuwa kama mtu yeyote
Kutoka ‘kiumeni’ ndani ya kundi la Wanaume Halisi, kijana Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’ ndiye staa aliyepata kupiga stori na safu hii, mapema wiki iliyopita. Cheki na Rebeka Bernard kwa ‘intavyuu’ zaidi.
Hot Corner: Mambo vipi Nature?
Juma Nature: Poa tu.
Hot Corner: Unajisikiaje kuwa supa staa?
Nature: Najisikia poa.
Hot Corner: Unahisi huwezi kuishi bila nini?
Nature: Pumzi.
Hot Corner: Unavutiwa na mwanamuziki gani wa Bongo?
Nature: Navutiwa na yeyote anayeimba nyimbo za uswahilini.
Hot Corner: Umewahi kukutana na Rais.
Nature: Ndio, kikazi.
Hot Corner: Ukipata nafasi nyingine utamshauri nini?
Nature: Aungalie muziki wetu kwa macho mawili
Hot Corner: Kundi gani la muziki East Afrika unalolizimia zaidi?
Nature: Maumau, vijana wa Kenya hao.
Hot Corner: Unautumia vipi muda wako wa mapumziko?
Nature: Kuchili na washikaji.
Hot Corner: Ungependa kuwa kama nani wa Tanzania au nje?
Nature: Sitaki kuwa kama yeyote, Nature kama Nature.
Hot Corner: Poa, aksante kwa muda wako.
Nature: Poa, hamna shida.
*********************************************************
Big Brother Richard akimkabidhi Thea tuzo ya heshima mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa sherehe za Vinara Awards 2008.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera (shoto), akimkabidhi Ahmed Halfan tuzo ya filamu bora 2008 huku akiangaliwa na mkewe Eliza ambaye pia ndiye kinara wa filamu hiyo.

No comments: