Halle Berry: MIAKA 42, WANAUME 21, MTOTO MMOJA!
Ebwana Dah! leo inadondoka na mkali wa muvi kutoka pande za Marekani, Halle Berry, kama kawaida yetu yakiwa ni maombi ya baadhi ya wasomaji ambao wamekuwa wakijenga uhusiano na safu hii kwa kuifuatilia kwa karibu zaidi.
Mashabiki wengi wa mrembo huyo mzaliwa wa Cleveland, OH waliufahamu zaidi uhusiano wake na aliyekuwa mumewe, mwanamuziki Eric Benet ambao walifunga ndoa 1998 na kusambaratika 2004 kwa kuwa ndiyo ulivuma zaidi.
Lakini ukweli ni kwamba, kabla ya kufunga ndoa na Benet, Halle Berry aliwahi kujirusha na mastaa wa kiume kibao na hata alipoachana na mumewe huyo aliendelea kujiachia na wanaume wengine mpaka hivi karibuni alipojifungua mtoto wake wa kwanza.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘intaneti’, staa huyo wa muvi ya ‘Cat Woman’ kabla hajaolewa na Benet alianza kujiachia na mastaa kama Bill Bob Thornton, Debbie, Allen, Kevin Costner, Terrence Howard, John Ronan, Danny Wood, Wesley Snipes na Orlando Jones.
Wengine ni Spike Lee, Eddie Murphy, Christopher Williams, David Justice, Prince Albert II, Larenz Tate, Warren Beatty ambaye alifuatiwa na Eric Benet aliyeamua kuchukua jumla. Baada ya kumwagana na Benet 2004, Berry aliendelea na Shemar Moore, Fred Durst, Pitof na Michael Ealy.
Hivi sasa, Halle mwenye umri wa miaka 42 amejiweka kwa Gabriel Aubry ambaye ndiye baba wa mtoto wake, Nahla Ariel Aubry aliyezaliwa Julai 20, mwaka jana. Staa huyo alizaliwa Agosti 14, 1966 na kupewa jina la Halle Maria Berry, huku nyota yake ikiwa ni Samaki.
Mwana FA kuchafua anga leo na ngoma mpya, aacha kazi benki
Akiwa anajiandaa kudandia pipa kuelekea Uingereza kwa ajili ya shoo kadhaa zitakazopigwa siku chache zijazo, kijana Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema na safu hii kwamba leo Jumatatu anatarajia kuchafua anga kupitia vituo vya redio na ngoma yake mpya yenye jina la ‘Waache waongee’ iliyomshirikisha Lady Jaydee.
Mchizi alitamka kwamba, wakati wimbo huo ukipasua anga redioni, video yake inaendelea kufanyiwa maujanja zaidi na Adamu wa Visualab kabla ya kudondoka luningani hivi karibuni. “Tayari imeshakamilika, ila kuna vitu vichache kwa ajili ya kuiboresha zaidi”.
Aidha ‘FA’ alisema kwamba, siku kadhaa zijazo anatarajia kurudi shule kwa ajili ya kujiongezea elimu zaidi, ndiyo sababu iliyomfanya aache kazi katika benki ya NBC alipokuwa ameajiriwa. “Niliacha kazi tangu Desemba 30, mwaka jana kwasababu nataka kwenda nje kuchukua ‘Masters’. Nashukuru nilipokuwa kazini mabosi wangu walikuwa wananielewa sana, nikashirikiana nao vizuri, nawashukuru sana kwa hili. Nahisi siwezi kupata mabosi kama hao sehemu yoyote ambayo nitafanya kazi hapo baadae kama mwajiriwa,” alisema FA.

JISHINDIE PAJERO YABAMBA MTAANI
Na Mwandishi Wetu
Bahati Nasibu ya Jishindie Mitsubishi Pajero, inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, imewashika wasomaji wengi mitaani ambapo sasa maelfu wanajitokeza kwa kujaza kuponi za uwakilishi.
Muitikio huo wa wasomaji, unafuatia matangazo yanayofanywa sasa hivi, ikiwemo ‘shoo’ ya barabarani, hivyo kutoa hamasa kwa Watanzania wengi.
Wasomaji wamejionea kwamba bahati nasibu zinazoendeshwa na Global hazipelekwi kiujanja ujanja, kitu ambacho kimetoa imani kwa wasomaji wengi kwamba mshindi ni yule mwenye bahati.
Wasomaji wameombwa kuendelea kununua na kusoma magazeti ya Global kisha kujaza kuponi zinazopatikana kwenye ukurasa wa pili wa kila gazeti kabla ya kuziwasilisha kwenye ofisi zao zilizopo Sinza, Bamaga, Dar es Salaam au kwa wakazi wa mikoani kutumia anuani ya posta iliyoambatanishwa kwenye kuponi.
Mbali na hilo, safari hii watakaofaidika si wasomaji peke yao, bali Global imeandaa baiskeli tatu kwa ajili ya mawakala watatu watakaofanya vizuri kwa kuuza magazeti yake kuliko wengine.
compiled by: mc george

No comments:
Post a Comment