Monday, January 12, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ

Dunia njia tayari inakimbiza kitaani

Ile albamu ya msanii Rutta Bushoke, ‘Dunia Njia’ ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenda burudani Bongo tayari imedondoka kitaani mwishoni mwa wiki iliyopita na kufanya vyema ndani ya soko gumu la muziki wa kizazi kipya.

Akipiga stori na safu hii muda mchache baada ya albamu hiyo kushuka sokoni, Bushoke alisema kwamba, kila kitu kuhusu usambazaji wanafanya wao wenyewe tofauti na watu wengi walivyozoea kwamba kazi hiyo huwa inafanywa na ‘Wadosi’.

“Dunia Njia ina jumla ya nyimbo kumi na moja, ukiwemo ‘Usiende Mbali’ ambao nilishirikishwa na Juliana wa Uganda, nimeuingiza kwenye albamu yangu ili kuwapa ladha zaidi mashabiki wangu. Kwa kifupi ni albamu ambayo haisimuliki, unachotakiwa kufanya ni kuinunua na kuisikiliza,” alisema Bushoke.

Ngoma nyingine zinazopatikana ndani ya albamu hiyo ni pamoja na Chupa ya Coca’, Nimekuchagua wewe, Nimeshafika, Mapenzi Yaongee na nyingine kibao.
Mwana FA na video ya 3

Baada ya kuufunga mwaka 2008 kwa mafanikio ya kutosha kupitia ngoma zake mbili, ‘Bado nipo nipo’ na ‘Naongea na wewe’, kijana Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ bado yuko na moto kwani hivi tunavyoongea tayari ameshapiga video ya wimbo mwingine mpya unaokwenda kwa jina la ‘Msiache kuongea’ uliyomshirikisha Lad Jaydee.

Muda mchache baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji picha wa video hiyo, FA alisema kwamba, wimbo huo umetengenezwa na Hermy B kupitia studio zake zilizopo pande za Kinondoni, Dar es Salaam, huku video ikiwa imegongwa na Kampuni ya Visualab kupitia mtayarishaji wake, Adam Juma
.
“Hiyo itakuwa ni video ya tatu tangu nilipoanza ‘projekti’ ya albamu yangu mpya, nataka kuwaonesha mashabiki wangu vitu vipya na kwamba bado ninao uwezo wa kuandika vitu tofauti ambavyo vimeizunguka jamii yetu. Siku chache zijazo nitalitaja jina la albamu hiyo ikiwemo siku ya kuitambulisha,” alisema Mwana FA.
Ze Dudu kutafuta kipaji kipya Moshi

Msanii Godfrey Tumaini a.k.a Ze Dudu au Baba Willy ameiambia Abby Cool & MC George kwamba, anatarajia kudondoka pande za Kaskazini mwa Tanzania, kwa ajili ya kusaka kipaji kipya katika game ya muziki wa kizazi kipya kupitia ‘talent show’ itakayofanyika Moshi, Januari 18, mwaka huu kuanzia saa nane mchana.

Dudu alisema kwamba, zoezi hilo ambalo linasimamiwa na Kampuni ya Art in Tanzania lilianzia Dar es Salaam ambapo kipaji kimoja kilipatikana na sasa linaendelea Moshi, kisha sehemu nyingine itakayopangwa. “Lengo ni kuinua na kuendeleza vipaji vipya, kwani wasanii wengi wanaouwezo wa kuimba lakini wanashindwa kujua waanzie wapi”.

Aidha Dudu alisema kwamba, mshindi atarekodi bure katika studio hizo na kusimamiwa na kampuni ya Art in Tanzania.
Sister P: huu ndiyo ujumbe wako

Wiki iliyopita, kupitia hapa ‘Hot Corner’ tulitoa nafasi kwa wasomaji na wapenzi wa msanii Sister P watoe maoni yao kuhusiana na kupotea kwenye game kwa ‘mwanadafada’ huyo pichani juu na hivi ndivyo baadhi yao walivyosema.

