Wednesday, April 29, 2009

MAAFA MBAGALA!



Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyoko Mbagal Kizuiani, inalipuka na nyumba zilizopo jirani na kambi hiyo baadhi zimeshika moto!! Habari kutoka kwenye eneo la tukio zinasema kuwa, mabomu hayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye ghala la silaha la kambi hiyo na yamekuwa yakiripuka kila baada ya sekendu chache na yanendelea kulipuka hadi wakati huu tunawaletea taarifa hii. Kishindo cha milipuko ya mabomu hayo, ambayo yameleta hofu kubwa katika jiji la Dar es salaam, hasa maeneo ya Mbagala, Mtoni kwa Azizi Ally na maeneo ya Temeke, kimekuwa kikisikika hadi maeneo ya Mwenge.
PICHA ZAIDI NENDA: global publishers

1 comment:

Anonymous said...

anafanya makamuzi tarehe gani na wapi, mbona hakuna hata poster!