Saturday, December 13, 2008

Anusurika kufa baada ya mshale kuzama kwenye kichwa!!

Mwanafunzi wa umri wa miaka 11 nchini China (pichani juu), amenusurika kufa baada ya mshale uliorushwa na rafiki yake kuzama kichwani mwake kupitia kwenye jicho
lake, aliwahishwa hospitali huku mshale huo ukiwa bado umezama kwenye
kichwa chake...

kwa habari zaidi: NIFAHAMISHE.COM

HII INAWEZEKANA KWELI KWENYE RUGBY?

Friday, December 12, 2008

This is wonderful!

Ten-year-old Malia and 7-year-old Sasha joined their parents to shake hands and give holiday wishes to hundreds of people who had been lined up for hours at the food bank on Chicago 's south side.

The soon-to-be first lady said the Obamas wanted to give their children "an understanding of what giving and Thanksgiving is all about."
The Obama family's activities in the courtyard quickly drew the attention of schoolchildren whose windows overlooked the courtyard. They put up a sign against the glass that read: "We love our prez" and screamed when the president-elect waved to them.
"I just wanted to come by and wish everybody a happy Thanksgiving," he said. He then asked the children what they would be eating for Thanksgiving dinner.

Has any other President-Elects done something like this out in public?

CHICAGO - President-elect Barrack Obama and his wife took their daughters to work at a food bank on the day before Thanksgiving, saying they wanted to show the girls the meaning of the holiday, especially when so many people are struggling.

Thursday, December 11, 2008

SHOWING SOME LUV!

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwa na mwenzake K-Sher, waki shoo some luv!

Wednesday, December 10, 2008

SAUTI ZA BUSARA 2009!



Greetings from Zanzibar!

We are just eight weeks away from unwrapping the SIXTH edition of the Sauti za Busara music festival.

After months of searching and selecting, we are confident that we have put together one of the finest music programmes yet. All you have to do is make sure you are in Zanzibar, 12-17 February 2009.

Sauti za Busara (Sounds of Wisdom) is an international festival featuring top-quality musical performances by more than 400 established and upcoming artists (40 groups in total). In six "short" years it has established itself as one of Africa’s leading music festivals. It’s an event that brings people together, under African skies, in appreciation of the rich variety of music from the region. It takes place in an historic open-air fortress on a beautiful tropical island and admission is free to all each day before sunset. Too good to be true? - make sure you don't miss it.

STAILI HII INAKUFAA JIDE!




Wadau na mashabiki wa Lady Jaydee wamevutiwa na gauni alilovaa siku ya sherehe za THT kutimiza miaka mitatu, Rais wa nchi akiwa mgeni rasmi. Wamesema gauni alilovaa lilimpendeza kuliko siku yoyote uliyowahi kuvaa...wameshauri atumie staili hiyo ya uvaaji hata katika shoo zake nyingine na atapendeza zaidi kuliko anapovaa 'kimitego'...ni ujumbe wako Jide!

Tuesday, December 9, 2008

UMUHIMU WA NDIZI MBIVU KWENYE AFYA YAKO


Baada ya kusoma makala yangu ya leo na kuzingatia nilichokiandika, bila shaka utaanza kuingalia ndizi kwa mtizamo tofauti na uliokuwa nao hapo awali. Ndizi mbivu ni tunda maarufu sana duniani lakini ni watu wachache wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo kwenye tunda hili.

Ndizi ina aina tatu za kipikee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama Sucrose, Fructose na Glucose na vile vile ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre) ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.

Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya muda wa dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda muhimu sana kwa wanamichezo. Hata hivyo, nishati siyo faida pekee unayoweza kuipata katika ndizi, ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na kuzuia matatizo mengi ya kiafya:

MFAIDHAIKO WA AKILI (DEPRESSION)
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tataizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi ina kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.

MATATIZO WAKATI WA HEDHI (PMS)
Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.

UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA)
Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upunguvu wa damu kwa sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.

SHINIKIZO LA DAMU
Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo sana cha chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.

Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.

NGUVU YA AKILI
Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti unaonesha kuwa potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kujisomea.

KASUMBA (HANGOVERS)
Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover) ni kunywa ‘Milkshake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.

Mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo juu, ndizi pia husaidia katika matatizo mengine mengi kama vile kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa asidi tumboni, kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.k

Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora, ukiilinganisha na Epo (Apple), ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga mara mbili, vitamin A na chuma mara tano na vitamini na madini mengine mara mbili zaidi ya epo. Mwisho; USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU!
Asanteni kwa kunisoma!

21st Century....

We are becoming lesser by the day

Our communication - Wireless

Our dress - Topless

Our telephone - Cordless

Our cooking - Fireless

Our youth - Jobless

Our food - Fatless

Our labour - Effortless

Our conduct - Worthless

Our relation - Loveless

Our attitude - Careless

Our feelings - Heartless

Our politics - Shameless

Our education - Valueless

Our follies - Countless

Our arguments - Baseless

Our Job - Thankless

Our Salary - Very Very less

Our emails - useless (especially this one)!

JK AIFAGILIA THT

Rais Jakaya Kikwete, Jumatatu alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 3 za kuanzishwa kwa taasisi ya Tanzania House Of Talents, zilizofanyika Karimjee gardens na kusema kuwa amefurahishwa sana na burudani aliyoipata. Pichani akitoa hotuba yake kwa wageni waalikwa.
...wasanii wa THT wakifanya vitu vyao
...baloon likipaa ikiwa ni ishara ya mafanikio ya THT
wadau kutoka Vodacom, Mwamvita Makamba (kushoto) na Fina Mango nao walikuwepo
Afande Sele akisalimiana na First Lady Mama Salma
Mwaciti (kati) akiwa na wasanii wenzake wa THT
Msanii K-sher(kati) akiwa na msanii mwenzie Monica (kushoto) na mbunge wa kuteuliwa Mh. Al-shymaa ambaye ni dada wa Monica wakati wa sherehe hizo
JK katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Flava
JK akiondoka baada ya sherehe huku akisindikizwa na mwenyeji wake Ruge Mutahaba

Monday, December 8, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Fat Joe
Eve
Fat Joe, Eve Kujiachia na Wabongo leo

Baada ya wabongo kujiachia na mastaa kibao kutoka kiwanja kwenye tamasha la Likizo Tyme wikiendi iliyopita, sasa ni zamu ya mtu mzima Fat Joe, Eve na P-Square ambao kwa pamoja watasababisha furaha ya kutosha leo ndani ya viwanja vya Gymkhana Bongo.

Kwa mujibu wa waandaaji wa ishu hiyo, ‘Str8 Music’ wakali hao wataungana na mastaa kibao wa kibongo katika shoo hiyo wakiwemo Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Ambwene Yesaya ‘A.Y’ ambao watatambulisha albamu yao ya pamoja, ‘Habari ndiyo hiyo’ yenye ngoma kali kama Nangoja Ageuke, Asubuhi na nyingine kibao.

“Tayari Fat Joe na kundi lake la Terror Squard, Eve na P-Square wameshadondoka Bongo, kinachosubiriwa ni muda wa shoo ambayo itaanza majira ya saa mbili usiku mpaka kunakucha. Wasani wengine wa Bongo watakaokuwepo katika shoo hiyo leo ni Profesa Jay, Mr. Blue na wengine kibao,” walisema waandaaji.

Aidha, waandaaji hao walitaja viingilio katika shoo hiyo kuwa ni shilingi elfu kumi kwa wale watakaokata tiketi mapema na shilingi elfu kumi na tano kwa watakaokatia getini. Ebwana ee! Hiyo ni nafasi nyingine kwa wasanii wa Bongo kujifunza baadhi ya maujanja kutoka kwa wakali hao.


Wema anadatisha
Kutoka ndani ya shindano la ‘nani anadatisha’ kupitia midomo yake ambalo liliwavutia wasomaji wengi, tunayofuraha kuwafahamisha kwamba, ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, yaani kumtaja mshindi ndiyo hii Jumatatu ya leo.

Kwa mujibu wa kura za wasomaji na wapenzi wa safu hii, mshindi ni Miss Tanzania 2006, WEMA SEPETU ambaye amemfunika Miss Tanzania 2008, Nasreen Karim kwa asilimia 55 ya kura zote zilizopigwa, kitendo kilichomfanya mpinzani wake huyo aambulie asilimia 45 tu.

Sisi kama waandaaji tunampongeza Wema kwa ushindi huo na ameonesha ni jinsi gani anavyowazingua watu wengi kwa mvuto wa mdomo wake, hasa watoto wa kiume. Pia tunachukua fursa hii kumpongeza Nasreen ambaye alifanikiwa kuingia fainali kwa kuwafunika warembo wengine kibao waliokuwa kwenye mpambano huo ambao unamalizika leo.

Tunarudia kuwakumbusha kwamba, shindano lilianza na warembo kumi, ambao ni Nelly Kamwelu, Maureen Gislary, Irene Uwoya, Jaqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lyin’, Maunda Zorro, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Maimartha Jesse, Jokate Mwegelo, Nasreen Karim na Wema Sepetu aliyeibuka na ushindi.

Pia tunawashukuru wasomaji na wale wote waliofanikisha shindano hili kuwa juu. Mwisho wa mpambano huu ndiyo mwanzo wa mashindano mengine mazuri yajayo, usicheze mbali na safu hii kwani tutaendelea kukuletea vitu vingine vipya kabisa ambavyo haujawahi kuvisoma sehemu yoyote.

*******************************
Lil kim Hawa wote kaangusha nao gari
Kupitia pande hizi hapa ambapo huwa tunakutana na listi ya mastaa wa kiwanja wa kiume au wa kike waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa wenzao, tunaye malkia wa Hip Hop, Kimberly Denise Jones a.k.a Lil Kim (pichani juu), ukipenda muite Queen Bee au Big Momma aliyezaliwa huko Brooklyn, NY, Marekani.

Kama ilivyo kwa mastaa wengine waliopita, Lil Kim anaweza akawashangaza watu wengi kwa kuwa na listi ndogo ya midume saba aliyoiwahi kujiachia nayo tofauti na anavyofikiriwa, hasa kutokana na tabia yake ilivyo, ya kupendelea kupiga pamba zinaonesha sehemu kubwa ya mwili wake au kupiga picha za kupamba majarida mbalimbali akiwa mtupu.

Mpaka sasa staa huyo wa kike ameshajiachia na mastaa wa kiume saba ambao ni Scott Storch, marehemu Notorious B.I.G., Damian Hardy, Nelly, Ray-J, Jamie Foxx na Tracy Morgan ambaye kupitia mtandao wa intaneti haijawekwa wazi kama bado anaendelea naye au naye wameshazinguana.

Mpaka hapo natumai wale walitutumia meseji nyingi wakitaka kufahamu Lil Kim amewahi kuwa na uhusiano na nani watakuwa wamepata jibu. Je, wewe msomaji ambaye unafunua safu hii leo, ungependa kufahamu staa gani wa nje amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nani? Tuandikie ujumbe mfupi (SMS) kupitia simu namba +255 0715-110 173, nasi tutakudondoshea.

compiled by mc george

Sunday, December 7, 2008

EID MUBARAK!


WAISLAMU NCHINI TANZANIA, JUMATATU WANASHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD EL-HAJJ, WASOMAJI WANGU WOTE NAWATAKIA KHERI NA IDD NJEMA!