Sunday, August 10, 2008

Mshindi Miss Tanzania Arudisha Taji!

Angela(no. 26) siku ya fainali za Miss Tanzania

Mshindi wa taji la Balozi wa Redd’s katika mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu, Angela Lubala amevua taji hilo na kurudisha kwa waandaaji.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Angela alisema amechukua uamuzi huo kutokana na imani yake ya dini ya Kikristo, ambapo yeye anaabudu kanisa liitwalo World Alive International Outreach lililopo Sinza, Dar es Salaam.


Alisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa na mtu na anaona halitakuwa jambo la busara kuendelea kuwa Balozi wa kinywaji cha Redd’s, wakati imani ya dini yake haimruhusu.


Balozi wa Redd's wa mwaka jana, Victoria Martin, akijiandaa kukabidhi 'mikoba' kwa Angela

“Nachukua fursa hii kuiambia jamii kuwa kutokana na imani yangu katika Yesu Kristo, sitaweza kuwakilisha Redd’s kama Redd’s Fashion Ambassador 2008.


“Kwa kuwa mimi si mbinafsi, narudisha taji hili na zawadi zake zote kwa Redd’s, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Vodacom, Lino na Redd’s kwa uelewa juu ya uamuzi wangu huu”, alisema. Vodacom ndio wadhamini wakuu wa Miss Tanzania. Angela ambaye pia ni Miss Temeke 2008, alisema zawadi anayorudisha ni fedha sh. Milioni 2.5.


Alipoulizwa kama hakujua wakati anashiriki mashindano hayo tangu mwanzo kama kuna jambo kama hilo, alisisitiza kuwa suala la kuwa Balozi wa kinywaji hicho haliendani na imani yake.


Balozi wa Redd's wa mwaka jana Victoria Martin, akikabidhi 'mikoba' kwa Angela(kulia)

Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoandaa mashindano hayo, Hashim Lundenga alipoulizwa jana kwa simu alisema yupo nje ya Dar es Salaam, lakini wasaidizi wake pamoja na watu wa Redd’s ambao ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wamethibitisha ni kweli amerudisha taji hilo na kuwa atatoa ufafanuzi zaidi atakaporudi.


Angela Luballa

Mashindano ya Miss Tanzania yalifanyika Agosti 2 ambapo Nasreem Karim (22) ambaye ni Miss Kanda ya Ziwa aliibuka Miss Tanzania 2008 na kuzawadiwa pia gari aina ya Suzuki Grande yenye thamani ya sh. Milioni 42 na fedha taslimu sh. Milioni 8.8.

(kwa wasiofahamu, baba mzazi wa Angela ni mchungaji wa kanisa mwenye imani ya kilokole)

(credits- spoti starehe, Sun 10, 2008)

5 comments:

Anonymous said...

hakuna point yoyote ya yeye kurudisha taji, kama yeye ni mcha mungu haswa, sijui mlokole wherever, ilikuwaje akaingie katika mashindano ya umiss ambayo wasichana wanakuwa nusu uchi, hilo hakuliona, au hao wazazi wake walokole hawakuliona hilo? hata wakamruhusu aingie kwenye mashindano? kwani kuwa balozi wa redds ndio kunywa pombe? bora huo ubalozi wa redds kuliko kukaa uchi mbele za watu, upuuzi mtupu!!!!!!

Anonymous said...

amechemsha huyo binti , kwani hhuo uchmungu umentokea gafla? mbona alidiriki kuziba 10% ya mwili wake wakati wa kinyanga' nyiro ? Mungu kwake alikua wapi? Ana jambo huyooo

Anonymous said...

Upuuzi mtupu!! Kilichomfanya akalipokea ni nini? Hawa ndo wanaingiaga kuwazibia wenzao! unajijua kabisa una ulokole, huko kwenye mambo ya kidunia ulikwenda kutafuta nini? pambaaaafffff

Anonymous said...

USUMBUFU,MSHAMBA KWANI HAKULIJUA HILO TANGU MWANZO KAMA YEYE NI MLOKOLE HUKUTAKIWA KUSHIRIKI TANGU MWANZO NA KWAIMANI HIYO ALIYOSEMA ANATAKA AJULIKANE SAANA NA ANDIKWE YEYE SASA KULIKO MISS TZ NDO YALEYALE YA USA MISS ALIYE JIANGUSHA

Anonymous said...

Kujiachia nusu uchi ni mbaya zaidi kuliko hata kuwa balozi wa Reds.Huenda ameshinikizwa na wazazi wake!