Akizungumza Dar es Salaam jana, Angela alisema amechukua uamuzi huo kutokana na imani yake ya dini ya Kikristo, ambapo yeye anaabudu kanisa liitwalo World Alive International Outreach lililopo Sinza,
Alisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa na mtu na anaona halitakuwa jambo la busara kuendelea kuwa Balozi wa kinywaji cha Redd’s, wakati imani ya dini yake haimruhusu.
“Nachukua fursa hii kuiambia jamii kuwa kutokana na imani yangu katika Yesu Kristo, sitaweza kuwakilisha Redd’s
“Kwa kuwa mimi si mbinafsi, narudisha taji hili na zawadi zake zote kwa Redd’s, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Vodacom, Lino na Redd’s kwa uelewa juu ya uamuzi wangu huu”, alisema. Vodacom ndio wadhamini wakuu wa Miss
Alipoulizwa kama hakujua wakati anashiriki mashindano hayo tangu mwanzo kama kuna jambo kama
Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoandaa mashindano hayo, Hashim Lundenga alipoulizwa jana kwa simu alisema yupo nje ya
Mashindano ya Miss
(kwa wasiofahamu, baba mzazi wa Angela ni mchungaji wa kanisa mwenye imani ya kilokole)
(credits- spoti starehe, Sun 10, 2008)
5 comments:
hakuna point yoyote ya yeye kurudisha taji, kama yeye ni mcha mungu haswa, sijui mlokole wherever, ilikuwaje akaingie katika mashindano ya umiss ambayo wasichana wanakuwa nusu uchi, hilo hakuliona, au hao wazazi wake walokole hawakuliona hilo? hata wakamruhusu aingie kwenye mashindano? kwani kuwa balozi wa redds ndio kunywa pombe? bora huo ubalozi wa redds kuliko kukaa uchi mbele za watu, upuuzi mtupu!!!!!!
amechemsha huyo binti , kwani hhuo uchmungu umentokea gafla? mbona alidiriki kuziba 10% ya mwili wake wakati wa kinyanga' nyiro ? Mungu kwake alikua wapi? Ana jambo huyooo
Upuuzi mtupu!! Kilichomfanya akalipokea ni nini? Hawa ndo wanaingiaga kuwazibia wenzao! unajijua kabisa una ulokole, huko kwenye mambo ya kidunia ulikwenda kutafuta nini? pambaaaafffff
USUMBUFU,MSHAMBA KWANI HAKULIJUA HILO TANGU MWANZO KAMA YEYE NI MLOKOLE HUKUTAKIWA KUSHIRIKI TANGU MWANZO NA KWAIMANI HIYO ALIYOSEMA ANATAKA AJULIKANE SAANA NA ANDIKWE YEYE SASA KULIKO MISS TZ NDO YALEYALE YA USA MISS ALIYE JIANGUSHA
Kujiachia nusu uchi ni mbaya zaidi kuliko hata kuwa balozi wa Reds.Huenda ameshinikizwa na wazazi wake!
Post a Comment