
Msanii Witness Kaijage ambaye ni mmoja kati ya vijana watatu waliokuwa wanaunda Kundi la Wakilisha kabla halijasambaratika, amesema na ShowBiz kwamba anatamani siku moja ‘cruu’ yao hiyo irudi katika game ili heshima iendelee kuwepo. Edna Katabalo alicheki nae.
“Licha ya kubanwa na majukumu ya hapa na pale, naamini siku moja ‘Wakilisha’ itarudi tena katika gemu, hiki ndicho kitu ambacho nataka mashabiki wetu wafahamu. Kundi lipo, kilichotutenganisha ni harakati za kutafuta maisha,” alisema Witness.
**********

Kiongozi wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat, amesema na ShowBiz kwamba hana bifu na mwanamuziki Ndanda Kosovo kama ilivyowahi kuripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari, Rhobi Chacha alicheki nae.
Ndani ya safu hii, Nyoshi alisema kuwa hawezi kuwa na ugomvi na Mkongomani mwenzake huyo wala mwanamuziki wa bendi yoyote hapa nchini, bali watu wanaoeneza uvumi huo wanalengo la kumchafua.“Nadhani kuna watu wanaeneza maneno hayo kwa lengo la kunichafua ili jamii inione mimi ni mkorofi,” alisema Nyoshi.
********

Kutoka ndani ya Familia ya Hot Pot, iliyopiga kambi pande za Karataka, Dar es Salaam, msanii Suma G ambaye alipotea kwa muda ndani ya game ya muziki wa kizazi kipya ameibukia ndani ya studio za MJ, zilizopo Masaki, Dar es Salaam ambako anapigia kazi hivi sasa.
Akipiga stori na ShowBiz, mchizi alisema kwamba ukimya wake ulikuwa ni wa kujipanga, sasa amepangika na kuibukia kunako studio hizo ambako anapiga kazi na mtayarishaji Maco Chali, kabla ya kuachia ngoma yake mpya yenye jina la ‘Silaha maneno’.
“Kaka huo ni ujio mwingine, ngoma hiyo itatambulisha albamu yangu mpya ambayo nimewapa shavu mastaa kibao kama Fid Q, Nature, Chegge, Hardmad na wengine kibao,” alisema Suma G.
******************************************
Dar es Salaam: Put Your Hands- UP
Baada ya kukamilika kwa mpambano wa kumtafuta staa wa kike mwenye mvuto wa kimapenzi, ‘Ijumaa Sexiest Girl’ ambapo mrembo Irene Uwoya aliibuka na ushindi, ShowBiz inakuletea bonge la shindano lingine, ‘Dar es Salaam Put Your Hands Up’ (Dar es Salaam Mikono Juu) ambalo litawahusu wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka ndani ya wilaya tatu za jiji hili.Mpambano huo una lengo la kutafuta wilaya moja yenye wasanii wakali na utawahusisha mastaa kutoka pande za Ilala, Kinondoni na Temeke, mwisho wa siku, itatajwa iliyoibuka kidedea kama ilivyokuwa kwenye mashindano yaliyopita ndani ya gazeti hili.
Kwa kuanza, wewe msomaji unatakiwa ututumie majina ya wasanii kutoka katika Wilaya ya Kinondoni ambao unadhani wataiwakilisha vyema sehemu yao kunako shindano hili. Tumefanya hivyo kwa kuwa kila wilaya ina wasanii wengi na hatuwezi kuwaweka wote kutokana na ufinyu wa nafasi.
Andika ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu yako ya mkononi ukilitaja jina la msanii kutoka Kinondoni ambaye unadhani anastahili kuiwakilisha wilaya yake, kisha tuma kwenda simu namba 0787-110 173. Wiki ijayo tutazitoa picha na majina ya wasanii watakaotajwa kabla ya kuendelea kuwatafuta wakali wa Ilala na Temeke.
*****
No comments:
Post a Comment