Nikiwa na na timu ya Customer Care ya Cellulant, Moi Avenue, Nairobi, ambao wamedai wanasumbuliwa sana na vijana wanaoulizia nyimbo mpya za Ray C kwa ajili ya kuweka kwenye Ring Tones.
Pichani (shoto) nikiwa kwenye ofisi za Cellulant- Customer Care, Nairobi pamoja na Pruduct Architect wa kampuni hiyo, Josephat Kimani.
Mwanamuziki Ray C, anasubiriwa kwa hamu nchini Kenya kutoa nyimbo zake mpya kwa ajili ya RingTones kutoka kutika albamu yake mpya baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa Kampuni ya Cellulant ya nchini Kenya, inayojishughulisha na kutoa Ring Tones na mambo mengine kwenye simu za mkononi, watu wengi wamekuwa wakifika kituoni hapo na kuulizia nyimbo zake mpya ili kuweka katika simu zao. Katika gazeti la The Standard, toleo la Leo, kwenye Pull Out ya Pulse, Ray C amepamba ukurasa wa mbele na kunadi ujio wa albamu yake mpya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment