

DAR ES SALAAM HANDS UPKupitia shindano lako la kijanja, ‘Dar es Salaam Hands Up’ (Dar es Salaam Mikono Juu) bado tunaendelea kupokea kura zenu wasomaji na wapenzi wa mpambano huu ambao ndiyo majaji wetu mpaka pale tutakapoanza zoezi la kutoana.
Mpambano huu ambao ulianza rasmi wiki iliyopita kwa kuzikutanisha Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni, Ilala na Temeke tayari umeanza kujikusanyia mashabiki wengi, huku kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kufahamu mwisho wa siku ipi itaibuka na ushindi.
Kama kawaida zoezi letu la kupiga kura liko vilevile, unachotakiwa kufanya wewe msomaji na mpenzi wa shindano hili, bila kuwasahau wadau wa burudani, hasa waishio Dar es Salaam ni kuandika ujumbe mfupi (SMS) ukilitaja jina la wilaya ambayo unadhani ina wasanii wakali kisha tuma kwenda simu namba 0787-110 173. Kura yako ndiyo itaifanya wilaya yenye wakali wa Bongo Flava iwe juu.
******************************************

Jhikoman yuko tayari
Kutoka pande za Bagamoyo Mkoani Pwani, msanii anayeendelea kukomaa kunako game ya muziki wa Reggae Bongo, Jhikoman yuko tayari kuitambulisha albamu yake mpya yenye jina la ‘Yapo’.
Akipiga stori na ShowBiz kwa njia ya mtandao, msanii huyo alisema kwamba shughuli hiyo kubwa itapigwa Aprili 18, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Sweet Eazy uliopo maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam na kwamba kila kitu kuhusu ishu hiyo kinakwenda kama kilivyopangwa.
“Nimeshaitambulisha sehemu mbalimbali ikiwemo kwetu Bagamoyo na kwingine, sasa ni zamu ya Dar es Salaam ambapo kiingilio kitakuwa ni buku 5 kwa kila mtu. Napenda watu wafahamu kwamba, muziki wa reggae bado uko juu ila wapo watu wachache ambao wanaufanya usiendelee zaidi hapa Bongo,” alisema.
Kutoka pande za Bagamoyo Mkoani Pwani, msanii anayeendelea kukomaa kunako game ya muziki wa Reggae Bongo, Jhikoman yuko tayari kuitambulisha albamu yake mpya yenye jina la ‘Yapo’.
Akipiga stori na ShowBiz kwa njia ya mtandao, msanii huyo alisema kwamba shughuli hiyo kubwa itapigwa Aprili 18, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Sweet Eazy uliopo maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam na kwamba kila kitu kuhusu ishu hiyo kinakwenda kama kilivyopangwa.
“Nimeshaitambulisha sehemu mbalimbali ikiwemo kwetu Bagamoyo na kwingine, sasa ni zamu ya Dar es Salaam ambapo kiingilio kitakuwa ni buku 5 kwa kila mtu. Napenda watu wafahamu kwamba, muziki wa reggae bado uko juu ila wapo watu wachache ambao wanaufanya usiendelee zaidi hapa Bongo,” alisema.
*********************************************
GK Kumbe anapiga buku!liyekuwa kiongozi wa kundi lililosambaratika, East Coast Team (ECT), lililokuwa na maskani yake pande za Upanga, Dar es Salaam, Gwamaka Kaihula ‘King Crayz GK’ ameamua kurejea darasani kupiga buku kwa ajili ya kujiongezea maujuzi zaidi, ShowBiz imebaini, Christopher Lissa anashuka nayo.
Baada ya kumtafuta kwa siku kadhaa bila mafanikio, huku simu yake ya mkononi ikiwa haipatikani, safu hii iliamua kudondoka kitaani kwao pande za Upanga na kuzama hadi anapoishi GK, ilipomkosa iliamua kupiga stori na washkaji zake wa karibu nyumbani hapo ambao walidai kwamba mchizi ameamua kurudi shule kusomea masuala ya Diplomasia katika chuo kinachotoa elimu hiyo kilichopo maeneo ya Kurasini, Dar es Salaam.
“Ah! GK huwezi kumpata kwa sasa, siku hizi anasoma katika Chuo cha masuala ya Diplomasia,” alieleza msela wake mmoja ambaye hakupenda kuuza jina gazetini. Hata hivyo, msela huyo alidai kuwa, ukimya wa GK utamalizika kwa kishindo kikuu kutokana na maandalizi anayoyafanya kimuziki.
*************************************
TX Junior: FM academia hewa safiMsanii chipukizi wa muziki wa dansi, Hassan Moshi ‘TX Jounior’ ambaye hivi karibuni alidondokea ndani ya Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ akitokea Msondo, tayari ameanza kujipa ujiko kwamba ndani ya bendi yake hiyo mpya atafanya vitu vya nguvu kwa kuwa kuna hewa safi, Issa Mnally alisema naye.
Akipiga stori na ShowBiz ndani ya Ukumbi wa Msasani Club, Dar es Salaam hivi karibuni, Hassan alisema kuwa anachoangalia kwa sasa ni kukuza kipaji chake cha kuimba na maslahi zaidi kwani anaamini muziki ndiyo maisha yake kama alivyoachiwa wosia na marehemu baba yake, TX Moshi William.
“Sasa nimeshaanza kuvuta hewa safi hapa Fm Academia, nawaambia wale mashabiki ambao walikuwa hawajapata nafasi ya kuniona waje waone makeke yangu,” alijifagilia mwanamuziki huyo bila kujua kwamba, mashabiki ndiyo wenye uwezo wa kuamua nani mkali na nani hayuko fiti kunako sanaa ya muziki.
***************************************
Witness yuko Kiafrika Mashariki zaidiKatika kile kinachoonesha kwamba, wasanii wa Kibongo kupitia game ya muziki wa kizazi kipya wanazidi kupasua anga kupitia game hiyo, msanii Witnes Kaijage anayegonga staili ngumu ya Hip Hop siku chache zijazo anatarajia kuanza ziara katika nchi za Afrika Mashariki, Edna Katabalo aliangusha naye stori.
Ndani ya ShowBiz, Witnes alisema kuwa, hiyo itakuwa ni mara yake ya kwanza kuzunguka Afrika Mashariki na anaamini muziki wa Bongo Flava utazidi kutambulika zaidi katika ukanda wa Afrika na nchi za mbali zaidi.
“Hiyo itakuwa ni hatua nyingine kubwa kwangu, kwa kuwazungukia watu wangu wa Afrika. Nilipoingia kwenye muziki na kuanza kufahamika nilikuwa na ndoto za kwenda kimataifa zaidi kitu ambacho kimekuwa kweli kwani kwa kiasi fulani nimefanikiwa na sasa ni wakati wa kuzunguka Afrika,” alisema Witnes.
Msanii huyo aliongeza kuwa, ziara hiyo itaanzia hapa hapa Bongo ambapo kabla ya kuondoka atapiga shoo ya nguvu kisha kuendelea katika nchi nyingine. Witnes ambaye kupitia video ya wimbo wake, ‘Ziro’ alifanikiwa kuibuka na tuzo ya Channel O ni miongoni mwa wasanii watatu waliokuwa wanaunda kundi la Wakilisha.
Imeandaliwa na MC George
No comments:
Post a Comment