Friday, January 9, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Dark Master Kuwafuata wana Chamber kileleni

Kutoka ndani ya familia ya Chamber Squard ambayo inaundwa na ‘membaz’ kama Ngwea, Noorah na Mez B, msanii Athumani Hamisi a.k.a Dark Master anatarajia kuwafuata wenzie hao kileleni baada ya kukamilisha ngoma zake kadhaa zitakazoibeba albamu yake mpya yenye jina la ‘Mtoto wa Chimwaga’.

Mchizi ambaye amefanya maajabu kanako korasi ya ngoma, ‘Nipe Dili’ ya kwake Ngwea, amesema kwamba, kitu kikubwa kilichomfanya achelewe kutoka kama wenzie ni kutopewa nafasi na wadau japo uwezo wake uko juu katika game ya muziki wa kizazi kipya, lakini hivi sasa wameshamkubali na kinachfuata na kazi tu.

Dark ambaye pia alifanya vyema kunako nyimbo nyingine kama ‘She Got Gwan’ wa Ngwea na ‘Part ya East Zou’ aliyoimba na kundi lake hilo na nyingine alisema na ShowBiz kwamba, kupitia studio za Backyard Records, tayari ana mawe kibao ambayo yataanza kwenda hewani siku si nyingi kwa ajili ya kuitambulisha albamu hiyo ambayo iko tayari. “Ndani kuna kazi kibao zikiwemo, Azimio, Bakora, Kalinga Chibite na nyingine, pia nimewashirikisha wasanii kama Prof. Jay, Sugu, Ngwea, Bushoke na wengine,” alisema.
Wachaji zote: Bado tuko pamoja kwenye mishemishe

Madogo wawili walioamua kufanya ajira yao kupitia game ya muziki wa kizazi kipya, Hery Willbad (Machaji Halisi) na Alex Semkuyu (AMX) wanaounda kundi la Wachaji Zote wamesema na ShowBiz kwamba, bado wako paoja na kwamba wanaendelea kupiga mzigo kama kawaida tofauti na baadhi ya mashabiki ambao wanadai wamesambaratika baada ya kusikika hewani na ngoma kadhaa, Rhobi Chacha anadondoka nayo.

Wakiwa wanasikika na kazi yenye jina la ‘Nisamehe’ ambayo wamemshirikisha ‘Madee’ vijana hao kutoka Moro wamesema kwamba, bado wamesimama imara na wala hakuna kilichotokea kwa upande wao, zaidi ya kuendelea kupambana kunako game kwani mpaka wamefanikiwa kukamilisha albamu moja ambayo bado hawajaipa jina.

“Tumeshafanya kazi zaidi ya nane, hivi karibuni tunatarajia kufanya ngoma nyingine tatu, tukiwashirikisha Afande Sele, Mr. Blue na Nature kwa ajili ya kuifanya albamu iwe na kazi taiti zaidi. Mbali na kufanya kazi hiyo kubwa, tunaomba sapoti kubwa kwa wadau wa sanaa hii ili tufike juu zaidi, kwani uwezo wetu tunauamini,” alisema AMX.

No comments: