
Wasomaji na wapenzi wa safu hii waliotutumia meseji kibao, wakitaka kufahamu mkali wa Hip Hop kutoka pande za Marekani, Nas Escoba (pichani juu) amewahi kujiachia na mastaa gani wa kike, leo ndiyo siku yao ya kufurahi kwani hii ndiyo listi ya mchizi huyo.
Unaweza usiamini, lakini kwa mujibu wa mtandao ukweli ni kwamba, Nas amewahi kujirusha na mke wa Jay-Z, Beyonce Knowles, akaja kwa demu wa sasa wa Rick Rosse, Foxy Brown. Mabinti wengi aliyowahi kuwapitia ni pamoja na K.D. Aubert, Karrine Steffans na Tracee Ellis Ross ambaye nyota yake ni Nge.
Mastaa wengine wa kike waliowahi kujirusha na Nas ni pamoja na Carmen Bryan (1992- 2001), Mary J. Blige (1997) na Kelis aliyeanza naye tangu 2005 hadi hii leo. Akiwa na umri wa miaka 35 hivi sasa, mchizi alizaliwa Septemba 14, 1973 katika Jiji la Long Island, Queens, huko New York, Marekani na kupewa jina la Nasir Bin Olu Dara Jones.
******************************

Wasanii Juma Kassim ‘Nature’ na Ferouz Mrisho ‘Ferouz’ Ijumaa ya wiki hii, wanatarajia kutambulisha albamu mbili kwa mpigo ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Wakati Nature akitambulisha albamu yenye jina la Tugawane Umasikini, Ferouz atasimama jukwaani na ‘Muziki na vyombo’.
******************************

Wasanii wawili, Baby Madaha (JUU KULIA) na Feisal waliotambulishwa kupitia Shindano la Bongo Star Search 2007, wanatarajia kutimkia nchini India Machi 18, mwaka huu kwa ajili ya kurekodi video za nyimbo zao, Imelda Mtema anashuka nayo.
Akipiga stori na safu hii Mkurugenzi wa Kampuni ya Pilipili Intertainment, Naresh Dhat ambaye ndiye Meneja wa wasanii hao alisema kuwa, ameamua kuwapeleka wasanii hao India ili kuleta mapinduzi mengine katika game ya muziki wa Bongo Flava.
“Wakiwa India watafanya video za nyimbo mbili ambazo ni ‘Indian Fruits’ wa Baby Madaha na ‘Back it up’ walizoimba kwa kushirikiana, huo ni mwanzo tu, tumeanza na wasanii hao wawili lakini lengo kubwa ni kuwasaidia wengi zaidi ambao hawana uwezo kifedha,” alisema meneja huyo.
*******************************

Kutoka ndani ya sanaa ya muziki wa Injili, msanii Flora Mbasha ameiambia safu hii kwamba, anatarajia kuzindua albamu mpya ya video za nyimbo zake yenye jina la ‘Furaha yako’, siku ya Sikukuu ya Pasaka ikiwa ni zawadi kwa wapenzi wa kazi zake, Ester Sylivester alicheki naye.
Staa huyo wa Injili alisema kuwa, sehemu kubwa ya maandalizi ya uzinduzi huo imeshakamilika na siku chache zijazo atalitaja eneo la tukio itakapofanyika shughuli hiyo.
“Nawaomba wapenzi wa nyimbo zangu na muziki wa Injili kwa ujumla wasikose kununua albamu hiyo ya video pamoja na ‘audio’ yake ili wapate kusikia maneno mazuri ya kumtukuza Mungu niliyoongea ndani ya kazi hizo,” alisema Mbasha ambaye bado anaendelea kutamba na nyimbo zake mbalimbali katika fani hiyo.
*****************************
Dar es Salaam Put Your Hands Up inakuja
'Dar es Salaam Put Your Hands Up’ (Dar es Salaam Mikono Juu) ni bonge la mpambano litawahusu wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka ndani ya Wilaya tatu za Jiji hilo la Dar, ambalo linaendeshwa na gazeti ndugu, Ijumaa, linalotoka kila siku ya Ijumaa.
Mpambano huo una lengo la kutafuta wilaya moja yenye wasanii wakali na utawahusisha mastaa kutoka pande za Ilala, Kinondoni na Temeke, mwisho wa siku itatajwa iliyoibuka na ushindi.
Kwa kuanza, wewe msomaji unatakiwa ututumie majina ya wasanii kutoka katika Wilaya ya Kinondoni ambao unadhani wataiwakilisha vyema sehemu yao kunako shindano hili. Andika ujumbe mfupi (SMS) ukilitaja jina la msanii kutoka Kinondoni ambaye unadhani anastahili kuiwakilisha wilaya yake, kisha tuma kwenda simu namba 0787-110 173. Mwisho wa kupokea kura yako ni Jumatano mchana wiki hii.
***********************************
1 comment:
MBONA HII HABARI YA BEYONCE INAKINZANA (inatofautiana) NA HII HAPA http://www.nifahamishe.com/entertainment.aspx?NewsID=1408406
LIPI KWELI KWA HAPA sasa?
mdauz j
Post a Comment