
Pamoja na kutangaza kung’atuka kunako game ya muziki wa kizazi kipya, huku akiendelea kushikilia msimamo wake huo, mkali wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ amewataka wasanii wapya wanaoibukia kwenye sanaa hiyo kutosita kumcheki pindi wanapohitaji msaada kimuziki, Christopher Lissa anashuka nayo.
Akisema na safu hii hivi karibu, memba huyo wa Lafamilia alitamka kwamba, yuko tayari kuwasaidia hasa kwa ushauri wasanii wachanga lengo likiwa ni kuiinua sanaa hiyo na kurithisha uwezo wake kwa wengine.
“Waje wanione, waachane na mawazo potofu kuwa mastaa tunaringa. Hakuna staa anayemdharau msanii mchanga kwani wote tumetokea huko. Nitakuwa tayari kuwasaidia kadri niwezavyo,” alisemaa Chid ambaye ni miongoni mwa wasanii waliompiga tafu Bushoke katika uzinduzi wa albamu yake, ‘Dunia Njia’ uliofanyika Mwanza na Mbeya hivi karibuni.
**************

Staa wa mchezo wa mpira wa tennis kutoka Marekani, Serena Williams ndiye tunamdondosha kunako safu hii leo kama anavyoonekana katika picha ya nguvu, hapo yakiwa ni maombi ya wasomaji wengi wa ‘Ebwana Dah!’.
Unaweza usiamini, lakini ukweli ni kwamba, pamoja na kuwa na umaarufu wa kutisha sambamba na mafanikio ya kutosha, mpaka sasa Serena ameshajiachia na mastaa wa kiume watatu tu.
Kwa mujibu wa mtandao wa intanet, staa huyo wa mpira wa tennis alianza kula raha na kijana Brett Ratner mwaka 2004 mpaka 2006, kabla hajadondokea mikononi kwa mwana Hip Hop Common 2007. Ndani ya mwaka huo huo wa 2007, Serena alijiachia na Jackie Long.
Akiwa na umri wa miaka 27 sasa, Serena bado hajaweka wazi kama ameshamwagana na Common japo alijiachia na Jackie Long. Staa huyo mwenye umbo la miraba minne na nyota ya Punda, alizaliwa Septemba 26, 1981 huko Saginaw, Marekani.
Je, wewe msomaji unatamani kufahamu uhusiano wa kimapenzi wa staa gani wa nje? Tuandikie ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu namba 0715-110 173.
compiled by mc george
2 comments:
naitaji kujua yule mwanadada alocheza filam ya kujifanya ni mkimbizi wa rwanda anaitwa farida kalala
Nataka kujua kuhusu Beyonce
Post a Comment