Monday, December 15, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!


Sababu za Nasreen kuchemka

Ikiwa ni siku moja imepita tangu Miss Tanzania 2008-09, Nasreen Karim Abdallah kuangukia mdomo kwenye kinyang’anyiro cha Miss World mwaka huu, sababu za kuchemka kwake zimebainika.

Kwa mujibu wa wadau wa Miss World waliochambua kitatange hicho kilichochukua nafasi katika Jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, Nasreen alichemka kutokana na sababu tatu za msingi.

Wakiongea na gazeti hili, Jumamosi iliyopita mara shindano hilo lilipomalizika bila Nasreen kufika hata hatua ya 15 bora (achilia mbali 10 bora), wadau hao walisema kuwa tatizo kubwa lililommaliza mrembo huyo ni saikolojia.

Wakichambua pointi hiyo, wadau hao walisema kuwa kitendo cha mlimbwende huyo kushinda taji la Miss Tanzania Agosti 2, mwaka huu kisha fainali za dunia kufanyika Desemba 13 ni kipindi kifupi ambacho hakitosholezi kumuandaa mrembo.

Walitolea mfano baadhi ya warembo wa nchi nyingine ambao walipatikana mwaka mmoja kabla, hivyo kupigwa msasa na kuandaliwa vizuri kisaikolojia kwa ajili ya shindao.

Pointi nyingine iliyoelezwa kuwa sababu ya Nasreen kuchemka ni skandali la kutembea na mume wa mtu, Mwinyi Ahmed ambalo liliibuliwa na gazeti hili kabla ya kupokezana na ndugu yake, Ijumaa na kuvuma kwa zaidi ya mwezi mzima.

“Unajua ile skendo itakuwa ilimchanganya sana, ukizingatia liliibuliwa na kuvuma siku chache kabla hajakwea pipa kuelekea Afrika Kusini,” alisema Idrisa Kibene wa Sinza, Dar es Salaam.

Sababu nyingine iliyoelezwa ni mazingira ya nchini Afrika Kusini kwa sababu Nasreen alikuwa hajaizoea nchi hiyo, mpaka pale alipokwenda mwezi mmoja uliopita.
Katika pointi hiyo, Miss Tanzania 1999-2000, Hoyce Temu, alisema juzi kupitia TBC1 kuwa: “Nasreen hajapata muda wa kutosha, mimi nilifuatilia haya mashindano, nikamsoma Miss India mwaka huu ndani ya kipindi kifupi ametembelea Afrika Kusini mara tatu kabla ya mashindano.

“Warembo wa nchi nyingine pia wamefanya hivyo, hiyo inawasaidia kuijua nchi wanayofanyia mashindano kabla na kuizoea hali ya hewa, tunaomba kamati ya Miss Tanzania ifikirie kufanya hivyo kwa warembo wake miaka ijayo.”

Katika shindano hilo ambao mwanzo lilikuwa lifanyike Ukraine lakini baadaye likahamishiwa Afrika Kusini kutokana na mgogoro wa kivita kati ya Urusi na Goergia, mrembo aliyeibuka mshindi ni Miss Urusi, Kseniya Sukhinova, wa pili Gablielle Walcott wa Trinidad na Tobago, wakati mrembo wa India, Parvathy Omanakuttan aliibuka namba tatu.

Warembo wengine waliobahatika kuingia tano bora ni Brigite Santos wa Angola na Tansey Coetzee wa Afrika Kusini.
Choki kumfuata Nyota Ndogo Mombasa

Kutoka ndani ya Bendi ya T-Respect, safu hii imeambiwa kwamba, staa wa muziki wa Bongo, Ally Choki hivi karibuni anatarajia kutimkia Mombasa, Kenya ili kuendelea kujiachia na mwanamuziki wa huko, Nyota Ndogo.

Akilonga na safu hii, Choki aliweka wazi kwamba, kinachompeleka huko siyo kujiweka kwa Nyota Ndogo kama baadhi ya watu wanavyozusha, bali anakwenga kugonga video ya wimbo wake mpya, ‘Usinifiche’ alioshirikiana vyema na binti huyo, mwenye ‘voisi’ ya kutosha.

“Habari za mimi kujiweka kwa Nyota Ndogo, zinazoenezwa na baadhi ya watu zimekuwa kero kwangu, lakini naomba waelewe ni kazi tu, wala siendi mwenyewe ila napelekwa na Respect Company,” alisema Kamarade Ally Choki.

********

1 comment:

Anonymous said...

Hayo ni matokeo ya upendeleo wa kuchagua watu wasiofaa kwa rushwa mbalimbali zikiwemo za ngono.

Washindi wanaofaa huwa hawapewi nafasi Tanzania. Hayo ndiyo matokeo yake. Excusses nyingi hazisaidii lolote.

Mdau USA