Ijumaa King of Hip Hop:Ni Prof Jay
Ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wasomaji wa safu hii pamoja na wapenzi wa muziki wa Hip Hop ndiyo hii hapa leo, ambapo tunamtaja msanii aliyeibuka na ushindi kupitia shindano la kumtafuta IJumaa King Of Hip Hop lililoendeshwa na gazeti hili kwa takribani miezi kadhaa.
Mratibu wa shindano hilo, Charles Mateso amemtaja Ijumaa King Of Hip Hop 2008 kuwa ni Joseph Haule ‘Prof. Jay’ ambaye kwa mujibu wa kura za wasomaji na wapenzi wa muziki huo amewaacha mbali washiriki wengine wawili Fareed Kubanda ‘Fid Q’ na John Saimon ‘Johmakini’ alioingia nao katika fainali.
“Baada ya matokeo hayo, hatuna budi kusema kwamba, tunampongeza Jay kwa ushindi huo, tunamshauri aendelee kukaza buti zaidi. Pia tunawapongeza wasanii wote waliyoshiriki katika mpambano huu, tunaamini wote wako fiti kwenye sanaa zao japo kura nyingi zimekwenda kwa Jay.
“Pia tunawashukuru wasomaji na wapenzi wa muziki wa Hip Hop, tunawaomba waendelee kushiriki katika mashindano mengine yajayo na yanayoendelea katika gazeti hili,” alisema Mateso
**********
JK mgeni RASMI THTKwa mara ya kwanza Tanzania, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ataungana na baadhi ya wadau wa burudani kama mgeni rasmi katika tafrija ya kuupongeza mradi wa kukuza na kuendeleza vipaji vya wasanii nchini, Tanzania House Of Talent (THT) kwa kutimiza miaka mitatu tangu ulipoanzishwa, itakayofanyika Desemba 8, mwaka huu ndani ya ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Akipiga stori na ShowBiz, Meneja wa mradi huo, Ruge Mutahaba alisema kwamba, sherehe hizo ambazo zitaanza majira ya saa 1 usiku mpaka saa 5 zitakuwa pia ni maalum kwa ajili ya kuwachangia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao wanalelewa kwenye vituo mbalimbali.
“Kutakuwa na meza maalum za chakula, ambapo kila moja itagharimu kiasi cha dola 1000, kiasi cha pesa kitakachopatikana katika sherehe hiyo kitakwenda kuwasaidia watoto hao wenye vipaji. Baada ya kutoka hapo tutaungana na maelfu ya wapenda burudani wengine katika shoo kubwa itakayofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana usiku huo,” alisema Ruge.
Katika shoo hiyo wakali wa muziki, Eve na fat Joe kutoka Marekani wataangusha bonge la shoo, huku A .Y na Mwana FA wakizindua albamu yao ya pamoja, ‘Habari ndiyo hiyo’.
***********************************
Likizo Tyme: BOYZ II MEN, JOE THOMAS, TANYA, TANTO MENTROWale mastaa wa muziki kutoka Marekani na Jamaika, Boyz II Men, Joe Thomas, Tanto Mentro & Devonte na Tanya Stephens wanaotarajiwa kufanya bonge moja la shoo katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam tayari wamedondoka Bongo, wako tayari kwa shughuli hiyo.
Entertainment Masters (EM) ndiyo waandaaji wa shoo hiyo kubwa, Likizo Tyme, walisema na safu hii kwamba bonge la burudani litaanza kudondoshwa majira ya saa moja usiku, yaani mastaa hao kuanza kushambulia jukwaa kwa awamu.
Kama bado haujakamata tiketi yako, muda bado upo, ukipenda kujiachia ile sehemu ya juu (VIP A) tiketi yake ni shilingi laki moja, elfu hamsini (VIP B) na sehemu ya kawaida ni shilingi elfu ishirini kama utakakata mapema.
Kwanini usijiachie na tiketi yako mapema kuliko kwenda kusumbuka getini ambapo utalipa mkwanja mrefu? Yaani kama utakatia getini utalipa shilingi lakini moja na elfu ishirini kwa ‘VIP A’, Elfu sitini (VIP B) na elfu thelathini kawaida. Hapo vipi?
No comments:
Post a Comment