Friday, January 16, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!





Jokate: Safari yake imeishia hapa

Safari ya mrembo Jokate Mwigelo kunako shindano hili la kumtafuta staa wa kike mwenye mvuto wa kimahaba ‘Ijumaa Sexiest Girl’ kwa leo inaishia hapa baada ya kuambulia kura chache kutoka kwa wasomaji na wapenzi wa mpambano huu.

Binti huyo analifanya shindano libaki na walimbwende wanne, Irene Uwoya, Hadija Sure, Wema Sepetu na Rose Ndauka ambao wapo katika safari ya kuitafuta tatu bora (Top 3) itakayowajia hivi karibuni.

“Tunawaomba wasomaji na wapenzi wa shindano hili muendelee kutuma kura zenu kwa kuandika ujumbe mfupi (SMS) kupitia simu ya kiganjani ukimtaja mshiriki ambaye unadhani anastahili kuibuka na ushindi, kisha tuma kwenda simu namba 0784-275 714,” alisema mratibu wa shindano hilo, Oscar Ndauka.

No comments: