Monday, June 9, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Monalisa:Bado yuko bize na mama yake
Pamoja na kuingia kwenye ndoa mpya, baada ya kuachana na mume wake wa zamani, Tyson, muigizaji mzuri wa michezo ya luninga na muvi, Yvonee Cherry 'Monalisa' ameonesha ni jinsi gani hawezi kucheza mbali na mama yake, Suzana Lewis ‘Natasha’ hata akiolewa, Imelda Mtema amezoza nae.

Ndani ya safu hii Mona amesema kwamba kwa kuwa mama yake ndiyo mtu wake wa karibu zaidi, amecheza naye ndani ya filamu yake mpya aliyoipa jina la Binti Nusa.

“Ndani ya filamu hiyo nipo kivingine zaidi, si Mona yule ambaye watu wamemzoea natumai kila mtu atakubali. Siyo mama yangu Natasha tu, pia nimecheza na wasanii wengine kama Mzee Uloto ‘Mzee Chilo’, Ndumbagu Mesayo ‘Thea’, Sudi, Big, Kambi na wengine,” alisema Mona.
***************************************************************
Mez B: Siwezi kusahau nilivyofanyiwa umafia Malawi
Kutoka ndani ya familia ya Chamber Squad, Moses Bushangama ‘Mez B’ ndiye mchizi aliyepata kupiga stori na Hot Corner na kuongea mambo kibao ambayo wewe msomaji hujawahi kuyasikia kutoka kwake. Khadija Mngwai alipiga nae intavyuu ya ukweli.....

Hot Corner: Mambo vipi mtu wangu?
Mez B: Hamna noma, karibu.
Hot Corner: Kitu gani hukipendi?
Mez B : Sipendelei majungu.
Hot Corner: Nasikia uliwahi kudhulumiwa pesa ulipokuwa Malawi, ni kweli?
Mez B: Ni kweli, siwezi kumsahau promota aliyenifanyia ‘umafia’ huo, kwani alinirudisha nyuma kisanii.
Hot Corner: Unajisikiaje kuwa maarufu?
Mez B: Najisikia furaha.
Hot Corner: Ni nani ambaye huwezi kuishi bila yeye?
Mez B: Bibi yangu kwani nampenda sana.
Hot Corner: Mwanamitindo gani wa Bongo anaye kuvutia?
Mez B: Irene Kiwiya.
Hot Corner: Ukipata nafasi ya kukutana na Rais utamshauri nini?
Mez B: Aweke muziki wa Tanzania mbele kama soka.
Hot Corner: Nini Malengo yako baada ya miaka kumi?
Mez B: Kuwa mfanyabiashara wa kimataifa.
Hot Corner: Unavutiwa na mchumba mwenye tabia zipi?
Mez B: Mwenye heshima.
Hot Corner: Poa Mez B, nashukuru kwa ushirikiano.
Mez B: Bomba, tutakutana siku nyingine.
**************************************************************

No comments: