Fat Joe, Eve Kujiachia na Wabongo leo
Baada ya wabongo kujiachia na mastaa kibao kutoka kiwanja kwenye tamasha la Likizo Tyme wikiendi iliyopita, sasa ni zamu ya mtu mzima Fat Joe, Eve na P-Square ambao kwa pamoja watasababisha furaha ya kutosha leo ndani ya viwanja vya Gymkhana Bongo.
Kwa mujibu wa waandaaji wa ishu hiyo, ‘Str8 Music’ wakali hao wataungana na mastaa kibao wa kibongo katika shoo hiyo wakiwemo Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Ambwene Yesaya ‘A.Y’ ambao watatambulisha albamu yao ya pamoja, ‘Habari ndiyo hiyo’ yenye ngoma kali kama Nangoja Ageuke, Asubuhi na nyingine kibao.
“Tayari Fat Joe na kundi lake la Terror Squard, Eve na P-Square wameshadondoka Bongo, kinachosubiriwa ni muda wa shoo ambayo itaanza majira ya saa mbili usiku mpaka kunakucha. Wasani wengine wa Bongo watakaokuwepo katika shoo hiyo leo ni Profesa Jay, Mr. Blue na wengine kibao,” walisema waandaaji.
Aidha, waandaaji hao walitaja viingilio katika shoo hiyo kuwa ni shilingi elfu kumi kwa wale watakaokata tiketi mapema na shilingi elfu kumi na tano kwa watakaokatia getini. Ebwana ee! Hiyo ni nafasi nyingine kwa wasanii wa Bongo kujifunza baadhi ya maujanja kutoka kwa wakali hao.
Wema anadatisha
Kutoka ndani ya shindano la ‘nani anadatisha’ kupitia midomo yake ambalo liliwavutia wasomaji wengi, tunayofuraha kuwafahamisha kwamba, ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, yaani kumtaja mshindi ndiyo hii Jumatatu ya leo.
Kwa mujibu wa kura za wasomaji na wapenzi wa safu hii, mshindi ni Miss Tanzania 2006, WEMA SEPETU ambaye amemfunika Miss Tanzania 2008, Nasreen Karim kwa asilimia 55 ya kura zote zilizopigwa, kitendo kilichomfanya mpinzani wake huyo aambulie asilimia 45 tu.
Sisi kama waandaaji tunampongeza Wema kwa ushindi huo na ameonesha ni jinsi gani anavyowazingua watu wengi kwa mvuto wa mdomo wake, hasa watoto wa kiume. Pia tunachukua fursa hii kumpongeza Nasreen ambaye alifanikiwa kuingia fainali kwa kuwafunika warembo wengine kibao waliokuwa kwenye mpambano huo ambao unamalizika leo.
Tunarudia kuwakumbusha kwamba, shindano lilianza na warembo kumi, ambao ni Nelly Kamwelu, Maureen Gislary, Irene Uwoya, Jaqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lyin’, Maunda Zorro, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Maimartha Jesse, Jokate Mwegelo, Nasreen Karim na Wema Sepetu aliyeibuka na ushindi.
Pia tunawashukuru wasomaji na wale wote waliofanikisha shindano hili kuwa juu. Mwisho wa mpambano huu ndiyo mwanzo wa mashindano mengine mazuri yajayo, usicheze mbali na safu hii kwani tutaendelea kukuletea vitu vingine vipya kabisa ambavyo haujawahi kuvisoma sehemu yoyote.
Kupitia pande hizi hapa ambapo huwa tunakutana na listi ya mastaa wa kiwanja wa kiume au wa kike waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa wenzao, tunaye malkia wa Hip Hop, Kimberly Denise Jones a.k.a Lil Kim (pichani juu), ukipenda muite Queen Bee au Big Momma aliyezaliwa huko Brooklyn, NY, Marekani.
Kama ilivyo kwa mastaa wengine waliopita, Lil Kim anaweza akawashangaza watu wengi kwa kuwa na listi ndogo ya midume saba aliyoiwahi kujiachia nayo tofauti na anavyofikiriwa, hasa kutokana na tabia yake ilivyo, ya kupendelea kupiga pamba zinaonesha sehemu kubwa ya mwili wake au kupiga picha za kupamba majarida mbalimbali akiwa mtupu.
Mpaka sasa staa huyo wa kike ameshajiachia na mastaa wa kiume saba ambao ni Scott Storch, marehemu Notorious B.I.G., Damian Hardy, Nelly, Ray-J, Jamie Foxx na Tracy Morgan ambaye kupitia mtandao wa intaneti haijawekwa wazi kama bado anaendelea naye au naye wameshazinguana.
Mpaka hapo natumai wale walitutumia meseji nyingi wakitaka kufahamu Lil Kim amewahi kuwa na uhusiano na nani watakuwa wamepata jibu. Je, wewe msomaji ambaye unafunua safu hii leo, ungependa kufahamu staa gani wa nje amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nani? Tuandikie ujumbe mfupi (SMS) kupitia simu namba +255 0715-110 173, nasi tutakudondoshea.
compiled by mc george
Baada ya wabongo kujiachia na mastaa kibao kutoka kiwanja kwenye tamasha la Likizo Tyme wikiendi iliyopita, sasa ni zamu ya mtu mzima Fat Joe, Eve na P-Square ambao kwa pamoja watasababisha furaha ya kutosha leo ndani ya viwanja vya Gymkhana Bongo.
Kwa mujibu wa waandaaji wa ishu hiyo, ‘Str8 Music’ wakali hao wataungana na mastaa kibao wa kibongo katika shoo hiyo wakiwemo Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Ambwene Yesaya ‘A.Y’ ambao watatambulisha albamu yao ya pamoja, ‘Habari ndiyo hiyo’ yenye ngoma kali kama Nangoja Ageuke, Asubuhi na nyingine kibao.
“Tayari Fat Joe na kundi lake la Terror Squard, Eve na P-Square wameshadondoka Bongo, kinachosubiriwa ni muda wa shoo ambayo itaanza majira ya saa mbili usiku mpaka kunakucha. Wasani wengine wa Bongo watakaokuwepo katika shoo hiyo leo ni Profesa Jay, Mr. Blue na wengine kibao,” walisema waandaaji.
Aidha, waandaaji hao walitaja viingilio katika shoo hiyo kuwa ni shilingi elfu kumi kwa wale watakaokata tiketi mapema na shilingi elfu kumi na tano kwa watakaokatia getini. Ebwana ee! Hiyo ni nafasi nyingine kwa wasanii wa Bongo kujifunza baadhi ya maujanja kutoka kwa wakali hao.
Wema anadatisha
Kutoka ndani ya shindano la ‘nani anadatisha’ kupitia midomo yake ambalo liliwavutia wasomaji wengi, tunayofuraha kuwafahamisha kwamba, ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, yaani kumtaja mshindi ndiyo hii Jumatatu ya leo.
Kwa mujibu wa kura za wasomaji na wapenzi wa safu hii, mshindi ni Miss Tanzania 2006, WEMA SEPETU ambaye amemfunika Miss Tanzania 2008, Nasreen Karim kwa asilimia 55 ya kura zote zilizopigwa, kitendo kilichomfanya mpinzani wake huyo aambulie asilimia 45 tu.
Sisi kama waandaaji tunampongeza Wema kwa ushindi huo na ameonesha ni jinsi gani anavyowazingua watu wengi kwa mvuto wa mdomo wake, hasa watoto wa kiume. Pia tunachukua fursa hii kumpongeza Nasreen ambaye alifanikiwa kuingia fainali kwa kuwafunika warembo wengine kibao waliokuwa kwenye mpambano huo ambao unamalizika leo.
Tunarudia kuwakumbusha kwamba, shindano lilianza na warembo kumi, ambao ni Nelly Kamwelu, Maureen Gislary, Irene Uwoya, Jaqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lyin’, Maunda Zorro, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Maimartha Jesse, Jokate Mwegelo, Nasreen Karim na Wema Sepetu aliyeibuka na ushindi.
Pia tunawashukuru wasomaji na wale wote waliofanikisha shindano hili kuwa juu. Mwisho wa mpambano huu ndiyo mwanzo wa mashindano mengine mazuri yajayo, usicheze mbali na safu hii kwani tutaendelea kukuletea vitu vingine vipya kabisa ambavyo haujawahi kuvisoma sehemu yoyote.
*******************************
Lil kim Hawa wote kaangusha nao gariKupitia pande hizi hapa ambapo huwa tunakutana na listi ya mastaa wa kiwanja wa kiume au wa kike waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa wenzao, tunaye malkia wa Hip Hop, Kimberly Denise Jones a.k.a Lil Kim (pichani juu), ukipenda muite Queen Bee au Big Momma aliyezaliwa huko Brooklyn, NY, Marekani.
Kama ilivyo kwa mastaa wengine waliopita, Lil Kim anaweza akawashangaza watu wengi kwa kuwa na listi ndogo ya midume saba aliyoiwahi kujiachia nayo tofauti na anavyofikiriwa, hasa kutokana na tabia yake ilivyo, ya kupendelea kupiga pamba zinaonesha sehemu kubwa ya mwili wake au kupiga picha za kupamba majarida mbalimbali akiwa mtupu.
Mpaka sasa staa huyo wa kike ameshajiachia na mastaa wa kiume saba ambao ni Scott Storch, marehemu Notorious B.I.G., Damian Hardy, Nelly, Ray-J, Jamie Foxx na Tracy Morgan ambaye kupitia mtandao wa intaneti haijawekwa wazi kama bado anaendelea naye au naye wameshazinguana.
Mpaka hapo natumai wale walitutumia meseji nyingi wakitaka kufahamu Lil Kim amewahi kuwa na uhusiano na nani watakuwa wamepata jibu. Je, wewe msomaji ambaye unafunua safu hii leo, ungependa kufahamu staa gani wa nje amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nani? Tuandikie ujumbe mfupi (SMS) kupitia simu namba +255 0715-110 173, nasi tutakudondoshea.
compiled by mc george
1 comment:
na EVE tungependa kujua habari zake mana kuna wengine wanasema ameshawahi kushiriki ktk picha za X mara kibao, je kuna ukweli wowote?????????
Post a Comment