Tuesday, April 14, 2009

UNUNUZI WA VIFAA VYA ENEMA


NAMSHUKURU Mungu kuwa mada yetu ya wiki iliyopita, ambayo imekuwa ikiandikwa mfululuzo kwa majuma manne, imekamilika wiki iliyopita na kuwavutia wasomaji wengi. Napenda kuwahakikishia wale wote walivutiwa na makala hizo na kuamua kuchukua hatua ya kufanya enema, kuwa wameamua jambo muhumi sana katika maisha yao.

Nasema hayo kwa sababu mimi mwenyewe ni shahidi wa jambo hilo, utakapofanya Enema vizuri utakuwa mtu tofauti na siku nyingine, kwani utakuwa umeutua ‘mzigo’ mzito ambao umekuwa ukibeba kila siku bila wewe mwenyewe kujijua.

Suala la msingi kuzingatiwa baada ya kufanya enema ni kujiepusha na ulaji wa vyakula visivyokuwa na manufaa kiafya na badala yake uanze kujenga tabia ya kupenda kula vyakula vilivyo bora kiafya, huku ukitilia maanani ulaji wa matunda, mboga za majani na vyakula vingine vya asili, bila kusahau kunywa maji ya kutosha kila siku, wastani wa lita moja mpaka tatu.

Swali kubwa nililoulizwa na wasomaji wengi lilikuwa ni wapi vinapatikana vifaa vya kufanyia hiyo enema, ambavyo vinajulikana kitaalamu kama ENEMA KIT. Wasomaji wetu wengi walioridhishwa na maelezo tuliyoyatoa, walipenda kuifanya hiyo enema ili kupata faida zake.

Vifaa vya kufanyia enema vipo vingi jijini Dar es Salaam na vinapatikana katika maduka yanayouza vifaa vya hospitali. Maduka hayo kwa Jiji la Dar es Salaam yapo maeneo ya Kisutu mitaa ya Jamhuri na Morogoro ambako ukiuliza unaweza kuoneshwa yalipo. Pia na sehemu nyingine unazojua kuna maduka kama hayo.

Kuna aina mbili za Enema Kit ambazo zinatofautiana katika kifaa cha kuwekea maji. Kuna kifaa cha kuwekea maji ambacho ni cha mpira (sachet) na kingine ni cha bati (steel) ambavyo vyote vinafanya kazi moja. Uchaguzi wa kununua cha bati au mpira, unategemea na ubebaji.

Kwa mtu ambaye atalazimika kutembea au kuhama na kifaa hicho kutoka sehemu moja kwenda nyingine mara kwa mara, kifaa cha mpira kinaweza kuwa bora kwake kwa sababu ubebaji wake ni rahisi, kinaweza kuwekwa hata kwenye mkoba wa kwapani.

Kifaa cha bati, ambacho kiko kama ‘jagi la bati’, kinafaa kwa matumizi ya mahali maalum na si kwa kuhama nacho au kutembea nacho kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kwani ubebaji wake unahitaji nafasi.

Kwa upande wa bei, ‘kit’ moja inauzwa kati ya shilingi 7,000 na 25,000. Bei inategemea na aina ya ‘material’ waliyotumia kutengenezea hicho kifaa. Ukisha nunua kifaa hicho, hasa kama ni cha bati, ni cha kudumu muda mrefu, utalazimika kubadilisha mrija wake ambao ni wa plastiki na koki zake pale unapochakaa, na bei za mirija na koki hizo haizidi shilingi 2000.

Nawasihi nyote kufanya enema kwa afya zenu, ni zoezi ambalo halina madhara yoyote wala halina ulazima wa kufanyiwa na daktari, wewe mwenyewe unapaswa kuwa daktari wa mwili wako kwanza.

No comments: