Monday, July 7, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Ray C
Irene Uwoya
Lisa Jensen
Full Kujiachia
Mpenzi mzomaji Wikenda ShowBiz, mambo vipi? Bado tunaendelea kubuni na kukushushia ishu mpya kabisa kupitia hapa.

"Full Kujiachia" itakuwa inakuonyesha picha za mastaa mbalimbali wa Kibongo na kukuuliza kwamba, kama ukipewa nafasi ya kujiachia (kujivinjari faragha) na mmoja kati ya warembo hao maarufu(pichani juu) ungemchagua nani na kwanini?

Kwa kuanza leo tunakudondoshea warembo hao watatu, kisha wewe msomaji utatuambia ukipewa nafasi ya kujiachia na mmoja wao ungemchagua nani? Tuambie kupitia email: wikienda@globalpublisherstz.com, simu +255 0713-403-202 na 0715-110 173. Kila wiki tutakuwa tunachapisha maoni yenu bila kuwabania.
***********************

Top Band kudondoka Tanga
Msanii Khaled Mohamed 'TID' akiwa na timu nzima ya wana Top Band watadondoka Mkoani Tanga na kuangusha bonge la burdani ndani ya ukumbi wa Chuo cha Waalimu (TTC) kilichopo Korogwe.

Wakisema na safu hii waandaaji wa ishu hiyo, Korogwe Traders ambao pia walitoa shavu la kutosha katika Droo kubwa ya Jishindie Safari ya Hong Kong iliyomalizika hivi karibuni kwa kudondosha zawadi flaniflani walitamka kwamba, Top Band wataangusha pati hiyo Julai 25, mwaka huu.

"Hivi sasa tayari shoo hiyo ipo masikioni mwa mashabiki kibao wa Top Band na muziki wa kizazi kipya kwa ujumla, tunachosubiri ni siku tu. Pia kutakuwepo na wakali kibao kutoka TA ambao watasimama jukwaani kuwapiga tafu TID na bendi yake," alisema Stanley Joel Bendera ambaye ndiyo mratibu wa ishu hiyo.
************************

Lord Eyes: Mashabiki wasikilize mistari ya ukweli
Msanii anayeshiriki Shindano la kumtafuta Ijumaa King of Hip Hop, Lord Eyes kutoka ndani ya kundi la Nako 2 Nako amesema kwamba, anatarajia kuibuka na ushindi kutokana na kazi zake kukubalika zaidi mbele ya jamii, Chausiku Omary na Eunice Macha walipiga naye stori.

Lord Eyes alitamka kwamba anao uhakika huo wa kushinda iwapo tu mashabiki watatumia fursa hiyo kumchagua mwana hip hop halisi na si vinginevyo.

"Kwa kweli najisikia fresh tangu mashabiki waliponipa shavu la kushiriki katika mpambano huo. Mashabiki wakae mkao wa kula kwani siwezi kuwaangusha.

"Simuhofii mshiriki yeyote katika shindano hilo, mashabiki wasikilize kwa makini mistari ya nyimbo zetu ili waweze kupata mfalme wa kweli na si kwa kuangalia sura," alisema msanii huyo.

Mratibu wa Shindano hilo Charles Mateso aliwataja wasanii waliochaguliwa na mashabiki kuingia kunako shindano hilo kuwa ni Fid Q, Chid Benz, Kalapina, Profesa Jay, Langa, Kala Jeremiah, Rado, Johmakini, Black Rhino na Lord Eyes.

Aidha Mateso aliwataka wasomaji kuendelea kupiga kura zao na kumchagua msanii wanayeona anapaswa kutwaa taji hilo. "Ili kumchagua mshindi msomaji anatakiwa atume ujumbe mfupi (sms) kwa kuandika neno HP halafu anaacha nafasi, anaandika jina la msanii unayeona anastahili kuwa Ijumaa King of Hip Hop kisha anatuma kwenda namba 15551".
********************************

2 comments:

Anonymous said...

sasa bro mrisho na cc wa huku Turkey tukitaka kumchagua mchizi wetu Joh makin inakuwaje???

au tunatengwa?
na cc pia tunataka kupiga kura!!!

Mrisho's Photography said...

Kaka nafikiri hata wewe waweza kutuma kura yako iwapo huduma ya sms inawezekana kati ya Turkey na Tz. andika +255 15551, hope itafika tu.