Sister P alitoka vizuri alipoanza game, sasa amekuwa kama nguvu ya soda, namshauri kama ameolewa ashughulikie ndoa kuliko kupoteza muda na vitu ambavyo haviwezi. Mrs Ally Ubumbulu, Buguruni, Dar.
***************
Bado anafaa kwenye game, kinachohitajika hapo ni kukaza buti kwani bado tunamuhitaji. Magee Mtanga, Mbinga Stendi.
***************
Kiukweli Sister P kaishiwa kabisa, game lina wakati na mudi yake, ila dadaangu umepotezwa vibaya. Kuwa shabiki tu sister, iko poa. Ghas, Moro
***************
Binafsi namshauri Sister P abaki kuwa shabiki tu, tena ikibidi aolewe kabisa. Kumbe akivaa mavazi ya kike anakuwa mzuri kihivyo? Game awaachie wenyewe. Jackson, Dodoma.
***************
Sister P ni miongoni mwa wasanii wachache wanaofanya muziki wa Hip Hop, komaa, kaza buti kwani game unalijua. Joshua Elinaza, Tegeta, Dar.
Kama vipi abaki kuwa shabiki, awape chansi madogo kina Zena na wengine. Samweli B, Geita, Mwanza.
*******************
Mimi kwa mtazamo wangu naona abaki kuwa shabiki tu, kwani fani inahitaji vina na ujumbe uelimishao jamii. Asanteni sana, Mungu aibariki kazi yenu. Mimi Chitumba Ngasi, raia wa Tanzania lakini kwa sasa naishi Kenya.
*******************
Mimi namshauri ajipange upya kwakuwa muda bado anao. Habiba, Kibweni, Zanzibar.
*******************
Namshauri Sister P kama anaweza kuachana na muziki afanye hivyo kwani sijaona alichofanya kwenye game. Mukebezi Mutoka, Nyasho Mitumbani, Musoma.
*******************
Sister P aendelee na game, asikate tamaa kwani naamini yeye ni kichwa bado. Kinachotakiwa ni kwamba, aendelee na staili yake iliyomtoa. Cosmas Festo, Loliondo.
*******************
Mimi namshauri Sister P aache muziki kama alivyosema Afande Sele “Baadhi wanapenda muziki, japo muziki hauwapendi”. Kwa hiyo aache muziki kwasababu anaupenda lakini wenyewe haumpendi. Naona bora abaki kuwa shabiki, huo ni wangu mtazamo. Hassan Mndeme, big up kwa masela wangu wa Makorola, Tanga.
******************
Mi naona atafute kitu kingine cha kufanya kuliko kutoa singo halafu hazisikiki sana hewani.Evance Mujemula, Dar.
******************
Sister P we mkali, soma game vizuri kisha urudi kundini uwakimbize, mbona unaweza tu! Isumba Ibobo, Magomeni, Tanga.
******************
Sister P akaze buti, mbona kuna wasanii walipotea na kurudi kisha wakakubalika. Anachotakiwa asifanye masihara kwasababu wasanii hivi sasa ni wengi.
*****************
Kwa ushauri wangu huyu ‘mwanadafada’ abaki kuwa shabiki tu, kwani ataendelea kutuboa kwa kuja na kupotea, siyo lazima wote tuimbe. Elias ibrahim, Mwananyamala Komakoma, Dar.
******************
Mimi namshauri aendelee kukomaa kwenye Hip Hop, kitu cha msingi akate, atulie atengeneze kitu cha kueleweka, ni hayo tu. Ommy, Ilala Sokoni, Dar.
******************
Namshauru sister P ajipange upya, aandike mashairi mazuri kwani penye nia pana njia, atatoka tu. Salehe Mdende, Iringa.
******************
Kama vipi abaki kuwa shabiki, kwani amejaribu kutoa singo nyingi lakini zimebuma, awaache wanaoendelea kushaini washaini tu. Joseph, Tanga.

CIARA HARRIS: KAJIACHIA NA WANAUME HAWA TU!

Ciara Harris ndiye staa anayefanya staili tofauti za muziki huko Marekani ambaye leo tunamcheki kunako ‘Ebwana Dah’ yakiwa ni maombi ya wasomaji na wapenzi wengi wa safu hii waliohitaji kuwafahamu mastaa wa kiume waliyowahi kupata chansi ya kujirusha na mrembo huyo.

Pamoja na kuonekana kama hajatulia, hasa katika staili yake ya uvaaji, Ciara hana listi ndefu ya wanaume aliyowahi kujiachia nao kama ilivyokuwa kwa mastaa wengine wa kike na kiume tuliyowahi kuwacheki kupitia safu hii ambayo tuliianzisha mapema mwaka jana.

Kwa mujibu wa mtandao wa intaneti unaodili na uhusiano wa kimapenzi wa mastaa wa kiwanja, Ciara amewahi kujiachia na mastaa wa kiume wanne tu, nawazungumzia ‘bwana mdogo’ Bow Wow, ambaye alianza kujirusha naye tangu mwaka 2005 hadi 2006.

Baada ya Bow Wow alifuatia mcheza filamu maarufu, Michael Ealy ambaye alijiachia na staa huyo wa kike kwa mwaka mmoja tu wa 2006, kabla mwana Hip Hop 50 Cent ‘hajajitwisha mzigo’ 2007. Mwaka jana wa 2008 ilikuwa ni zamu ya mwanamuziki Ludacris kujirusha na Ciara, mpaka sasa bado haijajulikana mrembo huyo mwaka huu kadondokea mdomoni mwa staa gani wa kiume.

Akiwa na umri wa miaka 23 sasa, huku nyota yake ikiwa ni Nge, binti huyo alizaliwa
kwa jina la Ciara Princess Harris, pande za Austin, TX, Marekani October 25, 1985.

Compiled by MC george

1 comment:

.. said...

Halo watu wote, jina langu ni Marvelyn Larry. Kwa muda mrefu, mume wangu alikuwa akiishi katika ghorofa nyingine kutokana na shinikizo la kazi na tulifurahi sana pamoja ingawa alikaa mbali nasi kwa miezi kadhaa. Sikujua mwenzangu wa kazi tayari alikuwa na uhusiano naye jambo ambalo lilimfanya mume wangu anipe talaka bila kutarajia. Nilijua kuna kitu kibaya kwa sababu hatukuwahi kupigana au kubishana kiasi hicho ili kumfanya aondoke. Nilikuwa na kiwewe na natafuta msaada wa kukabiliana na hali hiyo iliyonipeleka kwa DR DAWN kutokana na sifa walizomwagiwa na watu mtandaoni. Tulizungumza kwa kirefu na aliniambia kila kitu nilichohitaji kujua kuhusu kile kilichotokea na utaratibu unaofaa wa kurekebisha matatizo. Alitimiza ahadi zake na kumrudisha mume wangu kwangu na mchakato wa talaka ukafutwa. Sasa mume wangu amerudi nyumbani kwetu na tuna furaha pamoja. Inashangaza sana jinsi watu wanaweza kusaidia watu wengine wakati wanahitaji. Anaweza kukusaidia pia. Mtumie tu ujumbe kupitia WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com