Monday, July 14, 2008

MWEREKA WA MISS USA!

Mwereka alioupiga Miss USA, Crystle Stewart (pichani juu), katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Miss Universe usiku wa kuamkia leo, umezua mjadala sehemu mbalimbali duniani. Baadhi wamelaumu uvaajii wa viatu virefu na bila kuwa na mazoea ya kuvitembelea sehemu kama hiyo, wengine wamemlauma MC, Jerry Springer kuwa ndiye aliyechangia kuanguka kwake na wengine, hasa Wamarekani wenyewe, wamedai eti Crystle alijiangusha ili apate kuandikwa magazetini na kwenye mtandao na ndivyo ilivyokuwa...kawafunika wote, ishu sasa hivi ni mwereka wake na siyo ushindi wa Miss Universe ambaye ni Dayana Mendoza (22) ambaye pia ni Miss Venezuela.

....Mshiriki Miss Tanzania, nawe wataka umaarufu wa ghafla...jiangushe kwenye fainali zijazo...teh teh ..teh..!
Miss USA, Crystle Stewart, katika vazi la jioni kabla ya kupiga mwereka...
Miss Universe 2008, Dayana Mendoza

No comments: