Kutoka Kanda ya Ziwa, Mkoani Mwanza safu hii imepewa ishu kwamba, wanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili, Upendo Nkone na Christina Shusho wanatarajia kumsindikiza msanii Lugo Charles kwenye uzinduzi wa albamu yake mpya ya Injili utakaofanyika ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Desemba 9, mwaka huu.
Akisema na safu hii, Lugo alitamka kwamba, kila kitu kuhusu uzinduzi huo kimeshakamilika, kinachosubiriwa ni siku ya kuwapa neno la Mungu wakazi wa Kanda ya Ziwa ambao wameonesha kulisubiri kwa hamu tamasha hilo kubwa la uzinduzi, ambalo halijawahi kutokea, hasa kwa msanii wa nyimbo za injili wa mkoa huo.
“Nimeshaongea na Upendo na Shusho wote wamenihakikishia kushiriki, namshukuru Mungu kwamba, maandalizi mengine yote yako sawa. Watu watapata neno la Mungu kupitia nyimbo kama Upendo wa Yesu, hapa nilipo, Usifurahi juu yangu, Amina Aleluya na nyingine za Upeno Nkone, bila kusahau za Shusho, kabla hawajatakaswa na nyimbo zangu kama Nimewasamehe, Tupendane, Rafiki mwema, Siku za mwisho, Neno la uzima na nyingine nyingi,” alisema Lugo na kuwataka wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani wajitokeze kwa wingi siku hiyo.

******************************
Compiled by MC George
No comments:
Post a Comment